Ngoja niwahusie vijana, kuwa msomi ni tofauti na kuelimika

Kua msomi, ni tofauti na kuelimika.

Na unapoenda kusoma tarajia kupata maarifa ambayo ndio yatakua silaha yako kuelekea ama kufikia mafanikio huku mitaani.
Sorry..

Ninacho jaribu kumaanisha hapa nikwamba, unapo hitim chuo usitarajie kwamba cheti chako kitabadilika na kua fedha, bali unapaswa kutumia maarifa ili upate kutengeneza fedha.

Naomba niwaulize vijana, hasa wanao hitimu vyuo na kurejea mitaani.

Je, mlishawahi kujiuliza kwamba kwanini Serikali ama Bank haiwakopeshi fedha za mitaji kwa dhamana ya vyetu mara tu mnapohitimu vyuo..?? Sio lazima mnijibu hapa. Lakini ninachowasihi ni kwamba acheni vilio na punguzeni lawama, mnapaswa sasa kuzivua aibu na achaneni na mawazo ya kuchagua kazi/vibarua na punguzeni uvivu.

Kijana wa sasa anaweza akafanya shuguli yoyote halali hata kama ni dirty job, ilimradi kama kijana umejiwekea malengo lazima utafikia malengo ama pale unapotaka.

Bado nawasihi vijana muache tabia za kuamka na kusema hauna la kufanya, hauna pakwenda, hauna connection, hauwezi kubeba zege, hauwezi kuuza matunda, huwezi kupiga debe, hauwezi kulima mbogamboga nk:

Vijana punguzeni kuwalaumu wazazi, marafiki, Serikali, ndugu na jamaa. Bado nawashauri kupunguza ulevi, matumizi ya social networks ambayo hayana faida na kadhalika.

Badilikeni vijana, pengine wengi hamto upenda ushauri wangu hapa, na bilashaka wapo mtakaoanzisha lawama tena hapahapa kwa kuyarudia yale nilioyasema.

Asanteni, kwa leo yatosha...
Dah ubarikiwe mkuu.
Am not one of those wahitm wapya ila ushauri wako umenigusa.
 
Sawa mkuu...
Ebu niambie kwa hoja ili nami nijifunze kutoka kwako, yaani mfumo umefanyaje..??
Niseme tyuuh hivi, mfumo wa Elimu hapa kwetu upo kwa ajili kumtengeneza muhitimu kuajiriwa, na sio kujiajiri.
Hope umeelewa, vingnevyo wengine watakuja kudadavua zaidi.
 
Niseme tyuuh hivi, mfumo wa Elimu hapa kwetu upo kwa ajili kumtengeneza muhitimu kuajiriwa, na sio kujiajiri.
Hope umeelewa, vingnevyo wengine watakuja kudadavua zaidi.
Okay, nimekuelewa vizuri.
Sasa kama tayari basi umesha gundua tatizo lilipo, basi ndio badala yake nikaandika uzi kama huu.
Ninacho maanisha hapa ni kwamba, kama tayari tunao mfumo wa hovyo, badalayake sasa wahitimu/vijana wafanye Jambo/wachukue hatua mbadala na wasikae na kuanza kulalamikia mfumo.
Kumbuka maisha lazima yaende na dunia haisimami kungoja mtu no matter what.
 
Back
Top Bottom