Ngeleja amehonga wagombea wa upinzani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngeleja amehonga wagombea wa upinzani?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mdau, Aug 26, 2010.

 1. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Nimesikitishwa sana na wimbi la ubakaji wa demokrasia linaloendelea kuelekea uchaguzi mkuu 2010..kubwa katika yote,ni hili suala la 'kupita bila kupingwa" kwa baadhi ya wagombea katika majimbo mbalimbali..nimeguswa zaidi na jimbo la Sengerema, ambalo mbunge anayemaliza muda wake ni Waziri wa Madini;William Ngeleja,mtu muhimu sana katika mchakato mzima wa uwekezaji kati ya Tanzania na makampuni ya kigeni,katika sekta ya madini..katika jimbo hili, wagombea wawili wa upinzani, kutoka CHADEMA na CUF wametolewa katika mchakato eti 'kwa kushindwa kukamilisha taratibu za ujazaji fomu'...kama mfuatiliaji wa siasa za Tanzania, nina maswali yafuatayo kwa yeyote mwenye majibu ama mchago wa nyongeza:

  1. Je, ni kweli makampuni makubwa ya nje huingilia siasa za nchi changa ili kuhakikisha viongozi wanaoyasaidia hayo makampuni waendelee kushikilia nafasi zao za kisiasa??

  2. Je, ni kweli kwamba katika mchakato wa kura za maoni za CCM mojawapo ya mgombea ktk jimbo la Sengerema alipoteza kandarasi yake ktk mojawapo ya migodi ya dhahabu kwa vile tu alimpinga Ngeleja??

  3. Je, ni kweli mgombea wa CHADEMA, ambaye ni katibu wa vijana wa mkoa wa Mwanza, mhitimu wa Sheria toka UDSM mwaka 2009 na mwenyeji wa Sengerema alishindwa kutimiza wadhamini 25 na pia kusahau kujaza fomu moja??

  4. Je, ni kweli mgombea wa CUF alishindwa kabisa kujaza fomu zake??


  Majibu ya maswali haya (kama yapo), na michango ya ziada itasaidia kupata ukweli wa mambo katika utaratibu huu wa "kupita bila kupingwa"..PCCB tayari wanazo taarifa za kutoa rushwa za Nimrod Mkono..nadhani ni vema wakitanua wavu wao ili waweze kutoa utata katika matukio mengine kama haya..
   
 2. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Tanzania has significant uranium deposits - govt.

  And the country hopes to start mining it by 2011
  Posted: Monday , 27 Jul 2009  st1\:*{behavior:url(#ieooui) }Tanzania has at least 53.9 million pounds of uranium oxide deposits and expects to start mining some of that by 2011, the east Africa nation's energy and mineral minister said.
  Gold dominates Tanzania's mining sector -- which is Africa's third largest producer of the precious metal -- but there is increasing interest in other metals like uranium and nickel.
  Minister William Ngeleja said two companies -- Mantra Tanzania Limited, a unit of Australia's Mantra Resources (MRU.AX: Quote), and Uranex Tanzania Limited, a subsidiary of Australia's Uranex (UNX.AX: Quote) -- hoped to start producing in two years.
  "Mantra Tanzania Limited is expected to start mining uranium by 2012, Uranex Tanzania Limited ... expects to start producing the mineral in 2011," Ngeleja said in a speech to parliament published in local media on Sunday.
  Mantra is working on a project in south Tanzania, which it says has an inferred mineral resource of 35.9 million pounds of uranium oxide, and Uranex's project in the centre has an estimated 6.7 million pounds of the oxide.
  Ngeleja said that the two were among 20 companies licensed to explore for uranium in east Africa's second largest economy. Tanzania also has diamonds, Tanzanite and coal.
  The nation is working on a new mining law -- after 10 years of review -- aiming to increase the sector's economic contribution, change ownership rules, and increase royalties paid on minerals like gold and diamonds.
  "We hope to bring this law to parliament in October," Ngeleja said.
  Mineral exports earned $1.08 billion in 2008 from $983 million in the previous year, he said. (Reporting by George Obulutsa; Editing by Jack Kimball)

  Mineweb.com - The world's premier mining and mining investment website Tanzania has significant uranium deposits - govt. - URANIUM | Mineweb


  My take: Anatamani awepo tena kwenye baraza lijalo, Uranium is a hot stuff...
   
 3. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ni kweli hao uliowataja wameshindwa kuzaja fomu zao za kuteuliwa kugombea,hilo halina ubishi kwasababu wao ni binaadam kama wewe ambae kuna wakati unasahau na kupitiwa!
   
 4. m

  mzeewapori Member

  #4
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inawezekana hii ni nguvu ya RA. Kwani alikuwanaye Voda, akamtoa na kumpa uwezo wa kugombea ubunge/Uwaziri wa Nishati (Caspian ndiye mbia mkuu wa kampuni za madini) ili aje alinda maslahi yake. Hivyo inawezekana ni mwendelezo tu wa mambo hayo. Something is wrong somewhere kwa hawa wapinzani walioenguliwa.
   
 5. D

  Dick JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yawezekana mzuiaji awe mtoaji?:confused2:
   
 6. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  upo sawa mkuu...lakini kumbuka uongozi ni wajibu na dhamana, so kama tukiacha viongozi wetu waliopo na watarajiwa watumie suala la KUSAHAU kama escape route, ina maana hakutakua na uwajibikaji wowote...ukiamua kuwa kiongozi lazima ukubali kujitoa kafara kwa maendeleo ya wengine....
   
 7. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,935
  Likes Received: 12,204
  Trophy Points: 280
  Utaratibu wa Tanzania ni hopeless huwezi kumzuia mtu mwenye uwezo wa kuongoza kisa eti kasahau kuandika jina la pili au kuweka sahihi this is nonsense, haiingii akilini mfano Msajili kuwawekea pingamizi waliopitishwa na wananchi wa majimbo yao kisa hawakujaza fomu za gharama ya uchaguzi kitu ambcho ni irrelevant kabisa na maendeleo ya jimbo.

  Ndio maana UK sasa inafumuafumua muundo mzima wa uchaguzi ili kupunguza paper work ibaki na field works nyingi. Sisi Tanzania tuna- concentrate kwenye paper work election wakati wenzetu wanaachia madaraka hayo wananchi.

  Kwa Tanzania Msajili wa vyama amekuwa kama adui wa vyama badala ya kuwa rafiki na mlezi wa vyama, lengo lake limebaki kuangali chama gani akifute si chama gani akisaidie. Au kwa wakati huu badala ya msajili kuangalia wagombea gani wanahitaji msaada yeye anasubiri kuona ni wagombea gani hawaja jaza fomu vizuri awawekee pingamizi.

  Ningekuwa mimi natawala ningefutilia mbali kitengo cha Msajili na kuiacha NEC maana kuna muingiliano wa maslahi hapo na infact hana kazi. Kama anajitoa ulezi wa vyama kazi yake itakuwa nini basi endapo hakutakuwa na chama kipya kingine. Kitengo hiki ni matumizi mabaya ya pesa za serikali ningeshauri kivunjwe au kiunganishwe na NEC.
   
 8. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180

  Nakuunga mkono zaidi humo kwenye nyekundu mkuu....
   
Loading...