Ngekewa(Capybara): Mnyama pekee apendwae na wanyama wote

KAFA.cOm

JF-Expert Member
Jun 22, 2013
1,301
739
Je, wajua kuwa Capybara ndio mnyama rafiki kwa wanyama wengi ikiwemo crocodile (mamba), chui na simba?!..

Huyu ni rafiki mkubwa wa Anaconda na Nyegere.

Pia soma...
- Naomba mnieleweshe maana ya ''ngekewa''

===========

Mnyama anayefahamika kwa jina la kigeni Capybara ambapo kwa kiswahili huitwa Ngekewa ni mnyama mwenye ukubwa wa sentimita 134 na uzito unaokadiliwa kuwa kilo 66 anapokuwa mkubwa na mnyama huyu asili yake ni nchi ya America ya kusini.

Ni mnyama ambaye anapenda kukaa karibu na maji na anapojisi hatari hulazimika kukimbilia ndani ya maji na ana ujuzi mkubwa wa kuogelea.

Akiwa ndani ya maji anaweza kutumia dakika tano bila kuibuka ambapo hubana pumzi ndani ya maji anapokwepa hatari ya kushambuliwa na adui yake.

Huyu Ngekewa ndio mnyama anayependwa na viumbe vingi vya porini na majumbani.

Wanyama kama mamba, chatu, nyani, paka, kobe na hata ndege wa aina mbali mbali hupenda kukaa karibu naye na kufurahia maisha hivyo mnyama huyu huhesabika kama kiumbe chenye bahati ya kupendwa na viumbe wengine ukiondoa maadui zake.
capybara.jpg
Kwenye kamusi ya lugha ya kiswahili neno Ngekewa mbali na kumzungumza huyu mnyama pia limetafsiliwa kama bahati au yenye bahati na ndio maana hata mtaani mtu mwenye bahati huambiwa ana ngekewa.

Asili ya maana ya neno ngekewa ipo katika kupendwa kwa huyu mnyama na viumbe mbali mbali hata vile vya hatari.


Picha

cd11d58b8071e476c76ca1fdc2e52436.jpg
9ffb772bf9aea054441822e472c22436.jpg
fcc0a9536e18d56a47d7ab73952641bb.jpg

 
Wanyama wanauwezo wa kusoma nafsi ya mnyama mwenzake kasoro binadamu (labda awe ameaquire uwezo fulani wa kipekee/spiritual anointing). Ukiwa mnyenyekevu wa roho na mpole moyoni baada ya kukutanisha macho, mnyama anatambua hilo na anakuwa hana wasiwasi na wewe. Sishangai kwa mnyama Cabybara kuwa rafiki wa wanyama wenzake.
 
Back
Top Bottom