Kweni binadamu kufa ni kazi basi! Ila kwenye mikanda ya kiunoni siku hizi hata ukijinyongea ni kazi bure inakatika fasta,ila usipime ya kimasai.Mtandio huo wa china,india au KTM??!!!
Good ideaKujinyonga siyo suluhisho. Nahisi huo ni msongo wa mawazo umesababisha yote hayo. Haswa kwa mtu uliyekuwa unampenda sana hukutegemea akufanyie yote hayo.
Nawashauri watu wakiwa kwenye lindi kubwa la mawazo watafute vitu vya kuwasaidia kama kuwashirikisha marafiki, kusali sana na hata kuchukua muda mwingi kuongea na wanao kama mke/ mume amekuudhi watakuwa faraja yako
Unaweza ukakimbiwa na mume/mke lakini watoto watakuwa karibu yako. Kuongea nao tu hata kama ni wadogo ni faraja kubwa sana kwako na kuona kuwa bado kuna uhitaji mkubwa wa kuishi na kuwasaidia wanao waweze kuwa na maisha mazuri na kujivunia kuwa angalau yupo.mzazi mmoja anayewajali.
Kuongea na marafiki hukusaidia kushare experience katika ndoa. Nakuhakikishia Unaweza fikiri kuwa unapitia mambo magumu lakini ukiongea na wenzako utajiona cha mtoto. Kumbe wapo wanaopita mambo makubwa kuliko hayo. Na hii ikakusaidia kufahamu kuwa ni mapito tu mambo yatakuwa vyema.
Kusali sana, hili litakusaidia kuepuka kufanya mabaya kama kujiua au kumwua mwenzako. Maana ukiwa na hofu ya Mungu huwezi kufanya yote hayo. Katika kusali utajikuta hata kama mwandani wako anakuudhi unamuombea ili kama kuna roho chafu zimemuingia zitoke. Na utakavyozidi kumfanyia vyema ndivyo atakavyobadilika na kuwa mtu mwema.
Jamani mke/mume hatukuzaliwa nao. Tumewakuta ukubwani isiwe sababu ya kutuondolea uhai kabisa. Maisha yetu ni ya muhimu sana. Mtu akikuacha mwacha aende na hamsini zake.
Sizonje unaua hadi ngosha, hali ingekuwa nzuri mke asingefikiria kuuza kitanda.
Anafadhaisha kabila la kisukuma.....hawanaga ujinga kufikia kiasi hiki, huyu aliyejinyonga anatupa wasiwasi sana...wasukuma nao wameanza ujinga huu lini...
Kwanini mke akope? Jibu ni moja tu; alikuwa haachiwi Pesa za kutosha mahitaji ya familia ya watu watano. Kwa maana nyingine yeye marehemu ndio sababu ya yote japo ameyakimbia majukumu kiana na kumwachia mkewe. Tutegemee idadi ya watoto wa mitaani kuongezeka.
Ila kwa hawa viumbe inabidi kuishi nao kwa akili sana, ukilegeza kamba yatakukuta ya aibu. Km huyo ndg yetu aliyejinyonga....Bwihi
Mkuu fahamu kuwa Ujinga hauna kwao..!