Ngeleja: Mauzo ya madini yameongeza pato la taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngeleja: Mauzo ya madini yameongeza pato la taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tume ya Katiba, Apr 7, 2012.

 1. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Wakuu tusipende kukosoa serikali tuuu, kuna taarifa njema toka kwa Mh. Ngeleja na ni mwelekeo mwema wa CCM tanganyika.

  Ngeleja: Mauzo ya madini yameongeza pato la taifa

  SERIKALI imesema fedha za mauzo ya madini zimeongezeka kutoka Dola 26.6 milioni za Marekani hadi bilioni moja kwa mwaka.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa kuzindua Bodi ya Ushauri wa Madini, Waziri wa Nishati na Madini, Willium Ngeleja alisema, sekta hiyo imekua kutoka asilimia 7.7 hadi asilimia 10.7.

  Alisema mauzo ya madini nje ya nchi yanaongoza kwa kufikia asilimia 52 ya mauzo yote na kwamba pato la taifa kutokana na sekta hiyo limeongezeka kutoka asilimia 1.4 hadi kufikia asilimia 2.7.

  Alisema uchimbaji unaoendelea nchini hivi sasa unafanyika kwa asilimia 10 tu ya rasilimali zilizopo na kwamba kuanzia sasa serikali itakuwa inamiliki hisa katika migodi ya kati na mikubwa.

  “Tanzania bado ni nchi changa katika uchimbaji wa madini , hatuna zaidi ya miaka 15 hivyo hatuwezi kujilinganisha na nchi nyingine kama Afrika Kusini ambayo ina zaidi ya miaka 100,”alisema Ngeleja.

  Alisema pia wametenga jumla ya hekta laki tano katika maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya wachimbaji wadogo wa madini.

  Kwa mujibu wa Ngeleja mballi na hekta hizo pia wameanzisha utaratibu wa kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa kuanzisha vituo vya kuwakopesha na kuwakodishia vitendea kazi.

  Alisema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana zaidi ya leseni 27,000 zilikuwa zimetolewa kwa wachimbaji na watafutaji madini huku leseni 20,000 zikitolewa kwa wachimbaji wadogo.

  Alisema leseni kwa ajili ya watafutaji wakubwa zilitolewa 6,093 na kwamba muda wa leseni ndogo za madini umeongezwa kutoka miaka mitano hadi saba.

  Pia aliongeza kuwa madini ya vito yatachimbwa na Watanzania pekee isipokuwa kama uchimbaji huo utahitaji mtaji mkubwa na teknolojia ya kisasa na kwamba wageni wataruhusiwa kuingia ubia kwa hisa zisizopungua asilimia 50.
  Kwa upande wa mikataba alisema , kuanzia sasa itakuwa inapitiwa kila baada ya miaka mitano.

  Naye Mwenyekiti wa bodi hiyo yenye wajumbe tisa, Richard Kasesela alitoa ushauri kwa wachimbaji wadogo kuzishirikisha serikali za vijiji ziwe na hisa ili kuondoa mgogoro kwenye eneo husika linalochimbwa
   
 2. K

  Kanundu JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 891
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapa ndipo unapoona kwamba serikali hii ina mawaziri vilaza wa kutupwa. Eti tuna miaka 15 tango tuanze kuchimba madini. Hivi hata historia ya uchimbaji madini tanzania haijui. Hivi uchimbaji wa Almasi Mwadui hajui ulianza miaka gani? Hivi hajui Gypsum ya pale Mkomazi Tanga ilianza kuchimbwa miaka ipi? Hivi hajui uzalishaji wa chumvi Uvinza kigoma ulianza lini? Pamoja na machimbo haya kuwa machache, bado yaliweza kusaidia taifa la watanzania kiasi kwamba kila mTanzania wa wakati huo alisoma bure, kupewa transport warrant kwenda na kurudi shuleni, matibabu ya bure na ya uhakika.

  Ni wakati muafaka kwa waTanzania kupigania nchi yetu ili tuondokane na hawa wakoloni weusi, ambao kila kukicha wanafikiri mbinu za kuwafanya wao waendelee kutudhulumu ni kutudanganya kila siku.

  LAZIMA SASA TUSIMAME KIDETE.
   
 3. G

  Godwine JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2012
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
   
 4. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Halafu zimetumikaje?
   
 5. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Tatizo kwanini iwe leo au mwaka huu? Unajua ni kiasi gani kimeshachimbwa na ni reserve gani iliyobaki? Hii sekta ilitakiwa iwe ya kwanza tangu zamani.
  Nadhani wamefanya hivyo baada ya pato kutokana na utalii kushuka ndio maana wanaitolea mimacho Arusha mjini.
   
 6. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
   
 7. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Unachotakiwa kuelewa ni kuwa mapato yameongezeka FULL STOP.
   
 8. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #8
  Apr 7, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  eti eeeeeh!
  Mali bila daftari.............
   
 9. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #9
  Apr 7, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Sasa hiyo nyongeza ya kipato iliyoongezeka kutokana na madini ipo wapi? Mbona hali ya uchumi ya nchi pamoja na wananchi inazidi kuwa mbaya?
   
 10. L

  LOVI MEMBE JF-Expert Member

  #10
  Apr 7, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,121
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  w. ngeleja. hvi wewe unatumika au unatumiwa. kuna uhusiano gani kati ya ongezeko la mauzo ya madini na walalahoi watz? uwezo wa serkali kuendesha shughuli zake . usifikiri kwa kuwa wewe na familia mnapewa stahili yenu kuwa ndio kipimo cha ongezeko la mapto ya madini. nahisi hongo ndio zinakupelekea uongee namna. sisi tunauchungu kamshahara nakolipwa na majukumu niliyo nayo ni kama mchana na usiku. tatizo wewe hutofautishi misheni town ulipokuwa mtaani na sasa ukiwa waziri. HABARI JAMANI. ACHA HIZO DOGO
   
Loading...