Ngeleja akubali ushauri wa Sitta; awaomba radhi wabunge, watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngeleja akubali ushauri wa Sitta; awaomba radhi wabunge, watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 14, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Saturday, 13 August 2011 20:50

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]AWAOMBA RADHI WABUNGE, WATANZANIA

  Neville Meena, Dodoma

  BUNGE jana lilipitisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini huku baadhi ya wabunge wakiitahadharisha Serikali kuondokana na utamaduni wa kuwa na mipango ya dharura ambayo wamesema ni chanzo cha rushwa, wizi na ufisadi.Bajeti hiyo ilipitishwa jana baada ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Naibu wake, Adam Malima, kujibu hoja za wabunge na kuwasilisha mpango wa dharura wa kukabiliana na tatizo la umeme nchini.

  Ngeleja aliza kuijibu hoja kwa kuwaomba radhi wabunge na Watanzania kwa ujumla kuhusu makosa yaliyofanywa na wizara yake, hatua ambayo inatafsiriwa kuwa ni kukubaliana na ushauri tolewa hivi karibuni na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Samuel Sitta, jijini Mbeya akisema Serikali inapaswa kuwaomba radhi Watanzania kutokana na mgawo wa umeme.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba, alikuwa wa kwanza kutoa tahadhari hiyo pale alipoliambia bunge kuwa "Sasa dharura ifikie mwisho, na mpango huu wa dharura uwe wa mwisho maana haya mambo ya dharura yamekuwa kichocheo cha rushwa, wizi na ufisadi".

  Makamba pamoja na wabunge wengine walitoa kauli hizo Bunge lilipokaa kama kamati, baada ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuwasilisha mpango wa dharura wa kuliondoa Taifa gizani ambao utaigharimu Serikali Sh523 bilioni kwa miezi minne ambayo ni Agosti hadi Desemba, mwaka huu.

  Onyo la Wabunge
  Hoja ya ukomo wa mipango ya dharura iliungwa mkono na Mbunge wa Kibakwe (CCM), George Simbachawene na Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela ambao walisema mipango ya dharura katika sekta ndogo ya umeme ni chanzo cha ufisadi.

  Kilango alisema Serikali iwe na dhamira ya kweli ya kufikia mwisho wa mipango ya dharura katika kuzalisha umeme nchini na kwamba, taarifa rasmi za Bunge (hansard) zilizopo zinathibitisha uwepo wa dharura nyingi katika suala la uzalishaji wa nishati hiyo.

  "Tukubaliane, haya mambo ya dharura ndiyo yamekuwa yakitengeneza mianya yote ya ufisadi, sasa lazima tuwe na dhamira ya kweli ya kukomesha hali hii," alisema Killango na kuongeza:

  "Tunahitaji kuwa na uwezo kuzalisha umeme wetu wenyewe na kuondokana na dharura hizi, tuwe kama Msumbiji ambao wanauza umeme wao Afrika Kusini, tunaweza tukidhamiria".

  Naye Simbachawene alisema baadhi ya watu wanapenda dharura na kwamba, huenda wananufaika na uwezo wa dharura hizo. "Kuna wengine wanapenda kweli mipango ya dharura, mimi nadhani iwe mwisho na hali hii isiendelee tena," alisisitiza Simbachawene.

  Mbunge mwingine aliyezungumzia suala hilo ni Joseph Selasini wa Rombo (Chadema) ambaye alitahadharisha kwamba tatizo la umeme ni sawa mgonjwa ambaye anastahili huduma na kwamba wale wanaolishughulikia "wasinywe uji wa mgonjwa".

  Kwa mujibu wa Selasini, hoja za wasiwasi wa wabunge kuhusu miradi ya dharura ni za msingi na kwamba, uzoefu unathibitisha kuwepo kwa ufisadi, rushwa na wizi wa mali ya umma kupitia miradi hiyo.

  Alisema ikiwa ufisadi utaingia katika mchakato wa sasa wa mpango wa dharura ni sawa na kunywa uji wa mgonjwa na kwamba ikiwa hivyo, hali itakuwa mbaya zaidi kiasi cha kutishia uchumi na mustakabali wa nchi (mgonjwa atakufa).

  Mkamba
  Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli (CCM) alikosoa uamuzi wa Serikali wa kuweka sehemu ya mitambo ya Symbion katika mikoa ya Dodoma na Arusha akiseme ni ya gharama kubwa na ni lazima iwepo idadi kubwa ya magari ya kusafirishia mafuta.

  "Kusafirisha mafuta kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ili kuendesha mtambo wa kuzalisha megawati 100 unahitaji malori 50 ya kufanya kazi hiyo na malori 25 hapa Dodoma huku magari mengine yawe yanapakia. Hizi gharama hizi ni kubwa pengine Serikali ilitazame hili," alisema January.

  Mikopo ya Benki
  Baadhi ya wabunge wakiongozwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, walikosoa mpango wa huo wa dharura wa Serikali kutegemea zaidi fedha zinazotokana na mikopo ya benki ambayo ina riba kubwa za kibiashara.

  Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai (Chadema) alisema, "Kila mara zimekuwa zikitolewa kauli nzuri na Serikali hiihii na wizara hiihii ambayo ndiyo imetufikisha hapa tulipo. Sasa tungetaka watwambie wata-manage (watasimamia) vipi suala hili?" alihoji Mbowe na kuongeza:

  "Ni watu hawahawa ambao wameshindwa ku-deliver (kuleta tija) siku zote au Serikali inakubaliana na ushauri wetu wa kuunda task force (kikosikazi) kwa ajili ya kutekeleza mpango huu!"

  Alisema licha ya Serikali kuahidi kuwa fedha zilizokopwa zitalipwa, mzigo wa deni hilo utakaobebwa na Watanzania na ni matokeo ya uzembe wa Serikali ambayo imekuwa ikipanga mipango isiyotekelezeka.

  Alisema kwa kuwa Serikali imekopa kwa masharti ya kibiashara lazima tahadhari ichukuliwe ili matatizo ya umeme yasivuke mpaka na kusababisha matatizo makubwa zaidi kwa wananchi kupitia mikopo hiyo.

  Kwa upande wake, mbunge wa Ubungo, John Mnyika aliukosoa mpango huo huku akihoji sababu za Serikali "kukimbilia kukopa benki" badala ya kuchukua fedha katika matumizi yasiyo ya lazima.

  Alisema katika bajeti mbadala iliyosomwa na kambi ya upinzani, kulikuwa na mapendekezo ya vyanzo mbadala vya fedha ambavyo vingeiwezesha Serikali kupata zaidi ya Sh500 bilioni kama ushauri wake ungezingatiwa.

  Kwa mujibu wa Mnyika hata ahadi za Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliyoitoa wakati akiondoa bajeti ya nishati bungeni Julai 18, mwaka huu hazikuzingatiwa katika utafutaji wa fedha za dharura.

  Hata hivyo, Pinda alisema hawakuweza kupata fedha katika mafungu mengine ya Serikali kama ilivyoitarajiwa, ndiyo maana waliamua kutafuta fedha za mkopo kutoka benki.

  "Tanesco hadi sasa wana deni linalofikia shilingi bilioni 300, halafu leo hii tunaendelea kuwabebesha mzigo wa mkopo mwingine mkubwa. Tungeweza kuepusha kadhia hii kwa kutumia vyanzo vingine vya fedha. Hivi vipo vingi!" alisema Mnyika ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini.

  Kwa upande wake Ngeleja alisema wizara yake imechukua Sh10.3 bilioni kutoka katika matumizi yasiyokuwa ya lazima ndani ya Wizara na miongoni mwake ni kufuta mpango wa kujenga ofisi ya kanda ya madini jijini Dar es salaam na kufuta baadhi ya posho zisizokuwa na tija.

  Naye mbunge wa Mkanyageni, Mohamed Habib Mnyaa (CUF), alieleza kutoridhishwa na mpango huo wa Serikali kwa maelezo kwamba tatizo hilo ni la muda mrefu na kwamba ni wa gharama kubwa kwa wananchi.

  Mnyaa alisema zipo kampuni nyingi ambazo zinaweza kuziuzia Serikali mitambo ya umeme katika muda wa miezi miwili na kwamba, hoja ya Serikali kuwa ununuzi wa mitambo mipya ya kuzalisha umeme unahitaji mchakato mrefu, siyo ya kweli.

  Kadhalika Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP), alisema Serikali inapaswa kuacha utamaduni wa kutekeleza wajibu wake kwa kusukumwa huku akisema hana imani iwapo mpango huo utaweza kutekelezwa.

  Alitaka Tanesco kugawanywa ili kuleta tija ya shirika hilo ambalo licha ya kufanya kazi kwa muda mrefu limeshindwa kujiendesha kwa faida."Tanesco is overlodead (limezidiwa) kwa hiyo ninapendekeza ligawanywe katika sehemu tatu kama ambavyo imewahi kusemwa kuwa kuwepo sehemu ya generation (uzalishaji), transimission (usafirishaji) na distribution (usambazaji)," alisema Cheyo.

  Watendaji wa Wizara
  Baadhi ya wabunge pia walitaka Serikali kuchukua hatua dhidi ya watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini ambao wamekuwa kikwazo cha utekelelzaji wa mipango ya wizara hiyo.Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe alisema Serikali inapaswa kuwachukulia hatua watumishi ambao wamesababisha Tanesco kuwa Shirika la "usambazaji wa giza", badala ya kusambaza umeme.

  Alimtaka Waziri Ngeleja kuchukua hatua za kuisafisha wizara yake na kwamba, licha ya Katibu wake Mkuu kusimamishwa kazi kwa ajili ya kupisha uchunguzi dhidi yake, bado kuna watumishi wengine ambao wanatakiwa kuchukuliwa hatua ili kuwezesha kazi za wizara hiyo kufanyika.

  Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo kwa upande wake aliweka wazi kuwa wizara hiyo inahitaji kufanya mabadiliko makubwa ya kiutumishi ili kuwezesha mipango ya serikali kutekelezwa.

  Ngeleja aomba radhi
  Mapema wakati akijibu hoja za wabunge, Ngeleja aliwaomba radhi wabunge na Watanzania kwa ujumla kwa kile alichosema kuwa ni makosa yaliyofanywa na wizara yake.

  Hatua ya kuomba radhi inatafsiriwa kuwa ni kukubaliana na ushauri uliotolewa na Waziri Sitta katika mkutano wa hadhara wa CCM mkoani Mbeya hivi karibuni akisema Serikali ilipaswa kuomba radhi kutokana na matatizo ya umeme nchini.

  Hata hivyo kauli hiyo ya Sitta ilimweka matatani baada ya kushambuliwa waziwazi na baadhi ya makada wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, akiseme waziri huyo anaidhalilisha CCM mbele ya umma.

  Lakini jana Ngeleja alionekana kukubaliana na Sitta kwani alitumia takriban dakika kumi kuomba radhi kwa kile alichosema kuwa ni makosa yaliyofanywa ama na yeye mwenyewe akiwa waaziri mwenye dhamana au na watendaji wake katika wizara hiyo ya nishati na madini.

  "Leo nawasilisha bajeti hii ikiwa ni mara yangu ya nne, napenda kumshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa yale ambayo yalijitokeza pengine yamenigusa mimi kuliko yalivyowagusa wabunge wengine," alisema Ngeleja na kuongeza:

  "Yapo mambo ambayo hayajawahi kutokea nikiwa katika wizara hii ya nishati na madini. Lakini ninaamini kutenda kosa si kosa, bali kurudia kosa ni tatizo kubwa sana".
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Ngeleja msanii tu, ameomba msamaha ili kutetea kitumbua chake na si vinginevyo, anatia huruma lakin hakuna jipya litakaloleta matumaini kwani Ngeleja ni yule yule mapungufu yake ni yale yale katika serekali ile ile ikiongozwa na rais yule yule legelege.
   
 3. m

  mfngalo Member

  #3
  Aug 14, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mi Ngeleja namshaur aache usanii (1..2..)2mekaakimya 3 utatoka kwa nguvu a2taki usanii sahv
  Na kuhusu Jairo vp?mbona kimya sn 2naanza kupata wacwac
   
 4. Teacher1

  Teacher1 JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Huku Kyela umeme unawaka saa nane za usiku na kukatika saa moja kasolobo asibuhi sasa huu umeme wanataka utumiwe na wachawi au watu gani maana hata siku moja haupatikani mchana wala jioni jioni tumechoka sana
   
 5. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Kwa mtazamo wangu Ngeleja na timu yake pale nishati na madini hawana uwezo wa kusaidia kutatua tatizo tulilonalo la umeme....Hawana uwezo huo jamani maana energy level yao kuhusu suala hili iko chini. Kama hatuweki maslahi ya Taifa mbele tunatanguliza rushwa, forget about resolving this problem...stop using tax payers money calling investors, and we should all sleep comfortably in our country without disturbing anyone because our way out would be waiting a miracle from another planet.
   
 6. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Tatizo siyo Ngeleja bali ni (System) mfumo wa viongozi wote wa chama cha mapinduzi,hakuna anayewatetea wananchi wanatetea matumbo yao tu(MAFISADI)
   
 7. W

  We know next JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Bunge linabidi sasa kuwajibika, haiwezekani likakubali uongozi uleule uende ukatekeleze yaleyale yaliyowashinda miaka karibu mitano iliyopita. Watanzania, nadhani ktk dunia ya leo, hakuna tena ile mipango ya kujaribu kuona kama tutafanikiwa, hiyo inaonyesha madhaifu makubwa sana ktk suala zima la mipango mikakati kwa Serikali. Mimi nilitegemea Bunge kukomaa na kukubali kuipitisha bajeti ile lakini watendaji wawe wengine na sio hao watuhumiwa wa ufisadi ambao mpaka leo eti wanapewa likizo. Makosa yalifanywa na Bunge ktk hili, yatalijutia.
   
 8. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Upuuzi huu,wametuambia watapunguza mafuta kumbe uongo,serikali waongo
   
 9. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
   
 10. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni kubwa kuliko Ngeleja na wizara yake!!

  Kumtaka yeye ajiuzulu ..then Turidhike ... ni kumpa yeye na serekali yake heshima wasiyopaswa kupewa!
   
 11. F

  FUSO JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,856
  Likes Received: 2,333
  Trophy Points: 280
  Kwa maneno mengine mepesi ni kwamba kambi ya kina SIX imeshinda mtanange huu.
   
Loading...