Ngeleja Apiga stop Maandamano Nzega ya kupinga uwepo wa Mgodi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngeleja Apiga stop Maandamano Nzega ya kupinga uwepo wa Mgodi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sigma, Mar 12, 2011.

  1. Sigma

    Sigma JF-Expert Member

    #1
    Mar 12, 2011
    Joined: Feb 26, 2011
    Messages: 5,017
    Likes Received: 12
    Trophy Points: 135
    Akizungumza na NIPASHE jana jioni kuhusu madai ya kufungwa kwa mgodi, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema suala hilo ni la kisheria na anachofanya Dk. Kigwangalla(Mbunge wa Nzega-CCM) ni kutafuta umaarufu wa kisiasa.
    Ngeleja alisema kama kuna madai ya msingi Dk. Kigwangalla angefika ofisini kwake kuyasasilisha ili apate kauli ya serikali.
    “Mbunge huyu ni miongoni mwa wabunge wanaotunga sheria za nchi na yeye anazijua, lakini nashangaa anapohamasisha wananchi kuzivunja,” alisema Ngeleja.
    Hata hivyo, Ngeleja alisema wawekezaji wa mgodi wa dhahabu wa Golden Pride wapo kisheria na hawawezi kuondolewa kwa njia ya maandamano. Alimtaka mbunge huyu kama ana madai ya msingi kuwasiliana angalau na Baraza la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) ili kujua kama mgodi huo una athari zozote za mazingira kulingana na madai yake.
     
  2. Quinine

    Quinine JF-Expert Member

    #2
    Mar 12, 2011
    Joined: Jul 26, 2010
    Messages: 8,709
    Likes Received: 6,677
    Trophy Points: 280
    Mechi ya kirafiki haina mvuto wowote.
     
  3. s

    sem2708 JF-Expert Member

    #3
    Mar 12, 2011
    Joined: Nov 4, 2010
    Messages: 3,038
    Likes Received: 421
    Trophy Points: 180
    You are right.
     
  4. Naloli

    Naloli JF-Expert Member

    #4
    Mar 12, 2011
    Joined: Aug 26, 2010
    Messages: 416
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 0
    Kaka mbona unaipa chat kihivyo, Afadhali ingekuwa mechi ya kirafiki(ccm+cuf) tungesema ya kujipima nguvu, lakini hii ni mechi ya timu ya wachezaji wa akiba na kikosi cha kwanza, Aina mvuto
     
  5. B

    Byendangwero JF-Expert Member

    #5
    Mar 12, 2011
    Joined: Oct 24, 2010
    Messages: 872
    Likes Received: 3
    Trophy Points: 0
    Kuvunja kwa makusudi sheria inayoendeleza ufujaji wa rasilimali za taifa, kunamkweza mhusika kwenye kilele cha utiifu wa utawala wa sheria.
     
  6. Mhoja

    Mhoja JF-Expert Member

    #6
    Mar 12, 2011
    Joined: Aug 13, 2010
    Messages: 206
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 35
    Kigwangala endelea na uzi huo huo. Wewe ndiye unayejua madhara ya mgodi huo na siyo Ngeleja. Mechi haichagui wachezaji.
     
  7. nsimba

    nsimba JF-Expert Member

    #7
    Mar 12, 2011
    Joined: Oct 7, 2010
    Messages: 785
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 33
    inafurahisha sana, kigwangala go...go.............go andamaneno tu mpaka kielewe kuwa ndani ya ccm wanyonyaji ni akina nani na wakweli ni akina nani!!!!!!!!!!!!!! hali hii itawachanganua wenyewe na wananchi watajua ukweli wake.
     
  8. Quinine

    Quinine JF-Expert Member

    #8
    Mar 12, 2011
    Joined: Jul 26, 2010
    Messages: 8,709
    Likes Received: 6,677
    Trophy Points: 280
    Sure, timu moja iko mazoezini walichofanya ni kugawana jezi wengine wako vifua wazi.
     
  9. n

    niweze JF-Expert Member

    #9
    Mar 12, 2011
    Joined: Oct 21, 2009
    Messages: 1,008
    Likes Received: 2
    Trophy Points: 0
    Sheria zipi wewe fisadi. Kuna sheria yeyote unafahamu ya kutetea wananchi na raslimali zake? Hakuna sheria yeyote ile kama ipo mbona hizo taratibu na sheria zingezuia kuwepo kwa hiyo kampuni Nzega? Kama kungekuwa na sheria Tanzania Kikwete asingekuwa Ikulu na Mbunge usingekuwa Mbunge hapo Nzega.

    Sababu kama hizi ndizo zinatufanya wananchi tupiganie Katiba kwa manufaa yetu sio ccm. Mtaona kama ccm mtakuwepo mweiz ujao Ikulu[
     
  10. kapotolo

    kapotolo JF-Expert Member

    #10
    Mar 12, 2011
    Joined: Sep 19, 2010
    Messages: 3,717
    Likes Received: 68
    Trophy Points: 145
    Hivi ngeleja ana uwezo kisheria kuzuia maandamano? Aache ufisadi wake hapa, washaona hata kama ni mechi ya mazoezi lakini ina athari kwani watu watahoji nani alisaini mkataba wa mgodi huu, na kwa kuwa aliesaini ni bosi wake JK (alipokuwa waziri wa madini - kumbuka list of shame) italeta picha mbaya. Kigwa endelea na mipango yako mpuuze huyu mpuuzi Ngeleja.
     
