Ngoma London | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngoma London

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Game Theory, Mar 13, 2008.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Tangazo La Shughuli.

  Familia Ya Kina Kilemela Ya Great Ormond Street London, Ina Furaha Kuwatangazia Shughuli Ya Ngoma Ya Binti Zao, Asia Na Fatma Kilemela Itakayofanyika 65 Orde Hall Street, Great Ormond, Holborn, London.


  Shughuli Itaanza :

  27 April 2008 Ndoweka,

  Tarehe 1 May Mbiga,

  Tarehe 2 May Mkole,

  Tarehe 3 May Mkesha,

  Tarehe 4 May Kutoka.

  Hakuna Mchango Wowote Wa Kifedha Unaohitajika.  Sare Ni Khanga Zimeandikwa "hi Hivihivi Tuu", Au Kitenge Cha Wax, Ambavyo Vimeshaagizwa Kutoka Bongo Na Unaweza Kuvipata Kwa £7:50.
  Vanga, Mdundiko, Mkinda Na Gombe Sugu Vimealikwa Kutoka Bongo.kwa Maelezo Zaidi Fika Nyumbani (adress Hiyo Hapo Juu),

  Au Piga Simu Namba 07826007942.


  Kufika Kwenu Ndo Ukamilifu Wa Shughuli Hii.


  Ahsanteni.
   
 2. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  kuna kiongozi anasifika kwa kuchangisha akina mama michango !
   
 3. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  wazaramo wa London hawataki michango mambo hayo waachie hao hao
  sie tutabana hizi income support zetu na pesa za kutuma malori bongo ndio tunapata esa za shughuli kama hizi

  wale wanao lalamika eti wazaramo tunaendekeza ngoma wakajinyonge kwani wao na usomi wao wote mbona mpaka leo watu wanakufa kwa kipindu pindu..eti shule sule hizi kuna mtu alisoma kuliko nyerere na mwishowe akatupeleka wapi

  Mie ndio maana huwa nawaambia hawa ma sista duu kama binti hajachezwa aende huko huko kwa ma bitoz sie ma bwazameni pamoja na yote lazima awe kesha chezwa kama hajachezwa basi asahau na funguo za ile 3 bedroom council flat pale Barnet
   
 4. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Segere Litakuwepo ??
   
 5. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  nimegairi SIJI !
   
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  i hate to admit
  mimi nitakwenda lilwalo na liwe
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Brazameni mbona unatuacha hoi???? Maana weekend bado!

  Je na pilau (Shaba) litakuwepo?
   
 8. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2008
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Blaaadclat...wagwaan?? What the....? Hebu naomba maelezo ya Ndoweka etc ndo nini?
   
 9. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2008
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Duh! Washikaji sio siri hiyo Title ilinistua kidogo "NGOMA LONDON" nikasema sasa tumekwisha na watu mnavyopokezana mademu kama mchezo wa kupokezana vijiti!
   
 10. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2008
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  sikosi japo kuwa sijanunua sare lakini hivyo hivyo tu babu wee,kwa nini nisijukumbushe mwe,wenye wivu na wakale wembe
   
 11. Me370

  Me370 JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 995
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  siko london ila ningekuweko nisingeenda maana siku zote bure ni aghali.
   
 12. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #12
  Mar 13, 2008
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Mkuu Brazameni,

  Kwa kweli umenikumbusha mbali saana.

  Nakumbuka maeneo ya Tandale, Vikindu, Kimansichana, Mbezi( ya Temeke) Kisiju Pwani na Mkuranga kwa ujumla, ambako mambo haya ni muhimu ili kuhakikisha mwali anapotoka basi amewiva.

  Nakumbuka pia mwali siku ile ya kutoka kwamba kama mume ndio hana usafiri basi baiskeli hutumika tena ilionakshiwa kwa mafuta na kupambwa uzuuri!

