Elections 2010 Ngeleja Apita bila kupingwa kura za maoni Sengerema

Hii ndio sisi m.
Tukisema huwa viongozi wao wengi hamnazo wanasema twatukana.
Lakini ndivyo walivyo. Alafu utegemee lolote humo? Haya ndio matunda yao wenyewe wanaita ndio wenye chama.

Hii haina tofauti na wale wazee wa CHADEMA waliosema Mbowe hawezi kupingwa.
 
Siyo swala la shule hili: kwani hao wahariri wanapoandika Lowasa kapokelewa kama mfalme na wakati wakijua ni mchafu na kuandika hivyo ni kumsafisha kwa rungu ama omo hawakusoma.
 
Sitaki kuamini kwamba Watu wa Sengerema wanaweza kuamuliwa nani wa kuwaongoza. Mchezo wanaoufanya hao CCM ni wa aibu na siasa zilopitwa na wakati katika zama hizi.
 
Sitaki kuamini kwamba Watu wa Sengerema wanaweza kuamuliwa nani wa kuwaongoza. Mchezo wanaoufanya hao CCM ni wa aibu na siasa zilopitwa na wakati katika zama hizi.

Bila shaka waziri kamwaga fungu la kutosha sana pale jimboni. Laki ajue kwamba "You can foll some people sometimes, you can nnot fool all the people all times"
Watu tushashtukia dili feki hilo!
:angry:
 
Watanzania ndugu zangu tuamke hili swala la nani kapita bila kupingwa limepitwa na wakati.Tukae na kusikiliza sera za mtu na vitu atakavyo tufanyiaa kabla ya kumpigia kura.Tutaendelea kusikia maisha bora kwenye redio hadi tuingie kaburini.Tubadilike jamani tuwape nafasi na watu wengine ili nao watuonyeshe mambo yao.tuache mambo ya KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
 
These insanes are still existing? Mbona kijana huyu anajidhalilisha hivi,does it mean that he cannot stand competition? This is another Tyrannical move,it's disguisting...
you are wrong. Politically Ngelaja can stand with anybody. He stood with the so strong guy that time (minister -Shija) and he outperformed. The fact is that though Ngeleja is a minister unlike other many ministers and MPs he always remember to visit his people in his constituency!!!!! Anakubalika sana huyu jamaa kwao. Na hata alipoingia kwenye hiyo Wizara hajawahifanya madudu yoyote. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!!!
 
you are wrong. Politically Ngelaja can stand with anybody. He stood with the so strong guy that time (minister -Shija) and he outperformed. The fact is that though Ngeleja is a minister unlike other many ministers and MPs he always remember to visit his people in his constituency!!!!! Anakubalika sana huyu jamaa kwao. Na hata alipoingia kwenye hiyo Wizara hajawahifanya madudu yoyote. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!!!
Visiting is not tija ndugu yangu what has he done (delivered) to his people ndicho kitu cha msingi.
 
Baada ya tamko la Ngeleja kupita bila kupingwa;

  • Mkoa wafuta tamko la wilaya ya Sengerema.
  • Wasema lilikiuka kanuni
Na Mwandishi Wetu

CHAMA cha mapinduzi mkoa wa Mwanza (CCM), kimetangaza rasmi kubatilisha maamuzi ya chama ngazi ya wilaya yaliyomthibitisha mbunge wa sasa wa Sengerema William Ngelaja kuwa amepita kuwa mgombea kabla hata ya kura za maoni kupigwa.

Akizungumza na Matukio kuelezea jambo hilo, katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Mwangwi Kundya Rajabu, alisema tamko la CCM wilaya ya Seengerema lililotolewa kuwa ngeleja ndiye mgombea pekee limefutwa rasmi kwa barua ambayo ameiandika na kuipeleka kwa viongozi wa chama wilayani humo.

Alisema viongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya wakiwa kama viongozi wa chama walitoa tamko hilo kimakosa na hivyo kuungana na viongozi wengine wa chama hicho ambao mpaka sasa walishatoa tamko la kupinga hatua hiyo ya Ngeleja kutangazwa kupita bila ya kupingwa.

Kundya akielezea kwa kina alisema katika barua ambayo amewaandikia (ingawa hakutaja ni ya lini wala kumbukumbu namba yake) amewaeleza wazi kuwa tamkoa lao la kutangaza kumpitisha mbunge wa sasa aliyepo madarakani William Ngeleja kupita bila ya kupingwa ni kinyume na kanuni za uongozi na maadili ya chama.

Alisema kanuni za maadili na uongozi wa chama cha mapinduzi zinakataza viongozi wa chama, au kikao chochote cha chama kuweka ama kutangaza ‘msimamo' kwa magombea yoyote yule.

"Ukisoma kifungu hiki cha 7: 5.2 cha kanuni za uongozi na maadili ya chama, kunaelezwa bayana kuwa kikao chochote cha chama hakiruhusiwa kuweka ama kutangaza ‘msimamo' kwa mgombea yoyote kwa vile kufanya hivyo kunazuia haki za wanachama wengine za katiba Ibara ya 14(3)" alieleza Kundya.

Alisema mara baada ya kusikia mambo hayo katika vyombo vya habari aliandika barua haraka kwa viongozi ngazi ya wilaya kwa ajili ya kubatilisha maamuzi yao na kuwaagiza mara baada ya kubatilisha wahakikishe wanawatangazia wanachama batilisho hilo.

Wa kwanza kupinga kupitishwa bila ya kupingwa kwa Ngeleja alikuwa ni naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara Capt. George Huruma Mkuchika ambaye alikosoa azimio hilo la wilaya na kubainisha chama ngazi ya wilaya hakina mamlaka ya kutangaza hivyo.

Sambamba na kauli hiyo ya Mkuchika naye mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Clement Mabina, amepingana uamuzi wa chama wilaya na kusema kuwa hayo ni mawazo yao binafsi huku akisisitiza kuwa hayamaanishi kuwa ndiyo msimamo wa chama.

Mabina alisema maamuzi hayo yanapingana na demokrasia ya ndani ya chama na kunyima uhuru wa wanachama wengine kugombea jambo ambalo alisema linapaswa kuzuiliwa.

Uongozi wa chama hicho wilayani Sengerema, ulitangaza uamuzi wake huo kuwa mbunge wa huyo ambaye yupo ndiye atakuwa mgombea pekee kwa nafasi ya ubunge katika jimbo lake la sengerema kutokana na wao kumpitisha bila ya kupingwa.

Uamuzi huo ambao ulichukuliwa na wafuatiliaji wa masuala ya siasa kama ni sawa na kuwapiga chenga wafuasi wao na kumpitisha mbunge huyo ilihari wakijia kuwa chama kimebadili utaratibu wa kuwapata wagombea kwa kupigiwa kura za maoni na wanachama wote.

Uamuzi huo ulitangazwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM wilayani humo, Masumbuko Bihemo Mei 4 mwaka huu alikuwa akizungumza na waandishi wa habari huku akibainisha kwamba hatua hiyo ilifikiwa kikoa cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya kilichokutana Mei Mosi mwaka huu.

Alisema kutokana na utaratibu uliowekwa na chama hicho, kikao Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ndicho kikao cha juu na chenye mamlaka katika kubaini viongozi wanaotekeleza shughuli za chama kama inavyotakiwa.

Alifafanua kuwa uamuzi wao wa kumpitisha Ngeleja umeanzia katika ngazi za matawi, kata na kuzishirikisha jumuiya za chama ikiwamo ya vijana (UVCCM) na wazee wa chama hicho na wote walitoa mapendekezo ya kutaka mbunge huyo asiwe na mpinzani.

Alisema sababu pekee iliyowavuta na kufikia uamzi huo ni juhudi za mbunge huyo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini za utekelezaji ilani ya CCM na kuwatumikia wapiga kura wake ipasavyo.



Souce:
Gazeti la Matukio
 
Huu ndio uuaji wa Demokrasia nchini Tanzania. amefanya nini cha ajabu sana kupita bila kupigwa?!!!!! Hata ufisadi huuanza hivi hivi
 
Back
Top Bottom