Ngeleja yuko TBC live anazungumzia mambo ya umeme

Eti nini??? Ama kweli hili ni janga la taifa kama tuna watu wenye akili kama hizi.........hao jamaa wa tanesco ni lazima watakuwa kaitaka moja kati ya haya matau (i)Wanaiba umeme (ii)Wanaishi kwenye nyumba za serikali wasizolipia umeme (iii)Wanapewa vocha unit za bure kila mwezi.

Maana mtu anayelipa hela zake kununua umeme asingeweza kusema haya, na inawezekana aliyasema hayo huku akiwa na tabasamu
nani alikuambia watu wa tanesco wanalip bill za umeme? wale wanapata free electricity. unakuta mtu amewekewa unit 16000 za umeme wa luku, unategema aongelee suala la ongeeko akiwa amenuna? alikuwa anachekelea kuliko kawaida...
 
Taratibu gani sasa huyo jamaa yupo serious kweli?
kuhusu maandamano, anasema wananchi lazima wapwe wanapewa taarifa sahihi kama vil kuambiwa ongezeko la bei. anasema euwra iliwashirikisha wananchi ktk maamuzi hayo.
anasema tukiandamana tutakuwa tunaharibu taraibu zilizopo
 
eti anasema netgroup walikuwa wao hawawekezi bali kuvuna tu, ndio maana mpaka yakajitokeza mambo ya richmond na dowans...umeme wa dharura.!!

Kwa hiyo kwa kifupi ni kuwa waliosaini mkataba na Netgroup walisaini mkataba wa kulihujumu taifa..........asante sana Ngeleja kwa kukiri hili maana siku nyingi sana wenzako wamekuwa wakilikanusha na kusema eti Netgroup walisaidia tanesco.......ingekuwa China hawa wote wangelishakuwa marehemu
 
Back
Top Bottom