sulphadoxine
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 2,257
- 645
Mwazoni mwa miaka ya 1980 wakati huo nikiwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi mvuaha,wilayani morogoro vijijini, mkoani morogoro kilitokea kituko cha mwaka kama sio cha karne.
Kilikuwa kipindi cha cha sikukuu ya kiislamu.Vijana wawili walikunywa pmbe nyingi mapema asubuhi kabla ya saa 5.00 kusherekea sikukuu ile.Baada ya kuuchapa mtindi,vijana wale waliingia ndani kulala asubuhi ile huku wakiwaacha wake na wapenzi wao nje wakiendelea na maandalizi ya mapishi kwa ajili ya sikukuu.
Muda wa kati ya saa 9.00 na saa 10.00 alasiri mmoja wa vijana wale aliamka na kwa kudhani ni usiku,akawasha kibatari na kutoka nje uchi wa mnyama akienda chooni huku akikinga kibatari kwa mkono wa kushoto kuzuia upepo kisizimike!
Akidhani ni usiku wa manane,jua alilokuta nje likiwaka alidhani ni mbalamwezi ,alielekea chooni huku akina mama walio kuwa wanapika ukumbini wakikimbia na kutawanyika kulia na kushoto.Pale ukumbini alibaki mke wake akiwa mdomo wazi, akishangaa kilichomsibu mumewe hadi kuamua kutoka nje ya nyumba yake uchi,tena mchana akiwa ameshika kibatari.
Hayo ndio matatizo ya ulevi.Ulevi wa namna hii hadi kutoka nje uchi machana na kibatari ndio unao weza kulinganishwa na kitendo cha Waziri wa nishati na madini Wiliam ngeleja na katibu mkuu wake Dadid jairo kurejeshwa kazini na katibu mkuu kiongozi,Philemon Luhanjo"Kukumbatiana na kushangilia wakapigwa picha ,Ngeleja na Jairo walikuwa wametoka nje uchi mchanawa jua kali.Ngeleja alijishushia hadhi hadi akaacha shughuli za bunge mjini dodoma akatimka mbio kumpokea na kumshangilia katibu mkuu wake.
Tafakari chukua hatua,ulevi nomaaaaaaaaaaaaaa!