Ngeleja badala ya kushughulikia matatizo ya umeme, aenda Tarime kwenye kampeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngeleja badala ya kushughulikia matatizo ya umeme, aenda Tarime kwenye kampeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Sep 28, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,596
  Likes Received: 82,153
  Trophy Points: 280
  Date::9/28/2008
  Kampeni Tarime: Vyama vya Chadema, CCM vyazidi kujimarisha
  *Zitto, Lissu, Ngeleja, Mashishanga wawasili

  Frederick Katulanda, Tarime
  Mwananchi

  WAKATI zikiwa zimesalia siku 13 za kupiga kampeni kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Tarime, vyama vya upinzani vimeita viongozi wake wa juu ili kuongeza nguvu katika kampeni zake.

  Uchaguzi huo unafanyika Oktoba 12 kuhitimisha kampeni zilizojaa matukio tofauti tangu zilipoanza Septemba 14. Kampeni hizo zitaisha Oktoba 11.

  Uchaguzi huo mdogo unafanywa ili kuziba kiti kilichoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Chacha Zakayo Wangwe, ambaye alifariki kwa ajali ya gari mkoani Dodoma.

  Katika kuhakikisha vinaongeza nguvu katika siku zilizosalia, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetuma jopo la viongozi wake wa juu, akiwemo Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, Mwanasheria wake Tindu Lissu pamoja na wabunge wake wote 10 ambao watakuwa mjini Tarime kusaidia kampeni.

  Kwa upande wa CCM, licha ya kuwa na Katibu wake Mkuu, Yusuf Makamba na Makamu Mwenyekiti, Pius Msekwa, pia wamemwita mkuu wa zamani wa mkoa wa Mwanza na baadaye Morogoro, Stephen Mashishanga pamoja na mwanasiasa maarufu aliyepata kupitia chama cha upinzani cha CUF, Salum Msabaha na Waziri wa Nishati na Madini,William Ngereja kuongeza nguvu, wakijumuika na Stephen Wassira pamoja na Philimon Sarungi.

  Wagombea wa vyama hivyo katika uchaguzi huo ni Charles Mwera Nyanguru wa Chadema na Christopher Ryoba Kangoye (CCM).

  Akizungumza na gazeti hili, Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa Chadema, Msafiri Mtemelwa alisema tayari Zitto Kabwe ameshawasili na kwamba wabunge wengine wa chama chao watawasili leo (Jumatatu) wakati Mwenyekiti wake Freeman Mbowe atawasili kesho kutwa.

  Alisema kuja kwa viongozi hao ni sehemu na wajibu wao katika kuhakikisha wanasaidia chama na kwamba, wakiwa mjini Tarime watafanya mikutano yao katika kata za Nyamongo, Sirari, Tarime mjini pamoja na kata nyinginezo kadri chama hicho kitakavyoona inafaa.

  “Wanakuja katika kampeni, hili ni jambo la kawaida, wanakuja kwa ajili ya kurahisisha kampeni zetu, ndiyo maana wakiwa hapa tutawagawanya katika maeneo mbalimbali kusaidia kumnadi mgombea wetu, watafanya mikutano katika kata zile ambazo tunahitaji kufanya vizuri zaidi, lakini kwa upande wa Lissu yeye anakuja kuhakikisha haki na usawa kama mwanasheria inatumika,” alieleza Mtemelwa.

  Aliongeza kuwa pamoja na kushiriki katika mikutano ya kampeni hiyo pia Lissu atapambana na polisi ambao wameanza zoezi la kamatakamata vijana kwa kisingizio cha vurugu, ikiwa ni pamoja na kupiga kambi katika eneo la Mgodi wa Nyamongo ambako atapambana na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngereja.

  Kwa upande wa CCM akizungumza na Mwananchi Katibu wa CCM wilayani Tarime, Luteni Iddi Stambuli, alipoulizwa kuhusiana na ujio wa viongozi wengine alisema hawezi kueleza kwa vile hilo ni suala la mikakati yao ambayo hawawezi kuitangaza magazetini.

  “Hayo ni masuala yetu ya ndani, kama tunaongeza au hatuongezi hayo sio ya magazeti, kama ni huyo Mashishanga yeye yupo hapa kama wanachama wengine, haya si masuala ya kuzungumzia katika magazeti,” alieleza alipoulizwa kwa njia ya simu.

  Hata hivyo, habari kutoka ndani ya CCM wilayani hapa zimeeleza kuwa, viongozi hao wamegawanywa katika kata ambapo Sarungi na Wassira wamegawanya katika maeneo yenye migogoro ya koo za wenyewe kwa wenyewe kutokana na kuaminika kuwa wanakubalika na wana ushawishi mkubwa, wengine wameachwa Tarime mjini huku Ngeleja akitarajiwa kupelekwa eneo la Mgodi wa Nyamongo.

