Ngeleja ang'ara; Masaburi, Ngwilizi, Makongoro Mahanga WAGONGA CHINI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngeleja ang'ara; Masaburi, Ngwilizi, Makongoro Mahanga WAGONGA CHINI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 2, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]Ngeleja wang'ara

  • DK. MAHANGA, MASABURI, NGWILIZI WAKWAMA

  na Waandishi wetu

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amedhihirisha umwamba wake katika siasa za ndani ya Chama chake cha Mapinduzi (CCM), baada ya kuibuka na ushindi wa kishindo katika nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa kupitia Wilaya ya Monduli.

  Wakati Lowassa aking'ara Monduli na kumpiku kigogo mwenzake, Frederick Sumaye, aliyegaragazwa juzi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji na Uwezeshaji), Mary Nagu, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja naye amechomoza wilayani Sengerema.

  Hata hivyo hali si shwari kwa Naibu Waziri, Dk. Makongoro Mahanga, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi na Hassan Ngwilizi, kwani licha ya ukongwe wao ndani ya CCM safari hii kura hazijatosha.

  Uchaguzi huo umetawaliwa na vituko vya kila aina ambapo wilayani Kahama wajumbe walijikuta wakishinda na kulala njaa huku wengine wakishikiliwa kwa muda na kuhojiwa kwa tuhuma za rushwa.

  Taarifa kutoka Monduli zilisema kuwa Lowassa alijizolea kura 709 katika uchaguzi huo uliofanyika jana na kuwaacha washindani wake, Dk. Suleshi Toure aliyepata kuwa saba na Nanai Taon Konina aliyeambulia kura nne.

  Pamoja na Dk. Toure kutangaza kujitoa kwenye kinyang'anyiro hicho na kumpigia debe Konina, bado umoja wao haukuweza kufua dafu kwa Lowassa.
  Akijinadi mbele ya wapiga kura waliokuwa wakimshangilia muda wote, Lowassa alijivunia mafanikio makubwa ambayo Wilaya ya Monduli imeyapata katika sekta ya elimu, afya na barabara.

  Pia alisema uhai wa chama umekuwa mkubwa tofauti na wilaya nyingine za Mkoa wa Arusha ambazo zimekuwa ngome ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  "Mtu akiniuliza kwanini nagombea tena nafasi hii ya ujumbe wa NEC, nitamjibu kwa jeuri kwamba nimefanikiwa kuifanya Monduli kuwa moja ya wilaya bora nchini,"' alisema na kushangiliwa.

  Wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza, Ngeleja ameibuka shujaa katika nafasi ya NEC huku aliyekuwa mbunge wa Misungwi, Dalali Shibiliti naye akifanya hivyo wilayani Misungwi.

  Ngeleja alijizolea ushindi wilayani Sengerema kwa kupata kura 1,060 na kuwabwaga Joah Kasika (317), Philemon Lugumiliza (132) na Renatus Nchali (11).

  Katika uchaguzi huo, aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wilayani humo, Jaji Tasinga, aliangushwa na Chasama Makata aliyepata kuwa 888, huku yeye akiambulia kura 661 na Palelia Ngotezi alipata kura sita tu.

  Wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa waliochaguliwa ni Joseph Yared, Julius Butogwa, George Kazungu, Ahmed Jaha na Zena Mbisu, huku nafasi ya Katibu wa Uchumi ikitwaliwa na Onesmo Mashili, Katibu wa Uenezi na Itikadi ilikwenda kwa Masumbuko Bihemo.

  Wilayani Misungwi, Shibiliti alishinda ujumbe wa NEC kwa kura 667 na kuwabwaga Alexender Mnyeti (457) na Mwamba Makune (14).

  Nafasi ya mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, ilichukuliwa na Judith Mlolwa aliyepata kura 574 huku aliyekuwa mwenyekiti, Daud Samwel Gambadu akipata kura 420.

  Wajumbe watano wa mkutano mkuu wa taifa, waliochaguliwa ni Amina Ali Juma (425), Daud Katambi (532), Medadi Mwijage (437), Musa Mnyeti (655) na Mwamba Makune (777).

  Mahanga, Masaburi nje

  Jijini Dar es Salaam katika Wilaya ya Ilala, vigogo wawili, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga na Meya wa Jiji hilo, Dk. Didas Masaburi, nao wameonja joto ya jiwe baada ya kutupwa nje ya ulingo na wapinzani wao.
  Dk. Mahanga ambaye alikuwa akiwania nafasi ya ujumbe wa NEC Taifa,

  alidondoshwa na mpinzani wake, Ramish Patel, aliyeibuka na kura 664 dhidi ya kura 411 za naibu waziri huyo, huku wakifuatiwa na Simba Ulanga (135) na Seleman Ditopile.

  Katika nafasi ya wajumbe watano wa mkutano mkuu taifa, Meya Masaburi alishika nafasi ya saba akiwa na kura 418 hivyo kupigwa kikumbo na Athuman Chilu (689), Aisha Sululu (635), Bona Kiruwa (516), Yona Mwansuku (461) na Ramish Patel (442).

  Nako mkoani Tanga, waziri wa zamani na mbunge wa Mlalo, Brigedia Jenerali mstaafu, Hassan Ngwilizi, naye amekula mweleka katika nafasi ya ujumbe wa NEC Taifa.

  Kahama walala njaa

  Wajumbe 451 wa mkutano mkuu wa uchaguzi Wilaya ya Kahama wamelazimika kushinda na kulala njaa kwa kunywa kikombe kimoja cha chai na bagia mbili.
  Hata hivyo uchaguzi huo uliponea chupchupu kutofanyika baada ya wajumbe kusimamia hoja ya kupatiwa chakula kwanza lakini mwenyekiti wa uchaguzi huo,

  James Lembeli, aliingilia kati na kuwaahidi wajumbe kuwa watapewa sh 5,000 ya kujikimu.

  Katika hatua nyingine, diwani wa zamani wa Kata ya Kahama Mjini, Furaha Kagoro, alikamatwa na kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

  Kaimu Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Kahama, Lucas Sanya, alilithibitisha kukamatwa kwa kiongozi huyo baada ya kudaiwa kujihusisha na masuala ya rushwa katika nyumba ya kulala wageni ya Rock Point jirani na ukumbi ulikofanyika mkutano wa CCM.

  Uchaguzi huo ulimchagua Mabala Mlolwa kuwa mwenyekiti wa CCM wa wilaya kwa kura 992, akifuatiwa na Patricia Shimba (789), Edward Msoma (250) na Shida Soko (232).

  Mdogo wa Waziri Mary Nagu, Catherine Dalali, aliibuka kidedea katika nafasi ya mjumbe wa NEC kwa kumshinda mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Kahama aliyemaliza muda wake, Andrew Masanje.

  Wajumbe wapata ajali

  Kada wa CCM amefariki papo hapo na wengine zaidi ya 85 kujeruhiwa vibaya baada ya lori aina ya Fuso lenye namba za usajili T420 APM walilokuwa wakisafiria kwenda kwenye uchaguzi wilayani Chunya kupinduka.

  Ajali hiyo ilitokea juzi saa 2:30 asubuhi katika eneo la Matundasi umbali wa kilometa 21 nje ya mji wa Chunya wakati wajumbe hao zaidi ya 100 wakitokea katika kata za Lupa, Upendo na Mamba kwenda kwenye mkutano wa uchaguzi.

  Akithibitisha kupokea majeruhi wa ajali hiyo, Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Chunya, Dk. Henry Mwansasu, alisema kuwa alipokea mwili wa mtu mmoja pamoja na majeruhi 85.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  huyu ngeleja wamemchagua kwa lipi? anywy kwakuwa ni magamba u can expect anything from them.huyo makongoro haman kitu ,nakumbuka kipindi nikiishi home tabata b4 cjamaliza chuo, alikuwa anakuja kuongea na kinamama then wanapewa buku mbili mbili eti eli wamchague (2010 gen.election), so sad yani nilimdharau toka enzi hizo ,pesa walikuwa wanagawa wapambe.
   
 3. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kama hata Ngeleja anarudi ninawasiwasi na uelewa wa Watanzania(the electorate)
   
 4. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  yaani uelewa wa watanzania unanitia wasiwasi maana kama ccm bado inaleta uozo huu kwenye system yake sijui inasaidia nini kwa wananchi
   
 5. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Yani unaweza ukapata hisia tosha kuwa nini cha kutarajiwa 2015.
   
 6. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  ni dhahiri Makongoro hata ubunge ailishindwa
   
 7. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Tatizo sio uelewa wa watz! Ni kwamba sisiem hakuna mtu wa kumchagua huko. Ukiwekewa wajinga kumi, huwezi kukosa mwenye afadhali kati yao! Waliochaguliwa ndio afadhali.
   
 8. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Janamizi la kushindwa ubunge linaendelea kuwaandama waliochakachua kura! Ona yaliyompata Kigwangwalah!
   
Loading...