Ngeleja na giza lililomshinda Mkapa, Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngeleja na giza lililomshinda Mkapa, Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 1, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,209
  Trophy Points: 280
  Ngeleja na giza lililomshinda Mkapa, Kikwete


  [​IMG]
  Na Saed Kubenea - Imechapwa 29 December 2010


  [​IMG]


  WAZIRI wa umeme, William Ngeleja ameomba kufutwa kazi. Asipofutwa na mtawala atafutwa na wananchi.
  Akizungumza kupitia kituo cha televisheni cha taifa (TBC), Alhamisi iliyopita, Ngeleja alisema, “Tatizo la uhaba wa umeme nchini litamalizika ndani ya miaka mitatu kutoka sasa.”
  Akarejea tena kauli yake ya siku za nyuma, kwamba, “Serikali imejipanga kumaliza tatizo la umeme nchini; muda si mrefu mgawo wa umeme utabaki historia.”
  Kauli ya Ngeleja imekuja siku tatu tangu Shirika la Umeme la taifa (Tanesco), kutangaza mgawo mpya wa umeme ambao utaathiri mikoa yote inayopata umeme kupitia gridi ya taifa.
  Mgawo wa sasa, umetokana na kuzimwa kwa moja ya visima vinavyozalisha gesi vya kampuni ya Pan African Energy (PAE).
  Kama Ngeleja angekuwa mkuu wa kitengo cha porapaganda ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), labda angeeleweka. Tungesema anacheza “mchezo wa kisiasa.”

  Ngeleja na giza lililomshinda Mkapa, Kikwete | Gazeti la MwanaHalisi
   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  William Ngeleja ni kihiyo, makamba type
   
 3. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Huyu dogo hakuna kitu anacho fanya dhidi ya ku enjoy uwaziri. Kwanza anapenda kujirusha sana ni Masha type.
  Wana kundi lao linaitwa Victorious wanajifanya ni young CEO's and Executives. Shauri yako siasa si lele mama angalia mshikaji wako sasa hivi analewa tu Rose garden na Giraffe Hotel.
   
Loading...