Ngeleja na wakubwa wenzake wanashare Tanzanite One!!?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngeleja na wakubwa wenzake wanashare Tanzanite One!!??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MPadmire, Apr 29, 2012.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Huko Arusha katika Hotel ya Mount meru, yanaitwa Gems, jewelry and Mineral Fair East and southern Africa.

  Kumbukeni kuwa mwaka 2009 ilipitishwa bungeni kuwa madini yote ya Vito yachimbwe na wenyeji na yakatwe inchini.

  madini ya vito ni Tanzanite, Rubi, Sapphire, Diamond n.k

  Bunge liliamua kuwa Tanzanite one waondoke mwaka 2013.

  Wakati Tanzanite one wanaanza kuchimba, ilitokea migogoro mingi sana kama wachimbaji wadogo kupigwa risasi, Wafanyakazi kukaguliwa kwa X ray mbaya sana.

  Pia iliaminika kuwa Tanzanite One ilikuwa na maslahi kwa Kigogo fulani ambaye alipewa Hotel South Africa.

  Kwa sheria ya Bunge Tanzanite One ilitakiwa iondoke mwaka huu na kuachia KITALU C kwa wazawa. Kitalu C ndo kikubwa sana na kina madini mengi

  Sasa kwa historia hiyo hapo juu, turudi kwenye heading. Imethibitika kuwa mwaka huu kuwa Tanzanite One imeuza share kwa wajanja wachache (Vigogo) na itaendelea kubaki nchini.

  Sitaki kuwaaminisha, kila mtu afanye uchunguzi na habari iwekwe wazi wananchi wajue.
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hilo ni la kweli na mimi nimepata kusikia taarifa hizo. Ngoja tuendelee kuyachimba tutawaanika tu hapa.
   
 3. m

  massai JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kama mwanasheria ni riziwani unategemea kutakua na nini kipya hapo?hii nchi ni ya kifamilia hakuna kitakachoendelea mpaka walioko madarakani wapelekwe segerea au wanyongwe ndio mambo yataenda sawia
   
 4. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mbona hilo lina fahamika japo sio kiivyo, Ami ana shikilia maslahi ya wakubwa wetu ndio maana wana uhakika wa kuendelea kumiliki kitalu C japo mkataba wao unapaswa kuisha 2012, sasa hivi kampuni imekuja kwa staili ya Richland Resources Ltd. Lakini wananchi tukikomaa na wabunge wetu bila kujali maslahi ya vyama hasa cha magamba hawa jamaa lazima waondoke.
   
 5. O

  One Man Army JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mamaaa subiri nimshtue zitto sasa hv..
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Huyo Ami alituuza South Africa badala ya kutuwakilisha kule! Akauza nchi na akaacha ubalozi na kurudi akiwa na share kila kampuni y south aftica iliyowekeza hapa nchini. Sijui kwa nini hakukumbwa ni ile dhana ya conflict of interest yaani badala ya kuwakilisha nchi unajiwakilisha mwenyewe.
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Jaman jaman jaman,
  nina imani mamia ya wabunge kwa sasa WANAHANGAIKA KWA WAGANGA WA KIENYEJI WAPATE UWAZIRI,
  UKIWA WAZIRI HAPA TZ TUNASEMA
  'UMEULA'
   
 8. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Wajinga ndiyo waliwao. Tumekuwa wajinga sana. Rais mjinga, waziri mjinga, mbunge mjinga na mwananchi naye ni mjinga. tuamke tutetee nchi yetu.
   
 9. T

  Tiger One JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 569
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Laurence Kego Masha, a new Director & share holder, Kahama Gold Mines, Leagal Depertment.

  IMMMA Advocate, Leagal advisor & consultant Tanzanate One.
   
 10. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,569
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kama ulaji ndio huu basi kweli uwaziri dili! But we need changes Mawaziri wawe watumishi wa wananchi siyo wezi wa wananchi, sijui tunaliona hili kweli?
   
 11. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  watu wa sengerema mpo?? Mnajisikiaje kuwakilishwa na ngeleja mwizi, fisadi, mhujumu wa uchumi wa tanzania bungeni? Natumai mnajivunia kwani ndo mlimpa kura 2005
  hati mlimpitisha bila kupingwa leo anachangia kutuongezea uaskini wa tz, shame on your faces na muende mkatubukanisani pia misikitini kwa kutuletea mtu fisadi katika uongozi na waakikishia mungu anawaona kwa maamuzi yenu........
   
 12. Epason

  Epason JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 427
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Si Ngeleja tu hata Olenaiko ni board member. Na madini bado wanasafirisha yakiwa hayajakatwa ila wanakata yale mabovu kuzuga watu. TMAA wapo pale kama picha kwani kuna data muhimu hawapewi. Mtandao ni mkubwa mpaka juu. Ama kweli nchi imeinamishwa.
   
 13. M

  Moony JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nadhani kuna siku nilisema... kuhusu makampuni yaliyo chini ya wizara yake
   
 14. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Sasa wananchi wa Arusha anzeni kufanya uchunguzi kujua ukweli, halafu sasa kuweka mikakati jinsi ya kudaihaki zenu. iwe kwa maandamano ama njia nyingine.

  Christopher Ole sendeka ni kinyonga, amegeuka na kuwa upande wa ufisadi ghafla, Je nani atawasaidia wananchi wapewe vitalu?
   
 15. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Vipi One Man Army, umeshampa Mh. Zitto taarifa?
   
 16. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #16
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  hapa unataka kutueleza kuwa tatizo ni nini?, unakiri kuwa owners wa mwanzo waliokuwa wageni waliondoka na kuwauzia wazawa, unataka/ulitaka mmiliki awe nani ili ufurahi?, ulitaka imilikiwe na wamasai wote chini ya chifu wao. Unakiri kuwa share ziliuzwa; do you mean utaratibu wa kuuza share haukueleweka?!, ulitaka kampuni na malizake zigawiwe free kwa nyoka?. Kimsingi sijaelewa tatizo unalotaka ku-adress.
   
 17. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #17
  Jul 21, 2012
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Shamba la Bibi linafunwa.
   
Loading...