Ng'ombe Hanenepi Siku ya Mnada....!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Kila jambo linahitaji maandalizi. Kuna kisa cha mbweha na mbwa mwitu. Mbweha alishangaa sana kumwona mbwa mwitu akiwa na mazoea ya kunoa meno yake hata kama haendi mawindoni.

Mbweha akamwuliza mbwitu; " Iweje unahangaika kunoa meno yako wakati hutayatumia kuwindia kwa muda huu?"

Mbwa mwitu akajibu: " Kama nitasubiri kunoa meno yangu mpaka siku ya kuwinda ifike, basi, nitashindwa hata kukabiliana na ninayemwinda!"

Naam, ni wachache sana humu duniani waliofuzu mitihani migumu bila maandalizi. Aliyejiandaa vema hupata wepesi katika afanyalo. Tumekuwa tu wavivu sana wa kufanya maandalizi kwa tuyafanyayo.

Hatuna mipango. Wengi wetu tumekuwa tu watu wa kukurupuka asubuhi na kuitazama siku kama ilivyokuja. Tupo tupo tu. Unakutana na mtu mtaani atakwambia; ” Nashuka chini kidogo”.

Yawezekana kabisa huko chini hajui anakwenda kufanya nini. Ukikutana nae tena baadae atakwambia; ” Napandisha juu kidogo”. Usimwulize huko juu anakopandisha anakwenda kufanya nini.

Ndio maana ukisikia kelele ya kibaka mtaani, ghafla watatokea watu kutoka kila kona kumfukuza kibaka huyo. Wengi wa watu hao hawana mipango ya kuifuata katika siku hiyo. Kelele za mwizi huyoo zimewapa kazi ya kufanya.

Ndio, hatuna mazoea ya kufanya maandalizi. Utamkuta Kijana wa Kitanzania amemaliza kidato cha sita au Chuo Kikuu. Hajiweki katika hali ya siku moja anaweza akaitwa kusailiwa kwa nafasi ya kazi. Na ikifika siku hiyo ya kuitwa kwenda kufanya intavyuu, basi, hatolala usiku. Atakesha akijiandaa kwa intavyuu. Kesho yake ataingia kwenye chumba cha usaili akiwa amechoka sana. Yumkini atashindwa.

Ni kama mwenye ng’ombe, ambaye siku ya mnada, ndipo anapokumbuka kumlisha majani ng’ombe wake aliyekonda ili apate bei nzuri mnadani.

Naam, ng’ombe hanenepi siku ya mnada.
Na hilo ni neno fupi la usiku huu.

Maggid,
Iringa
0788 111 765
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
 
hizi sredi za uyu mtu mbona zinadoda hivi jamani??
changieni jamani wadau, sio vizuri hivi mnavyoipita hii sredi jamani.
 
Mwenyekiti sio siri huwa unasema ukweli kabisa japo wengi wetu tu wavivu wa kufikiri na kutafakari,na hapo nimejikuta nikicheka ulipotolea mfano wa mwizi,maana ni kweli kabisa purukushani hizo zinapotokea utashangaa watu huwa wanatokea wapi,na hakuna hata binadamu mmoja anayeweza kuacha sehemu yake ya kazi kwenda kukimbiza mwizi.Big up maggid endelea kutukumbusha wajibu wetu kaka...
 
Last edited by a moderator:
ugonjwa huo hautapona TANZANIA.ofisi nyingi utakuta zina kwasababu ndivyo taratibu zinavyotaka, laki utendaji wa kila siku ni nadra sana kukuta mpangokazi unafuatwa!! labda huko kwenye sekta binafsi.watu wamesoma lakini kutunza muda na kufuata taratibu smartly bado sana.wakati mwingine mpaka tunawakera watu.
 
Mkuu maggid, umenena kabisa wengi hawajitambui,tena kuna huu usemi "ngoja nikapoteze mda kidogo mtaani"
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom