Ngeleja amelewa madaraka?

Nyumbu-

JF-Expert Member
May 26, 2009
987
349
Jamani, kama kuwa waziri kwa miaka minne tu, inamfanya mtu awe hivi , mi nachelea tutarudi kwenye usultani sasa hivi! Hebu angalia habari hii......

Waziri Ngeleja nusura azichape kwa adha ya ATM Dar
*NI BAADA YA KUTAKIWA AWAPISHE WATEJA
Sadick Mtulya
WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja, juzi alizua tafrani kwenye mashine ya kuchukulia fedha (ATM) ya benki ya Standard Chartered, jijini Dar es Salaam baada ya kutaka kumchapa makonde mlinzi wa mashine hiyo, Pascal Mnaku.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na mlinzi huyo wa kampuni ya Ultimate Security, zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 3:00 asubuhi kwenye jengo la Habour View, maarufu kama JMall.
Mnaku aliliambia gazeti hili kuwa alinusurika kupigwa na waziri huyo kijana aliyekuwa akizungumza na simu ndani ya kibanda hicho, baada ya kumtaka atoke kuwapisha wateja wengine kupata huduma hiyo.
Mnaku alisema waziri huyo alikuwa anatumia muda mwingi kuzungumza na simu ndani ya mashine hiyo badala ya kuchukua fedha wakati msururu mrefu wa watu ukiwa unamsubiri atoke.
"Kwanza mimi sikujua kwamba mtu niliyemwambia awapishe wateja wengine ni waziri. Ni kweli nilimfuata na kumwambia awapishe kwa sababu alikuwa anatumia muda mwingi kuzungumza na simu, wala sikuwa na nia nyingine yoyote mbaya dhidi yake," alisema Mnaku na kuongeza:
"Lakini, waziri huyo ghafla aligeuka na kuanza kunifokea akiniambia wewe unanijua mimi nani?... hunijui mimi! na kunitusi, (matusi yasiyoweza kuandikika)."
Mnaku aliendelea kueleza kuwa; "Kutokana na hali hiyo nilipomjibu kwamba, mimi sikuwa na nia mbaya na nilifanya vile ili wateja wengine wapate huduma".
Aliongeza: "Baada ya kumwambia hivyo akazidisha ukali, lakini watu walipoanza kukusanyika, huku wengine wakimwomba radhi kwa kumtaja jina, alianza kupunguza hasira na kuondoka".
Kwa mujibu wa mlinzi huyo, baada ya tafrani hiyo iliyodumu kwa takribani dakika nane, Waziri Ngeleja aliondoka na baadaye kunako majira ya saa 7:00 mchana uongozi wa kampuni yake ya ulinzi ulimwondoa katika kituo hicho cha kazi na kurudishwa makao makuu.
Alisema saa 9:30 jioni, alichukuliwa na uongozi wa kampuni hiyo na kupelekwa ofisini kwa Ngeleja kwa ajili ya mazungumzo zaidi.
"Baada ya kutokea kwa tukio saa 9:30 jioni wakuu wangu walinipeleka ofisini kwa Ngeleja na kisha akazungumza mengi ambayo siwezi kukuambia na baada ya hapo wakuu wangu wakamuomba msamaha kwa niaba ya kampuni," alisema Mnaku.
"Na kwa sasa maelekezo niliyopata kutoka kwa waajiri wangu ni kwamba, wanalifanyia upelelezi suala hili hivyo hatima ya kibarua changu kinategemeana na majibu ya upelelezi huo," alisema Mnaku
Mashuhuda wa tukio hilo walilieleza gazeti hili kuwa hali hiyo ilijitokeza baada ya Mnaku kuwahamishia wateja kutoka katika mashine ya ATM ya Barclays iliyoko katika jengo hilo ambayo wakati huo ilikuwa imeishiwa fedha.
"Baada ya Mnaku kuona mashine ya ATM ya Barclays kuwa haina fedha, ndipo akalazimika kuwaambia wateja wakatumie ATM ya Standard Chartered ambayo wakati huo Waziri Ngeleja alikuwa anaitumia na huku akizungumza na simu,” alisema shuhuda mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe.
Shuhuda huyo alisema baada ya Mnaku kumtaka waziri kuwapisha wengine, ghafla na huku akiwa na hasira, Waziri Ngeleja alisema: "Ina maana hunijui mimi, hujui nafasi yangu, halafu...tusi," alisema shuhuda huyo.
Shuhuda huyo aliongeza: "Kutokana na maneno hayo, Mnaku akamjibu kwa kujitetea kwamba, mimi nimekuomba uwapishe wateja wengine, sikuwa na lingine".
Habari zaidi zinadai kwamba, katika kikao na waajiri wa Mnaku, Ngeleja alisema: "Siwezi kumsamehe (Mnaku) mpaka atakapopewe adhabu kali."
 
wanasiasa na watu wa sheri mpo?

mbona kimya Mwnakijiji tuelezeni mabo kiundani zaidi inamaana lazima watu wooote wamjue na kwa nini asijibu kwa utaratibu au anatumia uongizi wake kutishia matu kwa kali hii

Habari zaidi zinadai kwamba, katika kikao na waajiri wa Mnaku, Ngeleja alisema: "Siwezi kumsamehe (Mnaku) mpaka atakapopewe adhabu kali."
 
Back
Top Bottom