Ngoja kwanza,unamkumbuka mtu wa mwisho kukutia mboko(bakora)? Ilikuwaje?

Sir Khan

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
5,128
2,000
Habari zenu ndugu zangu Wagalatia?
Leo nimemkumbuka mtu wa mwisho aliyenishushia kichapo cha coco dog (mbwa koko), ilikuwa huko shuleni Kisimiri Arusha siku moja kabla ya Necta tulibambwa na mwalimu wa nidhamu wakuitwa Bon tukiwa tunasikiliza redio kwenye simu ya jamaa mmoja tukapelekwa staff room na kuanza kuulizwa kwanini tumekaa na mtu mwenye simu bila kutoa taarifa kwa walimu hili akamatwe basi tukawa tunajibu bila wasiwasi tukijua keshokutwa ni mtihani wa taifa so hatuwezi kupigwa eeeeh bablai tulishushiwa kichapo kizito kila mtu alipata nusu dazeni ya mboko zenye lishe kiasi kwamba hadi namaliza mtihani mapaja yalikuwa yanauma balaa.Baada ya mtihani tukaambiwa tubaki shule mpaka wiki inayofuata kwa ajili ya mahafali,nikaona hawa wananitafutia kesi ya uhujumu uchumi nikatoka nduki usiku hadi leo kivuli changu hakijawahi kuonekana maeneo yale japo bado naipenda shule yangu Kisimiri.
Tupe stori yako nani alikuwa mtu wa mwisho kukutia mboko na ilikuwaje?
 

Njemba Soro.

JF-Expert Member
Oct 5, 2013
1,588
2,000
KISIMIRI ulikuwa pale mwaka gani aisee??? NILISOMA A-LEVEL PCB PALE MAHALI..... dah, shule yangu kisimiri. Mara ya mwisho kula mboko ilikuwa shule moja inaitwa umbwe secondary nikiwa form one tulitoroka kwenda kunywa mbege na dadii.... tulipigwa lakini tukasamehewa hatukupewa barua...
 

Sir Khan

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
5,128
2,000
KISIMIRI ulikuwa pale mwaka gani aisee??? NILISOMA A-LEVEL PCB PALE MAHALI..... dah, shule yangu kisimiri. Mara ya mwisho kula mboko ilikuwa shule moja inaitwa umbwe secondary nikiwa form one tulitoroka kwenda kunywa mbege na dadii.... tulipigwa lakini tukasamehewa hatukupewa barua...
2016-18
Mkuu mbona Kisimiri hakuna PCB we ulisoma mwaka gani?
Unamkumbuka mzee Kisongo?
 

comred

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
1,871
2,000
Nakumbuka Pale Oldmoshi sec..nilikula zangu 4 kabla yakuanza pepa ya necta ya final..
Sababu sikuwahi kuonekana shule hadi siku ya mtihani wa taifa..2008
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom