Elections 2010 Ngoma ikilia sana.... Mgema akisifiwa....

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
Haya Dr. Slaa tunashukuru kwa kutaka kuingiza nchi yetu kwenye mfarakano usiokuwa na maana... kisa umesifiwa sana...

Hili jambo laweza kuondoa credit zote ulizopewa na wananchi nakutakia kila la kheri mkuu.

By the way, dalili za mvua ni mawingu:

---> Maboxi ya hewa ya kura kule Mbeya
---> Kulumbana na Jeshi letu tukufu kwenye vyombo vya habari.
--->
 
Kasheshe,

..yaani mnataka mchakachue kura halafu lawama muelekeze kwa walioathirika na udanganyifu wenu.

..pia hii tume ya uchaguzi si imeundwa na serikali ya CCM? sasa kama hamkuiwezesha kufanya kazi kwa umakini na ufanisi kwanini lawama zake mzielekeze kwa vyama vya upinzani?

..mabilioni ya pesa yaliyotumiwa na serikali na CCM kuhakikisha kwamba mnarejea madarakani yangeweza kutumika vema zaidi kuiboresha Tume ya Uchaguzi.
 
Izo ndo fikra za kdiumu chama cha.......................Zidumu fikra za mwenyekiti...........................
 
Nafikiri wananchi wamesema waziwazi kwamba tumewachoka CCM.Hata kama zitatumika mbinu mbadala za kuhalalisha kutawala, bado CCM haiakuwa ya kwanza. Wapo wengi ambao hata kuongea tu juu ya ubovu au dhuluma za system ilikuwa ni treason tosha na wamekwenda na maji. Sitashangaa kuona siku moja kule kwenye graveyard ya corporate stuffs, CCM ikiwa imelala usingizi wa amani kama haitabadilika na kuanza kuwatumikia wananchi. Ilivyo sasa ni sehemu ya wajanja kula na kuvimbiwa.
 
Haya Dr. Slaa tunashukuru kwa kutaka kuingiza nchi yetu kwenye mfarakano usiokuwa na maana... kisa umesifiwa sana...

Hili jambo laweza kuondoa credit zote ulizopewa na wananchi nakutakia kila la kheri mkuu.

By the way, dalili za mvua ni mawingu:

---> Maboxi ya hewa ya kura kule Mbeya
---> Kulumbana na Jeshi letu tukufu kwenye vyombo vya habari.
--->
Mkuu Kasheshe, huoni kuwa Dr Slaa ameleta changamoto na kuonyesha kwa vitendo ni jinsi gani demokrasia inaweza kutendeka. kasoro zilizojitokeza nadhani ni udhaifu wa taasisi nyingi sana, akiwamo Dr Slaa, na si vema, kwa maoni yangu, kumtwisha yeye mzigo peke yake kama ndio chanzo cha yaliyotokea.
Ndio, anaweza kuwa na lawama kutokana na mambo fulani aliyoyafanya vibaya, lakini amefanya mengi mazuri na kama ukiyaweka katika mizani, kwa maoni yangu. naona yale aliyoyafanya mazuri yanazidi kwa uzito
 
Kasheshe, nadhani ingekua vema ukajua hata kiini cha malalamiko ya Dr. Slaa then ndo umshukuru kwa kutaka kuingiza nchi yetu kwenye mfarakano usiokuwa na maana... kisa ni tofauti ya kura za mawakala wa chama na tume!

By the way, tume ndo chanzo cha yote yaliyotokea na yatakayotokea!
 
Kasheshe ana mtindio wa ubongo kama si roho. Yawezekana ni fisadi au juha mmoja anayejipendekeza kwa mafisadi lau mkono upate kwenda kinywani. Na ulaaniwe Kasheshe who ever you are.
 
Back
Top Bottom