Ngeleja, Jairo hawahitajiki wizarani

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
644
Mwazoni mwa miaka ya 1980 wakati huo nikiwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi mvuaha,wilayani morogoro vijijini, mkoani morogoro kilitokea kituko cha mwaka kama sio cha karne.

Kilikuwa kipindi cha cha sikukuu ya kiislamu.Vijana wawili walikunywa pmbe nyingi mapema asubuhi kabla ya saa 5.00 kusherekea sikukuu ile.Baada ya kuuchapa mtindi,vijana wale waliingia ndani kulala asubuhi ile huku wakiwaacha wake na wapenzi wao nje wakiendelea na maandalizi ya mapishi kwa ajili ya sikukuu.

Muda wa kati ya saa 9.00 na saa 10.00 alasiri mmoja wa vijana wale aliamka na kwa kudhani ni usiku,akawasha kibatari na kutoka nje uchi wa mnyama akienda chooni huku akikinga kibatari kwa mkono wa kushoto kuzuia upepo kisizimike!

Akidhani ni usiku wa manane,jua alilokuta nje likiwaka alidhani ni mbalamwezi ,alielekea chooni huku akina mama walio kuwa wanapika ukumbini wakikimbia na kutawanyika kulia na kushoto.Pale ukumbini alibaki mke wake akiwa mdomo wazi, akishangaa kilichomsibu mumewe hadi kuamua kutoka nje ya nyumba yake uchi,tena mchana akiwa ameshika kibatari.


Hayo ndio matatizo ya ulevi.Ulevi wa namna hii hadi kutoka nje uchi machana na kibatari ndio unao weza kulinganishwa na kitendo cha Waziri wa nishati na madini Wiliam ngeleja na katibu mkuu wake Dadid jairo kurejeshwa kazini na katibu mkuu kiongozi,Philemon Luhanjo"Kukumbatiana na kushangilia wakapigwa picha ,Ngeleja na Jairo walikuwa wametoka nje uchi mchanawa jua kali.Ngeleja alijishushia hadhi hadi akaacha shughuli za bunge mjini dodoma akatimka mbio kumpokea na kumshangilia katibu mkuu wake.

Tafakari chukua hatua,ulevi nomaaaaaaaaaaaaaa!


 
Ngeleja hawezi kuondoka madarakani kwa sasa kwani tatizo siyo yeye,Tatizo lipo na halishughulikiwi!!!
 
Wote hawa ni marafiki vipenzi wa bwana mkubwa. Bora kunyamaza tu maana hata tukisema haisaidii kitu
 
Watu hawa wawili wakitajwa tu roho yangu inachafuka! Wanaua watu na familia zao njaa halafu wao wanacheka cheka na kutengeneza michongo ya rushwa na kutoa empty rhetoric. Iko siku Mungu atatenda haki na kuwaumbua majahili hawa!
 
Mwazoni mwa miaka ya 1980 wakati huo nikiwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi
mvuaha, wilayani morogoro vijijini, mkoani morogoro kilitokea kituko cha mwaka
kama sio cha karne.

Kweli ni kituko cha mwaka hasa kukilinganisha kisa hiki na suala la Jairo na Ngereja...
Bravo!
 
............

Wafanyakazi wa nishati na madini wamezoea kuambulia makombo yanayo tolewa na wezi wanao itwa wawekezaji katika sekta ya madini,wanyama pori na gesi basi kwao wao wazuri ni wakubwa wao wanaowashirikisha ubadhirifu wa mali ya umma.
 
Watu hawa wawili wakitajwa tu roho yangu inachafuka! Wanaua watu na familia zao njaa halafu wao wanacheka cheka na kutengeneza michongo ya rushwa na kutoa empty rhetoric. Iko siku Mungu atatenda haki na kuwaumbua majahili hawa!


Hakuna sababu yoyote ya waziri ngereja kupaparika na kukimbilia kumpokea ofisa wa chini yake na kumpongeza kwa maua na vitambaa vyeupe na wapiga picha kushangilia huku wafanyakazi wao wakiimba kuwa wameshinda ,Je! ilikuwa ushindi zidi ya nani?
 
Wote hawa ni marafiki vipenzi wa bwana mkubwa. Bora kunyamaza tu maana hata tukisema haisaidii kitu

Bora kusema Jsaudi:kuliko kukaa kimya tu wafanyakzi wa madini hupata posho katika hizo semina elekezi za kuweka mikakati ya kuondoa kero ya umeme ,kukamilisha mipango ya muda mrefu na ya muda mfupi !upuuzi mtupu usio leta umeme.
 
Ni upuuzi wa mwaka pia

Ni zaidi ya upuuzi.
Kitendo cha ngeleja kujisahau hadi akaenda kumfungulia mlango jairo ndiye anaye paswa kumfungulia mlango yeye kinajieleza kwa nini hakuna umeme tanzania na hautakuwepo hadi ngeleja na jairo watakapo ondoka nishati na madini.
 
Swala si ngereja,Jairo wala Mkuu wa kaya. Tatizo lipo kwetu watanzania wote kwa nini hatufanyi kinachotakiwa kufanywa???
Twendeni tukawalazimishe wote waondoke ofisini mwao. Nguvu ya umma ilifanikiwa Kenya na bado inafanikiwa sehemu
Nyingine ya dunia. Sasa tuache kulaumu hao watu kwani wote hawajui wajibu wao mambo yanapoharibika. Maoni yangu.
 
Swala si ngereja,Jairo wala Mkuu wa kaya. Tatizo lipo kwetu watanzania wote kwa nini hatufanyi kinachotakiwa kufanywa???
Twendeni tukawalazimishe wote waondoke ofisini mwao. Nguvu ya umma ilifanikiwa Kenya na bado inafanikiwa sehemu
Nyingine ya dunia. Sasa tuache kulaumu hao watu kwani wote hawajui wajibu wao mambo yanapoharibika. Maoni yangu.
There is a time bomb ticking in this country. The peace that has been sang for decades is no where to be seen...you are likely to be robbed even as am writing this and this is a reality. Do you feel safe and peaceful? I don't
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom