Ngeleja na Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngeleja na Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Aug 22, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,203
  Trophy Points: 280
  Waungwana

  Baada ya ripoti ya madini kutolewa JK alimpa Ngeleja wiki mbili ili aipitie na kutoa mapendekezo yake. Hiyo ilikuwa June, 2008 kama sikosei. Ngeleja akadai kwamba mapendekezo yake kuhusiana na ripoti hiyo hasa katika umiliki wa Kiwira na mikataba madini isiyo na maslahi itatolewa Bungeni baada ya kupata ruhusa kutoka kwa spika Sitta ya kufanya hivyo.

  Pinda naye alitwambia kwamba atazungumzia jinsi serikali itakavyoyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na kamati ya Richmond Bungeni baada ya kupewa ruhusa na spika Sitta.

  Naona miezi inakatika tu na Sitta hatowi ruhusa hiyo! Je, kulikoni? Au ndiyo usanii wa mafisadi katika kuifilisi Tanzania yetu ukiendelea bila woga?
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145


  Jana walirusha jiwe lao la mwisho maana JK kaamua kufunika na kuwazuia wabunge kujadili jambo hilo tena na siamini kama Sitta ataruhusu
   
 3. Lady Capricorn

  Lady Capricorn Member

  #3
  Aug 22, 2008
  Joined: Jun 23, 2008
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante Bubu, nilikuwa na hofu kwamba mjadala wa hotuba ya rais itafunika ripoti hizi mbili muhimu kutoka kwa watendaji. labda kweli Speaker na mawaziri hao wawili wanatafuta mbinu ya kukwepa kutoa ripoti zao bungeni. umebaki muda mchache sana...
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Expect nothing than maneno ya kukwepa ukweli kama yale ya EPA
   
 5. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Pinda is already into the system and he is playing according to the rules.Talk and you are over and done with!he knows the Richmond Villains can put whoever they want in power coz they have the means and resources to do so!
  Its pure mendacious coz no one will ever pay for their misdemeanors!
  We have lost the war and they are doing it their way!
   
 6. Lady Capricorn

  Lady Capricorn Member

  #6
  Aug 22, 2008
  Joined: Jun 23, 2008
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I like to keep an open mind. sitaki kuweka maneno midomoni mwao, if they prove to be useless so be it.
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa mujibu wa ratiba mpya ya Bunge iliyotolewa juzi, hakuna masuala ya Richmond wala Ripoti ya madini
   
 8. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #8
  Aug 22, 2008
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  JF Kama inaweza kusaidia, Taarifa sahihi ni kuwa Taarifa ya Kamati ya Bomani ilipelekwa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini. Leo Mhe. Speaker ameelekeza kuwa kuitendea haki Taarifa hiyo, inahitaji kwa peke yake angalau siku 2, na kwa kuwa muda utakaokuwa umebaki baada ya Finance Bill Jumatatu, Appropropriation and Excess Vot, ni siku ya 27/8 na 28/8 huenda zitatumika kwa hoja binafsi za Wabunge(Kama zitakuwepo) pamoja na Taarifa ya Richmond na pia kujadili 'Hotuba ya Rais" kabla haijapoa! Tarehe 29/8 Bunge linaahirishwa. Kama itawasaidia kwa kufuatilia hii inaweza kuwa ratiba kwa siku zinazofuata juma lijalo.
   
 9. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kusema kweli mimi binafsi ninamheshimu sana Mh Pinda lakini kwa kauli zake tangu ashike madaraka ya Uwaziri Mkuu, nimeanza kuingiwa na wasi wasi hata hivyo baada ya kuwaza na kuwazua nikaona wakati ule Pinda alitoa ahadi tamu sana ili "kuimarisha kiti alichokabidhiwa akalie" sasa naona kimekomaa ameanza kutugeuka.
   
 10. Lady Capricorn

  Lady Capricorn Member

  #10
  Aug 22, 2008
  Joined: Jun 23, 2008
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bubu, si sahihi kutegemea kwamba mtu mmoja anaweza kubadilisha system yote ya serikali. Hata kama Pinda personally ni mtu mzuri, bado ni kada wa chama tawala na yumo ndani ya system, tena toka enzi za Nyerere. Ni yale yale ya kumpa Kikwete asilimia kubwa ya kura tukitegemea mabadiliko as though he is the second coming of Christ. haiwezekani, tuwe realistic.
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,203
  Trophy Points: 280
  Hmmm! Kauli zako inaelekea na wewe umo kwenye mtandao. Tuwe realistic mpaka lini? :confused:
   
 12. F

  Fisadi Mtoto JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 639
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mimi sioni huo ubora wa Pinda,nini ambacho amekifanya mpaka sasa ambacho ni mark ya uongozi wake.Mbaya zaidi huyu jamaa sio aggresive kabisa,na ngoja tuone kama walau hizo zahanati walizosema zitajengwa kila kata kama kweli zitawezekana lakini kwa Lowasa zingejengwa.
   
Loading...