Ngeleja ameanza Uchunguz umeme 132kv kwa Kakobe

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
864
Wiki iliyopita Mafundi wa Tanesco walianza kufanyia utafiti nguzo namba 19 na Namba 20 kubaini ni kwa nini Umeme haupiti Maeneo hayo.Hata hivya gari ya Winchi imeharibika mda mfupi baada ya kumupandisha Technecian kwenye nguzo namba 19 ambapo ilisababisha kushaka haraka na kuonda ktk maeneo hayo!Mpaka sasa gari hilo la Winch limetelekezwa kwenye nguzo namba 19
 
Tunaweza kuyaita ni maajabu ya Kakobe au ni maajabu ya Mungu wa Kakobe?
 
Kwani si alisemaga nadhani mungu wake alikuwa busy ndo maana utekelezaji ulichelewa kidoggo
 
Jamani, hivi ni kweli huu umemehaujapita pale? Niliwahi kusikia habari hizi z=kitambo kidogo nikadhani ni porojo tu
 
matengenezo ya kawaida
Ni kweli kabisa

Jamani, hivi ni kweli huu umemehaujapita pale? Niliwahi kusikia habari hizi z=kitambo kidogo nikadhani ni porojo tu

Ni porojo tu. Umeme unaendelea kupita pale kutoka Ubungo kuelekea Makumbusho palipo na 132 KV substation. Siku hizi umeme umetengemaa meneo yanayokuwa fed na ile substation, tofauti na awali ambapo eneo hilo lilikuwa na low voltage.
 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (F.G.B.F), Zakaria Kakobe amemtaka Rais Kikwete kutoa msimamo kuhusiana na mgogoro wa kanisa la F.G.P.F. na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Amechukua hatua hiyo kwa alichosema kuwa makubaliano ya mwisho kati yake na Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja yamekiukwa.

Akizungumza jana Dar es Salaam na waandishi wa habari, Askofu Kakobe alisema awali Bw. Ngeleja alikuwa na ushirikiano mzuri lakini alishindwa kuendelea naye kutokana na 'utawala kambale' uliopo katika wizara yake. "Serikali yetu imekuwa na makundi na mpasuko wa kutisha, ndio maana Ngeleja ameshindwa kabisa kuelewana na mimi kutokana na watu wanaojiita kambale," alisema Askofu Kakobe

Alisema katika kikao cha mwisho na Bw. Ngeleja iliamuriwa kutafutwa mshauri na mtaalamu anayejitegemea kuhusu upitishaji wa laini ya umeme mbele ya kanisa la FGBF. Alisema kutokana na ufisadi uliopo TANESCO, waliichagua Kampuni ya BICO ambayo walishirikiana na kutengeneza 'ripoti ya kifisadi' ili kuwakandamiza wananchi. Aidha maridhiano hayo yalidaiwa kuwa baada ya wataalamu hao kumaliza vipimo, ripoti hiyo ilitakiwa kurudishwa kwa waziri na wadau wengine kwa majadiliano.

"Nimeandikiwa barua kuitwa kwenye kikao kesho (leo) wakati ripoti hiyo haijafikishwa kwa waziri, ili kujadiliwa na wadau wengine, alisema na kuongeza kuwa". "Sitashiriki kikao hicho kwa kuwa ni kikao cha wahuni na kimeandaliwa na wahuni, mimi ni mwadilifu, siwezi kufanya upumbavu na nipo tayari kubeba msalaba huo," alifoka askofu huyo.

Aliongeza kuwa ripoti hiyo ilitengezwa na haikufanyiwa kazi, kwa kuwa TANESCO walishaamua kupitisha umeme katika eneo la kanisa. Askofu Kakobe ameitaka TANESCO kumaliza suala hilo kwa amani, ili kuepusha migogoro ya kidini kwa nkuwa FGBF haikushikishwa katika mradi huo tangu mwaka 2007.


source: http://www.wavuti.com/4/post/2010/02/ujumbe-wa-askofu-kakobe-kwa-serikali-na-kampuni-ya-tanesco.html#ixzz1gzBxQGHB
 
KAULI YA ASKOFU KAKOBE KWA SERIKALI YA KIKWETE
Gazeti habari Leo
Tarehe: 8th March 2010
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe amewaamuru waumini wake kuvua fulana walizozivaa kupinga Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuweka nguzo zenye msongo wa kilovolti 132 karibu na kanisa lake na ametangaza kuondoa ulinzi uliokuwa unafanywa na waumini hao.

Miezi miwili sasa (siku 77), waumini wa kanisa hilo wamekuwa wanapeana zamu kulinda eneo hilo la kanisa ili Tanesco wasiweke nguzo hizo za umeme na walifanya ulinzi huo huku wamevaa fulana zilizoandikwa maneno ya kuilaani Tanesco kuwa baada ya Richmond kuifisadi sasa wamegeukia kanisa hilo.

Akizungumza jana, Askofu Kakobe alisema kambi hiyo haina maana kuwepo kwani tayari serikali imetoa tamko la mwisho la kukataa maombi yake ya kutaka angalau nguzo hizo za umeme zipinde ili zisipite karibu na kanisa hilo.

"Kwa kweli huko mbele naona giza, ila naamini kuwa uamuzi huu wa serikali mwisho wa siku, Mungu atawafundisha kwamba amani iliyopo ilitokana na serikali kuheshimu dini za watu," alisema Askofu Kakobe.

Alisema Tanesco isijisumbue kwenda na majeshi yoyote kwani hakuna hata muumini mmoja wa kanisa hilo ambaye atawasogelea wala kuwadhuru. Alisema kanisa hilo lilijaribu kufikisha malalamiko yake hadi kwa Rais Jakaya Kikwete, lakini uamuzi wa serikali ni ule uliotangazwa na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.

Ngeleja alitangaza uamuzi wa serikali juzi na kusema kuwa maombi ya Askofu Kakobe ya kutaka kupindisha nguzo za umeme yamekataliwa kwa kuzingatia kuwa miundombinu ya eneo hilo imehusisha ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo kasi.

"Mwanzoni tulikuwa tunapambana na Tanesco ambao sio serikali, lakini sasa tayari Serikali tuliyoitegemea kutusaidia imeshatoa tamko lake, sasa kambi yetu ya ulinzi ina maana gani tena? Imebaki kupiga kelele tu…" alisema askofu huyo na kuongeza kuwa uamuzi huo umelifanya kanisa hilo lisimamishe mchakato wa kuanzisha kituo cha televisheni; licha ya kuwa walishaanza kununua baadhi ya vifaa.

Taasisi ya Utafiti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (BICO) baada ya kutokea mvutano kati ya Tanesco na kanisa hilo iliombwa kufanya utafiti wa vipimo na kutoa ushauri kwa Serikali. Ushauri wa taasisi hiyo ulionesha kuwa hakuna madhara ya kujengwa kwa njia hiyo ya umeme na serikali ikatangaza uamuzi kutokana na ushauri huo.
 
Tafakuri Yangu Ya Leo: Ya Kakobe na TANESCO mwogopeni Mungu tujaribu kwa Mafisadi




KAMA kuna jambo linalowakera watanzania basi ni hili la Ufisadi miongoni mwa baadhi ya viongozi wetu. Watanzania wanajiuliza, iweje wao waendelee kuwa masikini ilihali wachache wanazidi kuneemeka huku wakikodi ndege kwenda kutumbuliwa vipele huko Berlin Ujerumani? Sasa mimi nina pendekezo binafsi mkiona linafaa tulifanyie kazi wadau.

Hivi mnakumbuka enzi zile za mgogoro kati ya Askofu Zakaria Kakobe na TANESCO? , Kakobe aliendesha harakati zisizo na umwagaji damu akazipachika jina la "TANESCO Mwogopeni Mungu !!" na fulana za njano alichapa tunazikumbuka, Sasa kwa nini na sisi tusitumie mbinu hii kuwashughulikia Mafisadi?

Na hii iwe Tafakuri yangu ya leo jamani……

Nova Kambota Mwanaharakati
"Kitendawili sio deni ukishindwa nipe mji"
0717-709618 au 0766-730256
novakambota@gmail.com
novadream.blog.com
10 Machi 2011
Njombe , Tanzania.
 
Back
Top Bottom