  11. U

    Uswe JF-Expert Member

    #11
    Mar 12, 2011
    Joined: Nov 1, 2010
    Messages: 2,200
    Likes Received: 7
    Trophy Points: 135
    acha kuipa mvuto hii walao si mechi ya first team vs reserve haya ni mazoezi tu ya kikosi B ( yaani wenyewe kwa wenyewe :)
     
  12. V

    Vancomycin Senior Member

    #12
    Mar 12, 2011
    Joined: Jan 7, 2011
    Messages: 171
    Likes Received: 2
    Trophy Points: 0
    Ha ha ha Kigwangala hiyo ndiyo CCM lazima wakukabe koo,uwe ndani ya hicho chama utetee wananchi subiri ni imani yangu wanakuhesabia wakuchakachue.Hicho ni chama cha maslah binafsi.
    Sina shaka na wewe kwani najua ulivyoongoza mgomo wa madaktari Muhimbili kudai maslahi yao ila wasiwasi wangu ndani ya chama hicho cha ghilba ambacho hakijali tena maslahi ya wengi jitihada yako haita fika mbali.
     
  13. V

    Vancomycin Senior Member

    #13
    Mar 12, 2011
    Joined: Jan 7, 2011
    Messages: 171
    Likes Received: 2
    Trophy Points: 0
    Ha ha ha Kigwangala hiyo ndiyo CCM lazima wakukabe koo,uwe ndani ya hicho chama utetee wananchi? subiri ni imani yangu wanakuhesabia wakuchakachue.Hicho ni chama cha maslah binafsi.
    Sina shaka na wewe kwenye kudai haki kwani najua ulivyoongoza mgomo wa madaktari Muhimbili kudai maslahi yao ila wasiwasi wangu ndani ya chama hicho cha ghilba ambacho hakijali tena maslahi ya wengi jitihada zako hazita fika mbali.
     
  14. m

    miradibubu JF-Expert Member

    #14
    Mar 12, 2011
    Joined: Sep 21, 2010
    Messages: 310
    Likes Received: 2
    Trophy Points: 35
    Kigwangala kweliumedhamiria? hvi unafahamu kuwa serikali ya kijiji kinachozunguka mgodi walisainiana mkataba na mgodi kuhusu kupewa hudumaa za kijamii? je nani anafuatilia utekelezaji huu, mimi ninatarifa za kina kuwa jambo hili siku hizi halitekelezeki, unajiamini na upo pamoja katika mapambano dhidi ya mafisadi hata kwa gharama yoyote, jitokeze unijibu kwani kwa sasa ninatafakari kulifikisha suala hili kwa CHADEMA
     
  15. Raia Fulani

    Raia Fulani JF-Expert Member

    #15
    Mar 12, 2011
    Joined: Mar 12, 2009
    Messages: 10,228
    Likes Received: 75
    Trophy Points: 145
    huku kigwangala, huku makamba... Ngeleja kazi anayo
     
  16. Washawasha

    Washawasha JF-Expert Member

    #16
    Mar 12, 2011
    Joined: Aug 7, 2006
    Messages: 8,623
    Likes Received: 375
    Trophy Points: 180
    mechi ni mechi tu hata ya mchangani ni mechi
     
  17. M

    Munghiki Senior Member

    #17
    Mar 12, 2011
    Joined: Oct 10, 2010
    Messages: 153
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 35
    umenene!te te teh
     
  18. j

    junior2008 JF-Expert Member

    #18
    Mar 12, 2011
    Joined: Apr 27, 2009
    Messages: 528
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    CCM ina wenyewe nao ni mafisadi, wengine wote ni washika pembe tu! Kama kweli Dr Kigwangala amedhamiria kutetea haki za wananchi wake ajue tu kwamba hiyo ni vita kati yake na mafisadi, lakini akisimama imara atashinda kwasababu wananchi (nguvu ya umma) watamuunga mkono.
     
  19. Dr wa ukweli

    Dr wa ukweli JF-Expert Member

    #19
    Mar 12, 2011
    Joined: Feb 28, 2011
    Messages: 891
    Likes Received: 27
    Trophy Points: 45
    Hii metch ni ya kichangani lakini mwamuz atakuwa wa fifa
     
  20. Bu'yaka

    Bu'yaka JF-Expert Member

    #20
    Mar 12, 2011
    Joined: Jul 29, 2010
    Messages: 702
    Likes Received: 273
    Trophy Points: 80
    Kigwangala kampiga buti Ngeleja mazoezini, anataka sifa achukue namba, kumbe kocha mwenyewe anataka timu lake lishindwe, namba ya Ngeleja hachukui, na asipoangalia hata benchi watamtoa kama Selelii.
     
Loading...