  “Sisi viongozi wamegawanywa katika kata kulingana na umuhimu wa mtu na kata zenyewe na ugumu wake, lakini Makamba na Msekwa wao wamebaki kama viongozi na waratibu wa kampeni kila panapohitajika nguvu ya ziada wamekuwa wakienda kujazia,”kilieleza chanzo chetu kimoja.

  Tayari Zitto Kabwe ameshaingia mjini hapa wakati Lissu naye amethibitisha kufika kesho sambamba na wabunge wengine, lakini kwa upande wa CCM Ngeleja alipopigiwa simu kuthibitisha hilo aliomba kupigiwa baadaye kutokana na kuwa katika kikao.
   
 2. H

  Humble Servant Member

  #2
  Sep 28, 2008
  Joined: Aug 2, 2007
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kweli Viongozi wetu hawana PRIORITIES!wao maswala madogo na yasiyo na maslahi kwa taifa zima ndio wanaweka nguvu zote badala ya kuhangaika na tatizo la umeme linalo fanya miji na majiji yetu kuwa KIZA wao vimbelembele kwenda kuSAIDIA CHAMA! huyu Ngeleja si niyupo peke yake kama HEAD wa WIZARA??maana nimesoma mahali NAIBU wake MALIMA yupo KIJIJINII, sasa sijui nani anafuatilia swala hili kwa karibu huko yaliko makao makuu ya serikali na MARICHMOND(makampuni) yote ya umeme!

  Tusipo acha tabia ya kutukuza na kutanguliza maslahi ya chama kabla ya maslahi ya nchi wallah...! hatutafika mahali!
   
 3. H

  Humble Servant Member

  #3
  Sep 28, 2008
  Joined: Aug 2, 2007
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  hivi kwani hawezi kwenda mtu mwingine ndani ya CCM!mpaka aende NGELEJA? hizi kazi za kampeni wangeenda vibabu kama KINGUNGE au Chenge na Lowassa ambao kwa sasa hawana majukumu ya kiserikali na hawatafuni padiem za UWAZIRI na POSHO zingine za safari tunazo walipa kina NGELEJA na WASSIRA
   
 4. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu hawana cha kukosa shughuli hawa jamaa hupeana posho sawa sawa, awe Kingunge au Ngeleja, tafuta dataz vizuri mkuu utaupata ukweli,

  Kabla ya kwenda huko kwenye kampeni CCM hukutana kuchagua mtu wa kwenda, ndipo hapo ujue huyu Ngeleja kwa kutaka kujiweka vizuri kichama, alijitolea kwenda, maana sehemu kama Tarime, wajumbe wengi hukacha kwenda, wengi hupenda sehemu za mijini!

  Huyu Ngeleja alisimama na kuwaomba wajumbe kuwa yeye yuko radhi kwenda huko, ndio maana unaona ameenda! Ili kujikomba kichama waziri mzima maana hajiamini kabisa kwenye hiyo nafasi!
   
 5. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mkuu FMES, Kwanza Acha mambo ya speculation za uongo,Mhe Ngeleja Anajiamini sana katika nafasi aliyopo kwa sasa na hata Mhe. Rais ana Imani naye katika hili.Usitumie Ushaifu wa kwamba wewe ni mtu wa data kusema lile ambalo unafikiri litakunufaisha wewe na wengine.


  Rais alimuona Ngeleja Mwanzoni kabisa,akampa unaibu wa Wizara hiyo na baadaye akampa uwaziri kamili.Suala la Umeme litashughulikiwa na Songas na watendaji wengine wa wizara,suala ni dogo na ni la kifaa tu na siyo tatizo kama la kipindi kile cha RDC.Au unamtafuta ili ukalete mafundi wa hicho kifaa??


  Kusema ana jikomba haumtendei haki kabisa,Yeye ni WMana CCM na ana Haki ya kutetea sera za chama chake bila kuingiliwa na Mtu yeyote.Na suala la viongozi wengi wa CCM wanapenda kampeni za |Mjini ni Uongo ulio kubuhu,Wartu walienda Kiteto na CCM ikashinda.

  Basi kwa taarifa yako tu.,CCM itaibuka na ushindi wa kishindo kati9ka jimbo la TARIME na usitegeemee CHADEMA hii ya Mbowe na Ukabila wao watapewa dhamana hapo TARIME.The same happening in Kiteto will happen in TARIME.

  Screw CHADEMA and FMES na Ngelejha Ana jihamini kwa kuwa yeye ni Bora
   
 6. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu hiyo outburst yako unaipeleka kwa the wrong person, Ngeleja aliyetumia hela kibao alizopewa na mtandao kuwahonga wabunge ili wapitishe bajeti yake na wengine kuwaziba midomo wasiulize maswali ndio unatka kunitisha naye kwua eti anajiamini? Angekwua anajiamini si angekuwa Dar kushughulikia umeme wa mgawo badala yake anakwenda kuhangaikia jimbo ambalo haliwezi kusaidia anyhting as far as umeme wa mgawo is concerned?

  Mimi ni mwanachama wa CCM hai na tena damu, lakini haina maana ninatakwia kuwa ninashangilia ujinga tu hta kama unaonekana kuwa ujinga kama huu wa wazi wa kuwatumia kina Mtikila, wewe ulisema huko south Africa sasa hizi habari za Ngeleja umezipata wapi kama sio dataz, ambazo zinaweza kwua kweli au uongo?

  Acha huo ukali wako wa kitoto, hapa ni watuwazima tunaojua kinachoendelea bro na taifa letu, kama unaipenda CCM ipende salama lakini sio lazima utulazimishe wote tuwe kama wewe na mawazo yuako finyu!

  Ahsante Mkuu.
   
 7. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Du kaka kweli wewe HUNA mapenzi na nchi yako!!! Kwani huyo mgombea wenu hawezi jinadi mpaka Mawaziri waache kazi tuliyowatuma waende kumpigia deba?
   
 8. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135


  Mkuu Fmes,

  Suala la Wabunge kuhongwa na kunyamaza(hapa tunaongelea hata wabungwe wa CHADEMA) sio tatizo la waziri ni tatizo la wabunge which the samae thing applies to wanachi kipindi cha uchaguzi,wanahongwa ili wamchague flani..Nyani Ngabu I second you once again,waafrika ndivyo tulivyo.


  Ndio nilikuwa SA na nimerudi kwa muda kusalimia ndugu jamaa na marafiki na hili suala halikuhusu.Mimi kujau ahabarai za Tanzani ni jukumu langu na nafuatilia kila siku.
  Suala la Utu uzima na ukali vimetoka wapi.Yes i love CCM beacuase haina ukabila no matter wat..Masuala yanaohusu Ufisadi ni ya watu Binafsi na ni kama walivyo viongozi wa chadema na Pesa Ya ruzuku ya CHAMA.

  Mie naeleza ukweli tu
  Ahsante Mkuu.
   
 9. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mkuu FMES,

  Kusadia Chama ni kujikomba?ina maana mawaziri wasisaidie Chama.najua huu ni mwiba wa moto kwa CHADEMA hasa baada ya kuona mbinu mpya ya CCM katika Uchaguzi huo.

  Mie nina shaka na uanachama wako wa CCM,
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Ama Kiingereza ama Kiswahili kwa kuwa kuchanganya kumekufanya tuone kwamba uwezo wako katika hii lugha una mashaka makubwa .Rejea kwenye mabandiko yako .
   
 11. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145


  Gembe unasema kuna mbinu mpya ya CCM ? Ni ipi hii mbinu ? Mbinu safi ama chafu ? Gembe umepoteza mwelekeo namna hii ? Yes CCM wanaweza kushinda kwa kishindo sana maana kuanzia Tossi hadi Ngeleja na polisi wote wako nanyi .Ukabila Chadema ? Mnaleta mchezo hyie vijana .CCM hakuna amani kwa ukabila na udini .
   
 12. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Lunyungu,

  Nachookijua CCM Itashinda!
   
 13. Mkanya

  Mkanya JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 600
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duh! viongozi wetu wanasifa zakuwa kiongozi?
  Je? wanatuzidi nini hawa viongozi ktk kuwafanya wao wawe viongozi au tunawapaisha tu?

  Hivi hapo bongo hakuna wana-philosofia,ambao pia ni wana Arthematics?
  Nasema hivi kama haujasomea hivi vitu na wewe ni kiongozi basi wewe nikipofu unatuongoza vipofu wenzio,Maana haujui chochote. Naamini msomi yeyote aliye soma kwa haki bila kununua vyeti hawezi kuwa muoga,tunawapa vipofu wenzetu ndiomaana waoga hawana jipya.

  Jamani tuwe tunaangalia na taaluma za watu tunao wapa kura wajameni.
   
 14. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Gembe umetoa tamko kubwa sana ikitokea kwamba wana tarime wameamua kufa na kuupata ushindi kwa chama chao ambacho si CCM utafanyaje ?
   
 15. M

  Masatu JF-Expert Member

  #15
  Sep 29, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Inferiority complex hiyo unajistukia mwenyewe... tuliza mzuka ni vijimambo tu.....
   
 16. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Masatu bwana unampaka mafuta mwenzio siyo ?
   
 17. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2008
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,655
  Likes Received: 21,868
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa Gembe CCM ikitaka kujitangaza kushinda itashinda tuu hata kama kura hazikutosha. Hilo tunalifahamu siku nyingi. Ila kabla ya kufanya hivyo waangalie mazingira ya eneo lile kuwa ni tofauti sana na kule kwingine walikozoea kufanya hivyo.
   
 18. M

  Masatu JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  CCm itashinda Tarime sio kwa kuiba kura bali siasa chafu za Chadema zitawapa ushindi wa chee....
   
 19. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2008
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,721
  Likes Received: 1,212
  Trophy Points: 280
  CCM ya Makamba hii ni wezi wakubwa wa kura. Nduguyo Steven Wasira naye yupo huko akisaidia saidia.
   
 20. M

  Masatu JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Yamekuwa haya?
   
Loading...