Ngeleja kaudanganya umma, kilichotokea Sengerema kwa uongozi wa CHADEMA wilaya ni hiki hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngeleja kaudanganya umma, kilichotokea Sengerema kwa uongozi wa CHADEMA wilaya ni hiki hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jan 9, 2012.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  CHADEMA yamuumbua Ngeleja

  • Adaiwa kupokea viongozi ‘hewa'


  na Mwandishi wetu

  UPEPO wa mafanikio ambao kwa wiki nzima iliyopita ulionekana kumwendea vema Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, jimboni kwake Sengerema, umebadilika ghafla baada ya kubainika kuwa watu aliowatangaza kuwapokea kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo ni viongozi hewa.


  Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima na kuthibitishwa na uongozi wa CHADEMA, ngazi ya taifa na wilaya, ambao umelazimika kutoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari, umebaini kuwa mbunge huyo alimtangaza Ayub Malima kama mwenyekiti wa chama hicho pinzani wa wilaya ya Sengerema ambaye alikuwa amehamia CCM, huku akijua kuwa alikwishafukuzwa siku nyingi.

  Taarifa za uhakika zimebaini kuwa Malima alivuliwa uongozi na uanachama wa CHADEMA tangu Julai 20, 2010, katika mkutano mkuu ulioitishwa kujadili utovu wa nidhamu wa kiongozi huyo.

  Aidha imedaiwa kuwa Malima ni rafiki wa siku nyingi wa Ngeleja na kwamba kulikuwa na mipango ya chini kwa chini ya watu hao wawili ambayo iliponaswa, ikawa chanzo cha kutimuliwa kwake CHADEMA.

  Habari zimebainisha kuwa Malima alifukuzwa baada ya kubainika kuwa alikuwa na mipango ya kujipatia fedha kutoka kwa Ngeleja aliyekuwa akiwania ubunge kupitia CCM ili amsaidie kumwangusha mgombea ambaye angesimamishwa na CHADEMA.

  Jana Tanzania Daima ilipokea taarufa rasmi ya CHADEMA ambayo imebainisha kuwa lengo la watu hao wawili, Ngeleja na Malima, lilikuwa kufanya kila njia inatumika, kuhakikisha anapita bila kupingwa akiogopa kubwagwa.

  "Kwa umakini wa CHADEMA kiliweza kujua hata mipango ya hujuma hizo ilipokuwa inafanyika katika moja ya hoteli mjini hapa iliyoko Barabara ya Kamanga. CHADEMA ilikuwa na ushahidi mkubwa juu ya njama hizo, ikiwemo sauti zilizorekodiwa na hata wajumbe aliowaita ili wamsaidie kufanikisha suala hilo, bahati nzuri walikuwa waaminifu na wapambanaji wa kweli, hivyo walileta taarifa zote," ilisema sehemu ya taarifa ya chama hicho jana kwa gazeti hili.

  CHADEMA ilisema kuwa baada ya wajumbe kumvua uanachama Malima, kamati ya utendaji ya jimbo la Sengerema ilimteua Saidi Shabaan kukaimu nafasi ya mwenyekiti wa wilaya ambaye anaendelea kukaimu hadi leo.

  Aidha CHADEMA pia imemuumbua Ngeleja baada ya kubainika kuwa mtu aliyetajwa kwa jina la Sarah Mathayo, siyo katibu wa baraza la wanawake (Bawacha) kama ilivyoripotiwa katika vyombo vya habari, bali ni mke wa Katibu wa Wilaya, Kesy Misalaba, ambaye yeye pamoja na mumewe wana tuhuma mbalimbali ndani ya chama.

  Aidha Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Wilaya ya Sengerema ni Deus Juma, ambaye habari zimedai kuwa hadi jana alikuwa akiendelea na utekelezaji wa majukumu yake ndani ya chama hicho, na hivyo kupingana na madai ya wana CCM yaliyomtaja Stanslaus Pastory kuwa ndiye mwenyekiti wa BAVICHA wilaya aliyekihama chama hicho pinzani.

  "Baadhi ya watu hao waliokimbia majukumu ya kutumikia umma….walishafukuzwa siku nyingi kwa sababu walikiuka taratibu za chama kwenda mahakamani kupinga uteuzi wa Diwani wa Viti Maalum Sarah P. Nyanda.

  "Kiuhalisia, waliowahi kuwa wanachama wa CHADEMA Sengerema waliovutana na Ngeleja kwenda safari moja ya kifo cha CCM, ni Ayub Malima na mke wake, Lucy Mussa na Kesi Misalaba na mke wake, Sarah Mathayo. Wengine waliotajwa katika vyombo vya habari kuwa ni wanachama wa CHADEMA wala hata hatujui uanachama wao ukoje, maana hawakuwahi kuwa wanachama wa chama hiki makini," ilisema sehemu nyingine ya taarifa ya chama hicho.

  Kutokana na hali hiyo, CHADEMA inapanga kufanya mikutano ya hadhara wilaya nzima ili kuwafikishia ukweli wanachama na Watanzania wote.


  Mapema wiki iliyopita, katika ziara ya Waziri Ngeleja jimbo la Sengerema, alidaiwa kufanikiwa kuvunja ngome ya CHADEMA baada ya waliodaiwa kuwa viongozi waandamizi wa chama hicho pinzani kuhamia CCM.

  Juhudi za kumpa Waziri Ngeleja kuzungumzia juu ya tuhuma hizo, hazikuzaa matunda baada ya simu yake ya mkononi kuita mara nyingi bila kupokelewa. Hata alipotafutwa tena kwa mara ya mwisho majira ya saa 1.48 jioni ya jana, simu yake ilikuwa ikikatwa kila ilipoita kwa muda.

  Aidha hata alipotumiwa ujumbe wa maneno akiombwa kutoa ufafanuzi juu ya tuhuma hizo bado hakuweza kujibu chochote hadi tunakwenda mitamboni.

  Chanzo: T. Daima
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hivi kwa nini hadi sasa viongozi wa CCM hawajaifahamu vizuri CDM? Kwa nini wanafikiri wanaweza kuitokomeza CDM kama vile walivyofanya NCCR au CUF? Hawajui kwamba kila enzi ina Vitabu vyake?

  Unfortunately CDM is another thing completely, imejaliwa kuwa na viongozi very witty --- siyo akina Mrema. Hata hiyo mbinu ya kuwafungulia viongozi wao wengi kesi mahakamani uta-recoil kwao. Pambaff sana CCM!
   
 3. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280

  Mkuu walizoea vya kunyonga!
   
 4. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mi nimeshindwa kuwaelewa hawa mafisadi wana maana gani.
  Nahisi viongozi wao wanawaza kwa kutumia masaburi yao kama walivyo.
   
 5. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wadau, baada ya Ngeleja kutangaza kwamba amesabaratisha uongozi mzima wa CHADEMA pale Sengerema, Makamanda kutoka jimbo la Geita waliamua kwenda ili kujua ukwleli halisi wa tukio hilo.Yafuatayo ni baadhi ya mambo machache tuliyoyakuta na maazimio yake.  .Jimbo la Sengerema limekuwa likimtuhumu M/Kiti huyo wa Wilaya pamoja na Katibu wake kwa kushikiana na CCM na mkurugenzi wa uchaguzi wilayani humo kuvuruga fomu za mgombea ubunge wa jimbo hilo mwaka 2010; tuhuma ambazo, pamoja na tuhuma nyingine ndizo zilizopelekea kumfukuza uenyekiti wa wilaya pamoja na kumvua uanachama wake.Jambo hilo kama lingeliungwa mkono na jimbo la Buchosa pamoja na uongozi wa Mkoa basi hawa mamluki wangelikuwa nje ya chama siku nyingi sana. Imethibitika kuwa viongozi hao waliohamia CCM walikuwa wakipewa posho na Ngeleja ili kuhujumu CHADEMA.