  Lakini Brazameni , ruhsa imeombwa kwa diwani wa kata ya Holborn? Maana si vibaya wazungu wakialikwa nao waje waone ngoma.
   
 13. Yunic

  Yunic Senior Member

  #13
  Mar 13, 2008
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhhh....kwa kweli Wazaramo mnastahili sifa...Hongereni.

  Lakini me nna swali, hivi kuchezwa kunamfanya binti awe na tofauti gani haswa na sista du? What I mean to say is this: Kama ni mapishi, kwa kweli mwanamke yoyote anaweza kuwa mpishi mzuri, regardless of the background. Kama ni kumridhisha mumewe...this is an art. Any woman can be a good lover. zaidi ya hapo, sio masista du wote wanaohusudu mabitozi, on the other hand, hao wanaochezwa wanaweza kabisa ku-end up na mabitoz. Sasa kulikoni?

  Ukisema hii ngoma ni kukamilisha hatua ya mabinti hao wawili kimila, mie ninakubali. Lakini kuchezwa ngoma does not necessarily make a woman/girl any better in quality. Nina marafiki wengi washachezwa ngoma, na mara baada ya kuwekwa ndani na kutoka huwa hawashikiki!
   
 14. N

  NakuliliaTanzania JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 560
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Mkuu, nikunong'oneze, ulishawahi kulala na msichana aliyechezwa? wajua kwa nini wanawake watokao tanga kwa mfano, soko lao lipo juu?
   
 15. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2008
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Aichee njomba, ebu ninong'oneze na mimi, kasikio nimewekea gundi, kamenata kwa screen.
   
 16. N

  NakuliliaTanzania JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 560
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kaka hapa ni JF sio mahali pake, ila itoshe tu kusema kuwa wakati mtu anaweza kusema kwa ujumla kuwa wanawwake wote waliochezwa na wasiochezwa wako sawa na kwamba suala la ufundi ni la mtu binafsi, jiulize kwa nini hata kama unajua kucheza mpira inabidi uwe na kocha?

  hawa watoto wa mwambao wanafanya vitu vyao kitaalam na ni kwa vile wanachezwa, na wanafanya both theory and practical nadhani mkuu BRAZAMENI atakubaliana na mimi hapa..wamefunzwa kumfahamu, kumkubali na kumuenzi mwanaume, to say the least mkuu! sasa watakani huku duniani kama ni mtu unatafuta mwenza?
   
 17. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2008
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Brazameni, Hayo maandiko tu kwenye hizo Khanga, ni ujumbe tosha kwa Walengwa: HIV i HIV i tuu!!
  Ninaheshimu sana Tamaduni/Jadi za baadhi ya makabila yetu,lakini naelekea kufikiri kuwa hizi NGOMA(Kumtoa Mwali,Mdundiko)zinachangia kwa kiasi kikubwa sana Maambukizi ya VVU Tanzania.( hasa kwa Vijana wetu)
  **Kwa hiyo Anwani tuliyopewa(Residential Area) nina mashaka makubwa sana kama Hiyo 'Shughuli'itafana,labda ingekuwa kwenye Park fulani hivi au Country side.
   
 18. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #18
  Mar 14, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Kila mtu anaweza kuwa mchoraji lakini sio wote wanapaint masterpieces.
   
 19. J

  Jafar JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2008
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Duuuuu inanikumbusha mbali kweli kweli, wakati huo unakibwaya kiunoni, mguuni una zile kengere, na mkwaju ngoma pembeni. Kuna kigoma kidogo dogo kinaintwa "chapuo". Yoyoyo oooh oyi mama inanza mweeeeeeeee
   
 20. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #20
  Mar 14, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli hiyo tittle hata nami ilikimbiza kusoma, nilijua London ngoma nje nje..(HIV/AIDS) haya watani zangu wazaramo, jongolo jangu wa diba mie mwanangu kulumangira na kisamvu......kwa kuwa ni bure siji, maana bure aghali sana

  Ushi
   
Loading...