Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Ngombe zaidi ya 1,332 waliokuwa wanalishwa kwenye maeneo ya hifadhi mkoani katavi wamekamatwa na kutaifishwa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali la kuondoa mifugo yote katika maeneo yaliyohifadhiwa yakiwemo ya hifadhi za wanyamapori na misitu na vyanzo vya maji.
Mkuu wa wilaya ya Mlele Kanali Mstaafu Issa Njiku amemweleza Waziri wa Maliasili na Utalii mh prof Jumanne Maghembe aliyekuwa anafunga mafunzo ya jeshi USU kwa wakuu wa hifadhi na wakurugenzi wa TANAPA kuwa mifugo hiyo ni ya wafugaji waliokaidi maelekezo ya serikali ya kuondoka ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa.
Akizungumza baada ya kufunga mafunzo hayo ambayo ni awamu ya sita ambayo yameshatolewa kwa watendaji 175 wa shirika hilo Waziri Maghembe amewapongeza TANAPA kwa kuonyesha kwa vitendo dhamira ya kupambana na ujangili na akatoa angalizo kwa watendaji wa sekta ya misitu wakiwemo wanaoendelea kufumbia macho ukataji na usafirishaji wa magogo na mkaa katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria.
Akizungumzia tuhuma hizo mwakilishi wa meneja wa Pori la Akiba la Rukwa Lwafi bw Saidi Bilibili pamoja na kulalamikia changamoto zilizopo ikiwemo ya vitendea kazi amesema wanaendelea kukabiliana na matatizo yaliyopo.
Akizungumzia mafunzo ya jeshi USU kwa watendaji wa tanapa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo bw Alan Kijazi amesema hiyo ni sehemu ya mkakati wa kubadili mfumo wa utendaji kazi kutoka wa kiraia kuwa wa jeshi USU na ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwaunga mkono.
Chanzo: ITV