  Uongozi wa jimbo la Sengerema umekanusha madai yaliyoripotiwa na vyombo vya habari kwamba uongozi mzima wa wilaya umehamia CCM na badala yake ni kwamba watu waliohamia huko ni Mwenyekiti na Katibu wake pamoja na wake zao ambao waliamua kuwapachika vyeo.

  Tulikubaliana kwa pamoja kuwa kutakuwa na Mkutano wa hadhara siku ya Jumapili tarehe 15th January 2012 ndani ya Wilaya ya Sengerema ambao utaandaliwa kwa pamoja (Geita na Sengerema) na tumeuomba uongozi wa mkoa kumuandaa mgeni rasmi kutoka Taifa au miongoni mwa wabunge waliopo katika kanda hii ili tuwaeleze wanachi ukweli wa kilichotoke kwenye uongozi wa chama hapa Sengerema.
  Taarifa tuliyoipata kutoka kwa Katibu wa Mkoa wa Mwanza Mheshimiwa Wilson Mshumbuzi ni kuwa wabunge wote waliopo Mwanza wanaondoka Ijumaa kwenda Dodoma na Dar kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya kamati za Bunge, hivyo wameomba mkutano huo wa hadhara ufanyike siku ya Alhamisi terehe 12th January 2012. Geita tumekubaliana na tarehe hiyo.

  Jambo la kupendeza ni kuwa wabunge watakaohudhuria mkutano huo (Wenje, Kiwia na Machemuli) wamekubali kuchangia gharama za mkutano huo. Awali bajeti tuliyoiweka ni shs. 500,000/- pledge kwenye mkutano huo wa ndani ilifikia shs. 156,000/- na pesa tasilimu iliyotolewa papo kwa papo ni shs. 40,000/-. Tunawaomba wadau tuendelee kuchangia mkutano huu muhimu lakini usiokuwa na muda wa kutosha kwa maandalizi. Mbali na bajeti hiyo, Geita inahitaji michango ya shs. 150,000/- kwa ajili ya vyombo na usafiri ili kufanikisha shughuli hiyo ya Sengerema.
   
 6. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,582
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  Cha mlevi huliwa na mgema, na siku zote mali ya bahili huliwa na wadudu.
   
 7. p

  pat john JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tutasubiri huo mkutano ili tupate la kuongea. Ikidhihirika basi sijui Ngeleja atficha wapi uso wake. lakini kwa kuwa yeye ni mgamba hiyo sio issue kwa matu ambaye ni waziri.
   
 8. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,601
  Likes Received: 2,458
  Trophy Points: 280
  Nasubiri mkutano kesho kutwa kwa sasa no comment!
  Wasalaam!
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Hata mie siku ile ya kwanza sikuamini nilijua ni mamluki na ni kweli mamluki haya ngeleja ataficha wapi sura yake,nakumbuka 2005 Diamond kuna wanafunzi kama 30 hv walichukua kadi ya ccm,lakini viongozi wa ccm kwenye vyombo vya habari wakasema wanafunzi karibia 6000 wamejiunga na ccm yani machanga ya macho kwenda mbele
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Aibu zingine bwana hazina maana .
   
 11. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mmmmmmmmmmmm Ngeleja ana dili nyingi ishu ndogo hii ataimaliza Nape!!
   
 12. M

  Mendelian Inheritanc Member

  #12
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Ninapoelekea kukata tamaa hukumbuka kwamba siku zote ukweli na upendo hushinda, Dunia imekuwa na watu katili, lakini mwisho wa yote nao pia wameanguka" Vijana tusilale bado mapambano wakuu hakuna kulala mpaka kieleweke
   
 13. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nilijua tu, Ngeleja hana uwezo wa kumshawishi hata mtoto mdogo kuhamia Magamba. Hii ni kati ya milolongo ya viongozi wa ccm 'kuingizwa chaka', wakiongozwa na Mwenyekiti wao wa chama.
   
Loading...