Sir Khan
JF-Expert Member
- Jul 28, 2018
- 5,243
- 9,572
Habari zenu ndugu zangu Wagalatia?
Leo nimemkumbuka mtu wa mwisho aliyenishushia kichapo cha coco dog (mbwa koko), ilikuwa huko shuleni Kisimiri Arusha siku moja kabla ya Necta tulibambwa na mwalimu wa nidhamu wakuitwa Bon tukiwa tunasikiliza redio kwenye simu ya jamaa mmoja tukapelekwa staff room na kuanza kuulizwa kwanini tumekaa na mtu mwenye simu bila kutoa taarifa kwa walimu hili akamatwe basi tukawa tunajibu bila wasiwasi tukijua keshokutwa ni mtihani wa taifa so hatuwezi kupigwa eeeeh bablai tulishushiwa kichapo kizito kila mtu alipata nusu dazeni ya mboko zenye lishe kiasi kwamba hadi namaliza mtihani mapaja yalikuwa yanauma balaa.Baada ya mtihani tukaambiwa tubaki shule mpaka wiki inayofuata kwa ajili ya mahafali,nikaona hawa wananitafutia kesi ya uhujumu uchumi nikatoka nduki usiku hadi leo kivuli changu hakijawahi kuonekana maeneo yale japo bado naipenda shule yangu Kisimiri.
Tupe stori yako nani alikuwa mtu wa mwisho kukutia mboko na ilikuwaje?