Ngokolo, Shinyanga: Mume ajinyonga kwa mtandio baada ya kugombana na mkewe

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
0f56c392f70ecd58a6de3e716d33a01f.jpg
NB; Askari wakiwa wameubeba mwili wa marehemu Luhende Lusangija.

Mwanamume aliyefahamika kwa jina la Luhende Lusangija (34) mkazi wa Mwinamila Kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga amekutwa amejinyonga nyumbani kwake kutokana na kile kilichotajwa kuwa mke wake alikuwa anauza mali za familia kutokana na mikopo aliyokuwa anadaiwa.

Tukio hilo limetokea Jumamosi Juni 3, 2017 majira ya saa 11 alfajiri, ambapo marehemu akiwa na watoto wake watatu nyumbani, aliamka na kisha kuchukua mtandio huku watoto wake wakiwa wamelala, na kuamua kujitundika kitanzi sebuleni, na kusababisha kifo chake papo hapo.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema, Mwanamume huyo amejiua kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni ugomvi wa siku nyingi na mke wake ambaye siku kabla ya tukio alikuwa ameshaukimbia mji wake.

Wakisimulia tukio hilo majirani zake Safina Javali, alisema marehemu alikuwa na ugomvi na mkewe muda mrefu ambapo kila siku walikuwa wakipigana, kwa madai kuwa mwanamke alikuwa akikopa mikopo, na baada ya kushindwa kuirejesha alikuwa akiuza vitu vya ndani wakati mumewe akiwa safarini kwenye majukumu yake ya kikazi.

"Juzi alipokuja mwanamume kutoka safarini akakuta kitanda kimefungwa kwenda kuuzwa, ili mwanamke alipe deni la mikopo aliyokuwa akiichukua, ndipo ugomvi mkubwa ulipozuka hadi kusababisha mwanamke kuukimbia mji wake na kwenda kusiko julikana", alisema Javali.

Akiongea kuwa baada ya tukio hilo kutokea walimsikia mtoto wake wa miaka 7 majira ya saa moja asubuhi akilia kwa uchungu na kupiga kelele, kuwa baba yake amekufa kwa kujinyonga na walipofika kwenye nyumba na kuchungulia mlangoni ndipo wakamuona amening'inia kwenye paa la sebuleni akiwa ameshafariki.
Naye mwenye nyumba Halima Issa ambapo marehemu alikuwa mpangaji wake, alisema mji huo ulikuwa na ugomvi mara kwa mara na walikuwa wakiwasuluhisha lakini ugomvi wao ulikuwa pale pale, na walipopata taarifa ya kifo chake walifika eneo la tukio kisha kuwasiliana na uongozi wa mtaa ili kufuata taratibu za kisheria.

Aidha Mwenyekiti wa mtaa huo wa Mwinamila Ngokolo mjini Shinyanga Yohana Munisa, alikiri kupokea taarifa za marehemu huyo majira ya saa moja asubuhi, na alipofika eneo la tukio alimkuta Lusangija akiwa tayari amejinyonga, ndipo akatoa taarifa polisi ambapo nao wakafika ili kuuchukua mwili wa marehemu.

Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Elias Mwita alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, huku ndugu wa marehemu wakitafutwa ili kuuchukua mwili huo kwa taratibu za mazishi.
 
Naona statistics za watu kujiua kutokana na mapenzi zina kuwa kwa kiwango cha juu RIP baba chapo uamuz uliochukua aukuwa wa busara
 
Kujinyonga siyo suluhisho. Nahisi huo ni msongo wa mawazo umesababisha yote hayo. Haswa kwa mtu uliyekuwa unampenda sana hukutegemea akufanyie yote hayo.

Nawashauri watu wakiwa kwenye lindi kubwa la mawazo watafute vitu vya kuwasaidia kama kuwashirikisha marafiki, kusali sana na hata kuchukua muda mwingi kuongea na wanao kama mke/ mume amekuudhi watakuwa faraja yako

Unaweza ukakimbiwa na mume/mke lakini watoto watakuwa karibu yako. Kuongea nao tu hata kama ni wadogo ni faraja kubwa sana kwako na kuona kuwa bado kuna uhitaji mkubwa wa kuishi na kuwasaidia wanao waweze kuwa na maisha mazuri na kujivunia kuwa angalau yupo.mzazi mmoja anayewajali.

Kuongea na marafiki hukusaidia kushare experience katika ndoa. Nakuhakikishia Unaweza fikiri kuwa unapitia mambo magumu lakini ukiongea na wenzako utajiona cha mtoto. Kumbe wapo wanaopita mambo makubwa kuliko hayo. Na hii ikakusaidia kufahamu kuwa ni mapito tu mambo yatakuwa vyema.

Kusali sana, hili litakusaidia kuepuka kufanya mabaya kama kujiua au kumwua mwenzako. Maana ukiwa na hofu ya Mungu huwezi kufanya yote hayo. Katika kusali utajikuta hata kama mwandani wako anakuudhi unamuombea ili kama kuna roho chafu zimemuingia zitoke. Na utakavyozidi kumfanyia vyema ndivyo atakavyobadilika na kuwa mtu mwema.

Jamani mke/mume hatukuzaliwa nao. Tumewakuta ukubwani isiwe sababu ya kutuondolea uhai kabisa. Maisha yetu ni ya muhimu sana. Mtu akikuacha mwacha aende na hamsini zake.
 
Back
Top Bottom