Ngombale Mwiru: Kulikoni Mzee Kujaribu Kumpotosha Rais? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngombale Mwiru: Kulikoni Mzee Kujaribu Kumpotosha Rais?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Field Marshall ES, Dec 22, 2007.

 1. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2007
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Waraka wa Wazi kwa Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, nimesikitishwa na hatua zako za hivi karibuni za kujaribu kumpotosha kwa makusudi rais wetu. Umekuwa mnafiki mkubwa na muongo nambari moja ndani ya CCM, kulikoni? Kutokana na unafiki wako sasa CCM imeanza kupoteza dira za kwenda mbele na hadhi mbele ya jamii.

  Mzee Kingunge, inatia aibu na uchungu kwa mtu kama wewe na wenzako unayejua miiiko ya chama kushindwa kabisa kuishi kwa maadili ya TANU, je unafanya haya kwa kuwa hakuna wa kukuuliza au kwa sababu Mwalimu hayupo tena?

  Umebadilika mpaka sasa unatetea ufisadi ndani ya CCM?  .....Itaendelea..................!


  Source: Mwana-Halisi.
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Dec 22, 2007
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  .............itaendelea lini? nina hamu kukusikia unvyomwaga manyanga
   
 3. M

  Masatu JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2007
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuu mbona unapotea sana? au box kwa kwenda mbele...
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Dec 22, 2007
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Boksi kubwa kubwa siku hizi; mpaka summer ndipo tajiri ataanza kutoa boksi ndogo ndogo.
   
 5. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2007
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu FME endeleza basiiiii.. make umetuonjesha kiduchuuuuuu...
   
 6. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2007
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Tuna hamu kubwa ya kusikia mambo tafadhali.Hili ni jambo la muhimu sana.
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2007
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Huyu ndiye Es mimi ninaye mjua ikija katika issue za Nchi .Siku za karibuni ulikuwa kama JK na CCM sasa naona you are coming back to your sense .Karibu sana na endelea kumwaga maneno ili tujued kulikoni na huyu ajuza .
   
 8. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2007
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kutoa shutuma kwa jina la mtu bila kuzielezea at the very least si jambo la busara na inafanya shutuma zisichukuliwe kama za makini, ingekuwa vyema kama ingewekwa angalau paragraph moja ya kuanzisha shutuma hizo, then the suspense

  I believe somebody here stressed the importance of statistics/data as in "no statistics, no right to say"
   
 9. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2007
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 135
  FM sidhani kama hii issue ungepaswa kuianzia hapa, muandikie kero zako zote uzipost au uziemail kwake then utuwekee copy hapa kwa taarifa tu. I doubt kama kale kazee kanajua kutumia mtandao!!!!
   
 10. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2007
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Wengi tunajiuliza unafanya haya kwa sababu baada ya kuona hakuna wa kukuuliza, kutokana na wenzako wote kufariki dunia, au ni kweli malengo yote ya uhuru yalikuwa ni haya? Mbona mnaendesha nchi kwa kuvunja miiiko na utu wa Mtanganyika? Mbona mnaendesha nchi kwa kusahau ahadi za TANU, mlizozitoa wakati wa kudai uhuru?

  Nimeamua kukusulubu kutokana na wewe kuwa ndiye Mzee pekee uliyebaki ndani ya chama na ndiye uliyekaribu na mwenyekiti wetu rais Kikwete. Kingune, umebadilika mpaka umeanza kuwa bepari na hata kuunga mkono mafisadi? Nasikia siku hizi na wewe ni mfanyabiashara mkubwa sana na unamiliki miradi mikubwa mikubwa ikiwa ni pamoja na kukusanya mapato yatokanayo na ushuru wa kuegesha magari mjini Dar, nasikia unakataa kuwa sio miradi yako, sasa inawezekanaje nyumba ya mfalme ikaajiri kijakazi, halafu kijakazi hicho kikawa sio cha mfalme huyo?

  Mzee Kingune, unaweza kusema hapa wazi jinsi ulivyopewa hizo zabuni? Je mchakato uliendeshwa kwa uwazi na uhalali kisheria zetu? au ulipewa na kushinda kwa sababu wewe ni Kingunge? Au kutokana na kuwa kwako karibu na aliyekuwa mkurugenzi wa jiji? Nasikia umetumbukia kwenye biashara sasa hata neno "UJAMAA" hulitaki tena, limekuwa dhambi kwako kulisema hadharani, Azimio la Arusha, ndio kabisaa hutaki kulisikia, nimekuona kwa macho yangu ukiwatetea mafisadi kwenye mkutano na waandishi wa habari nilishituka na sikuwa na njia nyingine yoyote ya kuwasiliana nawe, ndio nikaamua kukuanidkia kupitia hapa, ambapo najua kuwa mtoto wako mmoja ni mjumbe.

  Bado ninajiuliza huu ujasiri wa kutetea mafisadi umeutoa wapi?


  ......Itaendelea.......!
   
 11. YournameisMINE

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2007
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 2,451
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 145
  ES,
  Mkome nyani giladi huypo babu, mie nashangaa kwanza mpaka leo sijui anafanya nini huko sirikalini. Hakuna la maana alilofanya kwa TZ zaidi ya propaganda zake za mwaka '60............nasubiri kwa hamu muendelezo wa habari hii!.
  Hivi "ufisadi" siku hizi imekuwa fashion nini kwa wana sisiem??
   
 12. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Pamoja na Kingunge kulaumiwa na kutokusikika kabisa katika kukemea tabia mbaya ambayo rais wetu ameikumbatia pamoja na mafedhuli wazulumaji kutoka ughaibuni the buck stops with the president himself. Huu ni wakati wa kuona keki ya taifa inawafaidia Wabongo wote, swala ni Je, JK atamaliza wakati wake kama rais au tutegemee makamu wa rais kuchukua nafasi yake?
   
 13. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #13
  Dec 23, 2007
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Kingunge, unajua jinsi wala rushwa na watoa rushwa wanavyoharibu chama chetu na taifa letu, na wanavyokitia doa kila siku, wakati wa uongozi wetu, rushwa ilikuwa adui wa haki, lakini sasa mtu hawezi kupata uongozi wa taifa bila ya kutoa rushwa kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi. Tulitarajia utamsadia kijana wetu Kikwete aliyezungukwa na mafisadi kila kona, lakini wewe nawe sasa umwekuwa fisadi pia, chama kinaonekana kimeokotwa baada ya wenyewe kuondoka, mbona mzee mwenzangu unashindwa kufikiri hata kidogo kuwa chama na serikali hutenganishwa, na chama hakimtumi kiongozi kuwa fisadi, mwizi, na mtoa rushwa? Na serikali haitumii kiongozi mbatilifu, mpenda makuu je ni sriklai gani inayotaka mtumishi wake awe mpenda rushwa na mfisadi?

  Kwa nini unashindwa kumshauri rais kuitoa hiyo mizizi ya uovu? Yaaani umeshindwa kabisa kumtenganisha na wabinafsi, walafi, wezi, na mafisadi, je hiyo ndiyo sera mpya ya CCM, kuwateua wasafi, lakini wanapofika madarakani wanaanza kuwa wachumia mtumbo yao tu?


  ......Itaendelea....!
   
 14. P

  Pedro Senior Member

  #14
  Dec 23, 2007
  Joined: Nov 17, 2006
  Messages: 114
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wape wape vidonge vyao mze.

  Lakini JK si mtu mzima jamani? mpaka asubiri kuambiwa na watu wanaomzunguka, si afanye kweli nae?
   
 15. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #15
  Dec 23, 2007
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Nadhani mwandishi ametumia njia hii ya kujifanya anamshauri Kingunge kumbe ujumbe ni kwa JK moja kwa moja!
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Dec 23, 2007
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Field Marshall Es,
  Nimependa sana approach yako ktk swala hili. kwanza umeenda direct kwa mtu (mtuhumiwa) bila kuficha na nadhani huu ni mfano bora sana kwetu sisi kuwatia singe hawa viongozi bila kuzunguka zunguka. Ni muda mzuri nasi tutumie kijiwe hiki kusema ukweli kama Dr. Slaa anavyofanya kiasi kwamba wananchi wapate kujua ni nani anayezungumziwa na kafanya mabaya gani na nini athari zake.
   
 17. K

  Kalamu JF-Expert Member

  #17
  Dec 24, 2007
  Joined: Nov 26, 2006
  Messages: 874
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sasa ni kwa vipi watu wanasahau 'vision' ni kuwapata mabillionea 100?

  Hakuna aliyesema hao billionea ni watu wenye sifa gani; na hakuna aliyetaja njia zinazokubalika kufikia ubillionea!

  Naona hapa hata huyo 'mzee mwenzake' naye itambidi akubali kuungana na 'gravy train' kama bado hajafanya hivyo tayari.
   
 18. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #18
  Dec 24, 2007
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kabadilika kama ile treni ya Dodoma ilivyobadili uelekeo na kusababisha maafa ndivyo alivyo Kingunge. Anajiona yeye yupo pale milele, ipo siku utakuwa nje utakuwa ni mmoja wa wahanga kama sisi ukisubiri maamuzi ya mtu kama wewe kwa Rais na ukaona athari zake. Kwa sasa hawa viongozi hawaoni athari za maovu yao kwa wananchi lakini ipo siku nyie mifisadi mtataifishwa mali zenu na kuwa miongoni mwa walalahoi, kama huamini kumbuka baadhi ya mawaziri wa enzi za wewe ukiwa kijana wakati huo ukikimbiza mwenge wa uhuru baadhi wamekufa masikini si kwasababu ya kufilisiwa mali bali kwa sababu wao hawakuchuma lakini hakuna hata waziri miongoni mwenu aliyewazungumzia wakafa masikini. Tunasubiri Kiongozi atakaye kuwa na uchungu na nyie mnaovuna msichopanda, mtanyang'anywa tu.
   
 19. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #19
  Aug 7, 2016
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180

  Babu anahaki kutimka Ccm.
   
Loading...