Ngeleja acha kutufanya watanzania wapumbavu.

Nduka Original

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
1,012
815
Kweli inakera saaaaaaaaaaaana kwani tunaishi maisha ya kubahatisha. Huwezi kuplan kitu chochote kila kwasababu haujui nishati ya umeme inapatikanaje.

Kama Arusha imekuwa ni upumbavu mtupu. Kwa siku tatu sasa umeme haujulikani unakuja saaa ngapi wala unakatika saa ngapi. This is terrible. Kinachoniuzi wiki iliyopita Ngeleja akasema kuanzia wiki hii mgao utapungua kwa kiasi kikubwa kwani Symbion, IPTL na nani sijui wameanza kuzalisha umeme.

Kweli this is ridiculous na Ngeleja kubali kwamba kazi umeshindwa achia vijana wengine competent, I am not sure if you know what you are doing, you are not serious and worse enough wala hili swala halikunyimi usingizi that's why you never miss your hangouts, Fiesta etc.

Ndo natoka ofisini hivi kwani umeme ndo kalasi
 
Mkuu hili limeshakuwa tatizo la Arusha
Siku nne hakuna umeme wala ile ratiba iliyokuwepo haifuatwi yaani tunaishi kwa kubahatisha tuu
Yaani nina siku tano sijauona umeme na wala sijui unarudi au kukatika muda gani maana kama upo ni usiku wa manane na unaondoka muda huo huo wa manane
Sasa sijui ni tatizo la Arusha tuu au na kwingine
 
Yani its terrible am telling you. Ukiwapigia TANESCO wanakupa majibu ya kipumbavu kabisa huku wakicheka. Naomba mwenye namba ya Ngeleja anipatie niongee nae moja kwa moja.
 
Yani its terrible am telling you. Ukiwapigia TANESCO wanakupa majibu ya kipumbavu kabisa huku wakicheka. Naomba mwenye namba ya Ngeleja anipatie niongee nae moja kwa moja.

Mkuu hana la maana
Maana siku aliposema kuwa mgao utapungua ndo ilikuwa kiama ya Arusha na wanaarusha maana ndo hii ratiba yao isiyoeleweka ilianza
Maana kama unaweza kukaa siku tano hujauona umeme unategemea nini
Na ukiwepo ni saa moja tuu umekatika tena na ni usiku wa manane wala sio muda wa kazi
Ishakuwa sugu sasa maana Arusha ni kama tunaonewa
 
Yani its terrible am telling you. Ukiwapigia TANESCO wanakupa majibu ya kipumbavu kabisa huku wakicheka. Naomba mwenye namba ya Ngeleja anipatie niongee nae moja kwa moja.

Nduka Original, wala usitake namba yake huyo Mr. Megawati atakuumiza kichwa bure achana nae.
 
KLM imeshidwa kuondoka jmosi saa 5 usiku kisa uwanjani hakukua na umeme,abiria wakapelekwa double tree hilton hotel kulala aibu gani hii kwa taifa.Mwenye hotuba ya Ngeleja ya kupitisha bajeti ile ya pili aiweke hapa tuone,jamaa alisema sept megawat kadhaa zingekuepo na tatizo kupungua..serikali punguzeni uongo muda si mrefu tutawapindua tumechoka.
 
Mkuu hili limeshakuwa tatizo la Arusha
Siku nne hakuna umeme wala ile ratiba iliyokuwepo haifuatwi yaani tunaishi kwa kubahatisha tuu
Yaani nina siku tano sijauona umeme na wala sijui unarudi au kukatika muda gani maana kama upo ni usiku wa manane na unaondoka muda huo huo wa manane
Sasa sijui ni tatizo la Arusha tuu au na kwingine

Ni kweli Mkuu, hata mie hua najuiliza kama hili tatizo linaapply kwa Mikoa yote.
 
Duh....! kumbe bora sie tuliopo "Tanzania E", maana tunatumia umeme wa Zambia....!
 
Nduka Original, wala usitake namba yake huyo Mr. Megawati atakuumiza kichwa bure achana nae.
Wacha achukue namba amp vidonge vyake wananchi kutulia na kukaa kimyaa anazidi kutuona wajinga wakati yeye anaendleza ufisadi na wizi kwenye madini na kununua mafuta mazito hewa kwa kusingizia dharura ya umeme na hata ukikutana njiani na mtu kama huhy ni kumpiga fimbo na mawe. Kuzalisha umeme wa kutosha inawezekana isipokuwa tunateseka kwa sababu ya ufisadi wa akina Ngeleja na kundi lake ndio wanafanya wizi wa mchana na umeme kuonekana hautoshi kila siku miaka nenda rudi
 
Ni kweli Mkuu, hata mie hua najuiliza kama hili tatizo linaapply kwa Mikoa yote.

Hili tatizo lipo mikoa yote...umeme hauna ratiba...unaweza katika mara 3 ndani ya saa moja.
Kila Ngeleja akitoa tamko hali inakuwa mbaya zaidi...akitoa tena ndio umeme unakatika nchi nzima.
 
maneno mawili ya mwisho kwenye kichwa cha hii post mbona kama yana chembechembe za ukweli,
kinyume chake tungepinga kwa nguvu zetu zote
tungeingia mtaani mpaka kingeeleweka,
tungewazomea si wao tu mpaka kuku wao,
tungewanyima ushirikiano wa namna yoyote katika jamii,
kuna wakati kipindi cha utawala wa ben, MUNGU alitusikia kwa mbaali, alishusha tetemeko dogo wakati bunge likiendelea dodoma, sumaye alichukua medali ya dhahabu kwa kutoka mkuku mjengoni, tukalcheka badala ya kuendelea kufikisha kilio chetu kwa muumba wetu.
sichochei vurugu bali ngeleja achochea,
sihujumu uchumi bali ngeleja+ccm wanahujumu
kama inawakera tuuondoe huo ujinga,
kama mahali pa kuwaka umeme hauwaki nasi tunachekacheka hatufanani na wajinga bali ndio wajinga wenyewe.
 
Hawa watu wanaajenda ya siri.kilochobaki sasa ni kuingia barabarini kudai umeme.bila hivyo tutaona rangi zote
 
Mzee wa megawatt atakuambia tuu kuwa mchakato unaendelea na grid ya taifa imeongezewa megawatt 30 ndo maana mgao unapungua

Nafikiri mpaka sasa neno mchakato litakuwa limepoteza maana yake ya asili, sijui kwa sasa lina maana gani toba yarabi?!
 
Yani its terrible am telling you. Ukiwapigia TANESCO wanakupa majibu ya kipumbavu kabisa huku wakicheka. Naomba mwenye namba ya Ngeleja anipatie niongee nae moja kwa moja.
<br /> <br /ALIVYONADHARAU hatapokea simu yako na AKIPOKEA ATAKUJIBU NYODO.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom