Ngo ngo ngo hodiii bishoo la kitaa nimetinga JF

Yaan kama kawa kama kawiz...kama kala mbwanda kama mbwai mbwai tuu unaambiwa wadau mambo ajee, wakubwa shikamoo wadau wote mnaombwa mnipokee msela wenu, nimetimba jf kwa ajili ya kukiwasha tuu, muda mrefu nilikuwag naisikia tu jf redioni na mitandaoni. Ninavyojua Jamii forum ni jamvi huru linalowakutanisha watu wa kada anuwai, watu wenye mawazo chanya kuielekea jamii kama sivyo mnijuze ila nina ka swali ka kizushi eti nasikia mpaka vigogo na viongozi wazito wa serikalini! wapo humu Jamvini! sasa kama ni kweli the great thinkers sijui mtanisaidiaje nionane nao maana nina mengi ya kuwaeleza, lakini kwa haraka haraka sababu zilizonifanya nijiunge jf ni

1.Kupata habari mbali mbali, matukio na mambo na vijambo.Yanayoendelea duniani.

2.Burudani mbali mbali, vituko, viroja na vimbwanga kupitia jukwaa la burudani.

3.kuongeza ufahamu na kupata elimu ili kuweza kuwa bora(self-development) kupitia jukwaa la elimu na mengineyo.

4.Kupata fursa ya moja kwa moja kushiriki katika mijadala mbalimbali ihusuyo jamii yetu, nami kushiriki kwa kutoa maoni yangu kwani watanzania tuna haki ya kutoa maoni ni haki yetu kikatiba.

5.kutafuta mke maana natarajia kuoa nikimaliza shule umri wangu ni miaka 19.nasoma A level na mwaka huu ninapiga pepa ninayaandika haya nikiwa shuleni.tumemaliza mitihani ya midterm.

Naomba kuwasilisha.
Kenge ww Toka hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom