Ngedere wanaharibu mazao msaada tafadhali.

Sammo Hung

JF-Expert Member
Aug 4, 2017
1,142
1,302
Habari za wakati huu!
Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza, ninasumbuliwa sana na wanyama waharibifu hususan ngedere shambani kwangu. Nimetumia mbinu mbalimbali mfano kuwatega mitego, kuwafukuza kwa kutumia mbwa n.k ila mbinu zote hizi zimefeli. Kwa yeyote ambaye anafahamu mbinu mbadala ya kuwadhibiti anifahamishe au kama kuna aina ya sumu ya kuwawekea isiyo na harufu pia itakuwa nzuri zaidi maana ni wajanja mno ukiweka sumu ya kawaida hawali wanasikia harufu.
Nawasilisha.
 
Fuga mbwa, nenda kariakoo sokoni pale juu utapata sumu.
 
Mbwa imeshindikana mkuu, wanajigawa makundi ukienda na mbwa upande huu wengine wanaingia upande ule. Ningepata jina la sumu ingekuwa bora maana nipo mkoa

"Cheka na ngedere uvune mabua"

Kila kiumbe kina akili ambayo ndio msaada/mtaji wake wa kukabiliana na mazingira.

Jitahidi kukabiliana nao, tumia kila aina ya mbinu ili uweze kuwazibiti

Suala la sumu naona unaweza kuweka sumu halafu ukaambulia mambua tu maana wao haijui sumu, ni mwendo wa kuvamia tu.

Mara nyingi watu huwa wanafunga matambara/ vitambaa kwenye mimea ili ionekane kama ni mtu ambapo ngedere akiona anaweza kuogopa na asiweze kuvamia mazao
 
Mbinu ya kwanza ni kupiga kuua mmoja kwa bunduki, akifa mmoja au wawili wanahama. Nenda kwa afisa wanyama pori aliyekaribu ili aifanye kazi hata ya kuwatisha kwa mizinga kadhaa.
 
Habari za wakati huu!
Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza, ninasumbuliwa sana na wanyama waharibifu hususan ngedere shambani kwangu. Nimetumia mbinu mbalimbali mfano kuwatega mitego, kuwafukuza kwa kutumia mbwa n.k ila mbinu zote hizi zimefeli. Kwa yeyote ambaye anafahamu mbinu mbadala ya kuwadhibiti anifahamishe au kama kuna aina ya sumu ya kuwawekea isiyo na harufu pia itakuwa nzuri zaidi maana ni wajanja mno ukiweka sumu ya kawaida hawali wanasikia harufu.
Nawasilisha.
Mshike mmoja usimwue wala kumjeruhi. Tafuta kakengele kadogo kama wanachofungiwa mbuzi ili wasipotee. Mfungie na mrudishe kwa wenzake. Hutawaona tena maana yule mwenye kengele akiwafuata watakuwa wanamkimbia nae kuwakibilia. Mpaka afe ndio utawaona tena.
 
ni balaa
 
Mkuu hiyo mbinu inafanya kazi kweli maana nimeshawahi kuisikia mara kadhaa. Shughili itakuwa kumkamata akiwa mzima sasa..
 
Wakuu hakuna anayefahamu sumu kali isiyo na harufu niwakomeshe wao na vizazi vyao
 
Habari za wakati huu!
Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza, ninasumbuliwa sana na wanyama waharibifu hususan ngedere shambani kwangu. Nimetumia mbinu mbalimbali mfano kuwatega mitego, kuwafukuza kwa kutumia mbwa n.k ila mbinu zote hizi zimefeli. Kwa yeyote ambaye anafahamu mbinu mbadala ya kuwadhibiti anifahamishe au kama kuna aina ya sumu ya kuwawekea isiyo na harufu pia itakuwa nzuri zaidi maana ni wajanja mno ukiweka sumu ya kawaida hawali wanasikia harufu.
Nawasilisha.
Tengeneza horny speak rekord tangazo weka flash na solar piga play back inakuwa kama kariakoo. TANGAZO TANGAZO...ONYO KALI.....................NGEDELE ATAKAEKAMATWA ATAUAWA.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom