Ngoma ya kilugwai: Ikichezwa ni lazima pachimbike | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngoma ya kilugwai: Ikichezwa ni lazima pachimbike

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by vukani, Mar 11, 2010.

 1. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Leo nataka niwape za maeneo ya Kigogo Mburahati. Hivi karibuni nilikwenda maeneo hayo ya Kigogo kumtembelea mama yangu mdogo anayeishi maeneo ya Kigogo Mburahati.

  Nilipofika maeneo hayo ya Kigogo, nikakutana na kundi la wanawake likiwa na mchanganyiko wa wasichana na kina mama wakiwa wamevaa sare ya khanga zilizoandikwa maneno ya kimipasho hivi, kwa bahati mbaya sijakariri maneno yenyewe, huku wakiwa na kijingoma kidogo hivi.

  Awali nilidhani labda wanaenda kwenye sherehe fulani, kumbe haikuwa hivyo. Nafikiri kuwa sikuwa mtabiri mzuri.
  Kwa kuwa walikuwa wanelekea njia niliyokuwa nikienda nilifuatana nao wao wakiwa mbele na mimi nikiwa nyuma.
  Wakati wakiendelea na msafara wao mara, akatokea mama mmoja akawauliza, "Haya, leo ngoma ya Kilugwai inarindima kwa nani?"
  Wale kina mama wakamjibu kuwa inaelekea kwa mama Tausina, mpaka hapo nilikuwa sijaelewa kwamba walikuwa na maana gani.

  Tulipofika mbele kidogo wakasimama kwenye nyumba moja na kuanza kumuita huyo mama Tausina na kumwambia kwamba wamekuja kumsuta. Basi kilichotokea hapo ilikuwa ni kurushiana maneno ya kusutana na kupigana vijembe viiingi kati ya pande mbili, kwani hata huyo mama Tausina alikuwa na wapambe wake, na ilikuwa kila wakisema neno wanamalizia kwa kusema, "Halo halooo……. Huku wakipiga kile kingoma kidogo kama kibwagizo.
  Muda wote nilikuwa nimesimama nikishangaa. Ilikuwa ni Burdaaani kweli kweli.
  Kwani tukio lile lilikuwa ni geni kwangu, ama kweli uswahilini kuna vituko vya kila aina.

  Kama mtakumbuka siku za karibuni kuna habari zilisambaa kwenye vyombo vya habari kuhusiana na Bi dada mmoja aliyekodisha matarumbeta kwenda kumsuta shoga yake kule Magomeni, labda kitu ambacho watu wengi hawakifahamu ni kwamba hii ngoma ya Kilugwai ndio ime-Graduate na kuanzishwa huu mtindo wa kusutana kwa Matarumbeta.

  Nilipofika kwa mama yangu mdogo na kumsimulia kuhusu tukio lile, aliniambia kuwa yale mambo ni ya kawaida sana kule mtaani kwao.

  Nikaambiwa kuwa ngoma hiyo ya kusutana ya Kilugwai ilianzia huko Vingunguti na ikaanza kusambaa kupitia Buguruni kwa Mnyamani, kwa Madenge, kwa Makukula, kwa Moto, Buguruni Ghana, Malapa, ikapenya hadi Kigogo, na kuingia Mburahati, kisha ikapitia Tandale kwa Mtogole na hatimaye Manzese hadi Mabibo.

  Kilichonishangaza zaidi ni kile kitendo cha watu kuingia gharama za kununua khanga za sare eti ili kwenda kumsuta mwenzao!!!,
  Hivi tunaweza kusema kwamba watu wana hali mbaya kiuchumi?

   
 2. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Tanzania ina vichaa wengi sana.
   
 3. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Maisha ya uswazi kazi hamna unategemea nn??
   
Loading...