Ngedere wanamaliza mahindi shambani naombeni mbinu za kuwadhibiti

Deontic

Member
Aug 26, 2020
14
7
Kama kichwa kinavyojieleza, nimelima shamba la mahindi kama ekari mbili maeneo ya Mufindi Iringa , mahindi yako kwenye hatua ya kuanza kuchanua.

Sasa Leo nimeenda kuangalia nimekuta jana wameshindia kuvunja vunja yale yaliyokuwa yameanza kuweka mahindi karibia shamba lote, naombeni mnisaidie niweze kuokoa yaliyobakia na niweze kuwadhibiti Kabisa hawa Ngedere.
 
Samaki wakavu ni balaa kwa nyani
Funga samaki kwenye baadhi ya mahindi na pindi watakapogusa ile harafu hawaipendi kabisa
Kwa hiyo watajaribu kuifuta kwa mikono mpaka damu iwatoke na huo utakuwa mwisho wao kuja hapo

Lingine huko India wao wana Tiger wengi kwa hiyo nyani wanaogopa hao jamii ya chui na wamebuni kuwapaka rangi mbwa waonekane kama chui
Ila kwetu hatuna tigers unaweza kuwapaka mbwa rangi kama ya chui wetu huko
IMG_6064.jpg
 
View attachment 1720566
Shukrani mkuu
 
Hao ngedere watazame vizuri usoni utaona wamefanana na baadhi ya member wa jf
 
Piga maombi mkuu, hakuna linaloshindikana mbona Corona tumeishinda kwa maombi.
 
Hao ngedere hata ukiua mmoja watakuja na ukitumia Gobore watakaa siku mbili tatu then watarudi hapo weka watu walinde na mbwa every day
 
Funga mbwa kwenye njia zote amabzo ngedere wanazitunia kuingia shamba kuanzia saa 12 asubuhi hadi 12 jioni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom