Ngeleja Again

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,143
3,196
Namhurumia sana Ngeleja na ninamsikitikia. Wizara aliyoshikilia ni kubwa kuliko uwezo wake wa akili, maono na hata fikra. Kwa hali ilivyo nchini ni kama wizara ya Nishati na madini ndiyo mzigo mkubwa kwa taifa na uchumi wa Tanzania. Wakati tatizo la umeme halijatulia, tayari limeshajitokeza la mafuta, wakati huo huo, mgogoro wa meremeta ukiwa unaendelea kufukuta. Hapo hatujasahau mauaji ya raia yaliyofanywa na polisi katika mgodi wa barrick. Pia tuna kumbukumbu nzuri ya ongezeko la gharama za umeme kwa asilimia 18. Kinachosikitisha na kuhuzunisha, ni pale ambapo waziri husika hana hata sauti juu ya yanayotokea. Lakini najiuliza, hivi tatizo ni nini?

1. Mipango mibovu ya wizara?
2. Ten percent ya baadhi ya viongozi katika wizara husika?
3. Rais wa nchi hana uwezo wa kusimamia sheria na taratibu za kila wizara?
4. Waziri mbovu?
5. Waziri mkuu mbovu?
6. Rais mbovu?
7. EWURA inafanya nini? Na ipo kwa shughuli gani?

Na ni nini suluhisho la haya yote? Maana maisha magumu nchini kisa ni gharama kubwa ya mafuta na umeme! Ni kama wizara hii ndo ilyoshikilia uchumi wa nchi? Wafanyabiashara wa mafuta wamekuwa wakijipandishia bei za mafuta kwa namna wanavyojisikia wao bila kujali hali halisi ya maisha. na hakuna aliyekuwepo kuwakemea. Leo wameshushiwa kodi za mafuta, lakini bado wanatia mgomo kupunguza bei. Ni akina nani hawa katika nchi yetu? Hivi Rais au wizara husika haina mamlaka ya kufuta lessen zote na kuitisha wabia wapya watakaokubali kuuza mafuta kwa kufuata taratibu za nchi?

Hii ni serikali gani isiyokuwa na kauli dhidi ya wananchi wake? Kama kweli ina uhakika kwamba wafanyabiashara ya mafuta wanapata faida kutokana na kuuza mafuta kwa bei ile iliyopangwa, serikali inashindwaje kulazimisha? Mbona Mkapa aliyaweza haya mambo, pale alipotishia kuzifutia daladala zote lesseni za usafirishaji? Ni nini hasa tatizo lililopo katika serikali hii?
 
Back
Top Bottom