Ngeleja akiri kazi aliyopewa ngumu

Hawakufunzwa uadilifu? Nitasema kweli daima , fitina kwangu mwiko . Hata rahisi kama hili Waziri mzima hawezi kuzingatia. Atazingatia nini sasa
Hopeless Minister
 
Huyu bwana ni msanii, na zaidi ya hapo anaamini watanzania walio wengi hawatunzi kumbukumbu yaahadi za viongozi wao; kutokana na hayoNgelenja ni mwepezi kusema lolote ili mradi siku ipite.
 
Huyu bwana ni msanii, na zaidi ya hapo anaamini watanzania walio wengi hawatunzi kumbukumbu yaahadi za viongozi wao; kutokana na hayoNgelenja ni mwepezi kusema lolote ili mradi siku ipite.

ni mpumbavu ambaye sijapata kuona...kama china angenyongwa kabisa!!!!
 
Ki ukweli ngeleja nae kashindwa kazi, kakalia maneno tu na kutaka kumlzisha bosi wake huku wananchi tunasota, wawe wakweli watofautishe siasa na utendaji.
 
Hii ngoma Ngereja sijui huyu mkwele kaiokota wapi ? Migao kibao, mafuta bei juu, umeme bei juu, yote haya ndani ya wizara yake ila yeye anacheka tu haoni kama ni tatizo!
 
Hii ngoma Ngereja sijui huyu mkwele kaiokota wapi ? Migao kibao, mafuta bei juu, umeme bei juu, yote haya ndani ya wizara yake ila yeye anacheka tu haoni kama ni tatizo!

Umesahau gesi ... Ni aibu
 
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Ngeleja amenakiliwa na gazeti la Majira la leo akibea msimamo wa TUCTA kuandamana nchi nzima kushinikiza bei ya umeme isipande kwa vile itakuwa ni mzigo mkubwa kwa wafanyakazi wenye kipato kidogo...

La kushangaza ni sababu ambazo Ngeleja alizitumia akidai watanzania siyo wajinga wa kuburuzwa na watu ambao wenye masilahi binafsi.................

Hivi kweli kushinikiza kutopanda bei ya umeme ni masilahi binafsi au ni ya umma?

Ngeleja abeza msimamo wa TUCTA


Na John Daniel

WAZIRI wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja amekejeli tishio la Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), kutaka kuandamana kupinga ongezeko la bei ya umeme na kueleza kuwa Watanzania si wajinga kuburuzwa na watu wenye
maslahi binafsi.

Alisema kiwango cha juu kilichoidhinishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (UWURA) ni sh. 28 kwa kila uniti moja katika matumizi ya kawaida, kiasi ambacho kwa mujibu wa Bw. Ngeleja si kikubwa kama inavyotafsiriwa na TUCTA na baadhi ya watu.

Kwa kiwango hicho, mteja wa TANESCO alikuwa anatumia uniti 100 za umeme kwa mwezi, kuanzia Jumapili atalazimika kutoa sh 2,800 zaidi ya bei aliyokuwa anatoa awali.

"Nilichoelewa ni kuwa TUCTA walikurupuka kutoa kauli bila kujua ukweli wa kiwango gani kilichoidhinishwa, kilichoongezeka kwa kila uniti ni sh. tano, sh. tisa, sh. 11 na kiwango cha juu kabisa ni sh. 28, kutegemea na aina ya matumizi.

"Hivi ni nani akipewa sh. 28 anaweza kununua chochote kwa dunia ya leo, wasidhani Watanzania ni wajinga wanaweza kuburuzwa tu na fikra binafsi za watu kujitafutia umaarufu hapana tutafute ukweli jamani," alihoji Bw. Ngeleja.

Alisema TANESCO iliomba ongezeko hilo kutokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji na kwamba mara ya mwisho bei hizo ziliongezwa Januari 2008.

"Serikali kwa maana ya TANESCO inatambua uwezo wa wateja wake ndio maana inajitadi kubeba sehemu kubwa ya gharama za umeme, ukiangalia tangu mwaka 2008 bei ya vitu ikiwemo mitambo imepanda kwa kiasi kikubwa," alisema Waziri Ngeleja.

Tanesco ilikuwa imeomba ongezeko la asilimia 34.6 lakini EWURA baada ya kusikiliza hoja za wadau ikapitisha asilimia 18.5.Wakati huo huo TANESCO imetoa taarifa inayoonesha mchanganuo wa ongezeko la bei mpya ya umeme kwa watumiaji kulingana na matumizi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kundi la watumiaji wadogo majumbani (D1) itapanda kwa sh. 11 kwa uniti moja hivyo kuwa sh. 60 kwa uniti badala ya sh.49 za awali.

Kundi la watumiaji wa kawaida (T1) ambao ndio wamepanda zaidi watalipa sh 157 kwa uniti moja kutoka sh. 129 za awali, sawa na ongezeko la sh. 28 kwa uniti moja.

Taarifa hiyo ya TANESCO imetaja kundi la mahitaji ya juu ya msongo mdogo (T2) kuwa na ongezeko la sh. tisa kwa kila hivyo na kufikia bei ya 94 kutoka sh. 85 za awali.Kundi la mahitaji ya juu ya msongo mkubwa (T3/T3a) ongezeko ni sh. tano kwa uniti, hivyo kupanda kutoka sh. 79 ya awali hadi sh. 84.

Kundi la mwisho linalohusu Tanzania visiwani (T5/T3b) ongezeko ni sh. nane kwa uniti moja hivyo gharama zitapanda kutoka sh. 75 hadi 83 kwa kila uniti moja.Wiki iliyopita Kaimu Katibu Mkuu wa TUCTA, Bw. Nicholas Mgaya, aliitaka Serikali kufuta uamuzi wa kupanda kwa bei ya umeme na kutishia kuandaa maandamano ya amani nchi nzima kupinga hoja hiyo.

Bw. Mgaya alisema Kamati ya Utendaji ya TUCTA ilifikia maamuzi hayo kwa maelezo kuwa ongezeko hilo ni kubwa na haliendani na hali ya Mtanzania na hivyo litazidisha ugumu wa maisha kwa wafanyakazi na Watanzania kwa ujumla.




2 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Ama kweli mambo yamebadilika Zamani ongezeko la bei linaangalia yule wa kima cha chini (kawaida) inaongezwa asili,ia ndogo, siku hizi yeye inakuwa asilimia kubwa Kwa sasa kuna ongezeko la sh 5 mpaka 28 Watumiaji wakubwa ni sh 5 watumiaji wa kawaida sh 28 Jamani tuhurumiane
December 28, 2010 8:29 PM
blank.gif

Anonymous said... Mimi nadhani viongozi wa TUCTA wako sawa kama kima cha chini cha mshahara ni laki moja na nusu ukiongeza bei ya umeme umeongeza bei ya kila kitu. Ingekuwa ni umeme tu umepanda watu wangekubali ila kila kitu kimepanda gharama mara tu baada ya uchaguzi. Je Mtanzania wa kawaida ataweza kumudu hali hii?
Ukiangalia Mtanzania wa kima cha chini ndiye anayetakiwa kulipa zaidi kuliko anayetumia umeme meingi Je huu ni uungwana? Inasikitisha sana kuona hali kama hii kila kitu Tanzania kimekuwa shaghala baghala ni heri kutawaliwa na mkoloni kuliko kuwa mtumwa chini ya mtanzania mwenzako. INASIKITISHA na INAUMA SANA.
Watanzania tuamke.
December 28, 2010 8:37 PM
 
Nionavyo mimi Ngeleja is an insulated leader ambaye haelewi nchi hii inatoka wapi, iko wapi na yaelekea wapi na ndiyo maana kilio cha wananchi dhidi ya kupandishwa kwa bei ya umeme hakioni kuwa ni masilahi ya kitaifa na ndiyo maana anakibeza kuwa ni masilahi ya watu wachache tu kwa maana ya viongozi wa TUCTA...

Hata hizo jitihada za kupeleka umeme vijijini ni bure kabisa kama bei hiyo itakuwa nje ya uwezo wa wanavijiji walengwa.

Wananchi wenye kipato kidogo wataishia kuzikodolea macho nyaya za umeme na nguzo zake lakini kamwe hawataweza kuufaidi umeme huo ambao unapita karibu kabisa na makazi yao.
 
Ngoja tu na hizo dhihaka zake miguu isije ikaota matende.

Maana kwa mgomo wa Wafanyakazi Tanzania hapo ni kwamba watu bila shaka watakua wanatetea usallama na uhakika wa kula ya watoto hapo na ndiyo maana napata hofu sana mimi.

Ogopa sana ugomvi wa kukupambanisha na mtu anayepigania KULA YAKE.
 
Ngoja tu na hizo dhihaka zake miguu isije ikaota matende.

Maana kwa mgomo wa Wafanyakazi Tanzania hapo ni kwamba watu bila shaka watakua wanatetea usallama na uhakika wa kula ya watoto hapo na ndiyo maana napata hofu sana mimi.

Ogopa sana ugomvi wa kukupambanisha na mtu anayepigania KULA YAKE.

Huu ni ukweli kabisa..........................
 
Huyu Mgaya aache kuwachanganya wafanyakazi. Toka aabandon ule mgomo wa May mimi sina imani naye tena. Actually, wafanyakazi ilibidi wamtoe watafute kiongozi bora zaidi ya huyu jamaa. Mgaya ni muoga na hawezi kuandaa kitu kama hicho. Anabeep tu!!
 
Huyu Mgaya aache kuwachanganya wafanyakazi. Toka aabandon ule mgomo wa May mimi sina imani naye tena. Actually, wafanyakazi ilibidi wamtoe watafute kiongozi bora zaidi ya huyu jamaa. Mgaya ni muoga na hawezi kuandaa kitu kama hicho. Anabeep tu!!


kweli kabisa Mgaya he is not firm in his decision
 
Ngeleja unabore na mipnago yako ya umeme kila siku.
Halafu ume kremu yaani wakati unatoa mipango ya uzalishaji ni kama vile unaimba jinsi ulivyo kremu.

This is boring with your fake plans we need powerrrrrrrrrrrrrrrrrr

Wabunge walikuwa wanacheka wakati unatoa mipango.
 
hata mimi nimeshuhudia vicheko wakati anatoa mada kwani hata yeye mwenyewe anajua kuwa anachoongea anakirudia kila siku, halafu kuna haja gani ya spika kilipinga swali la mbowe kwa ngeleja kuwa! ni lini hasa mgao wa umeme utaisha nchin?,
 
Wandugu namshauri Ngeleja na wanajamii wote, kusoma kibonzo kilichopo kwenye gazeti la Tanzania Daima la leo ukurasa wa 7. Niliumia lakini baadaye nikajistukia nacheka.Inaonyeswa picha ya ndege (airplane) na chini yake kuna milio mbali mbali. Rubani anawafahamisha abirua wake kama ifuatavyo "Ndugu abiria mkisikia kelele za majenereta, mjue ndio tumeingia Tanzania" Doh hii ndiyo Tanzania, kwa nini JK asikubali kushindwa? anangojea yanayomsibu mwenzake wa Misri?
 
Ishu ya Mgao inaonekana ni mpango wa wakubwa; watatumia kigezo cha kutokuwa na Umeme kwa sasa ili baadae waombe misaada wa mitambo mingine kama ya Dowans wakijua watanzania tutaafiki ili waendelee kuchakachua.

Tanzaniia si nchi ya kukosa umeme kiasi hiki: Almas-Mwadui, Tanzanite-Arusha, Makaa ya mawe-Liganga vyote vinaenda wapi'? Kwanini tusiuze hivyo tukapata Nishati?
 
Mipango ni mingi na ni mizuri lakini yote inaishia kwenye makaratasi...
 
ngeleja needs a chop, kama kuna uchawi basi huyu jamaa analindwa na uchawi balaaa

he is just crappy minister aliyezoea kuahidi bila tathmini yoyote ya utekelezaji
 
Yaani spika kuzuia swali la lini mgao wa umeme utakwisha mimi naona ni ujuha. Hilo ni swali la msingi kabisa lakini mtu analitolea nje. Anyway tutafika tu hata kama ni kwa kuchelewa.
 
Back
Top Bottom