Wakuu naomba niulize. Nimeona Mzumbe University wanatumia salary scale ya PGMSS. Je, mishahara yao inakuwaje, tafadhali? Mathalani, mshahara wa PGMSS 7.1 unaweza kuwa kiasi gani?
 
wadau ivi mtendaji wa kijiji na kata wenye elimu ya certificate na diploma respectively wanapokea shilingi ngapi
 
Wakuu naomba niulize. Nimeona Mzumbe University wanatumia salary scale ya PGMSS. Je, mishahara yao inakuwaje, tafadhali? Mathalani, mshahara wa PGMSS 7.1 unaweza kuwa kiasi gani?
Ukiipata na nijuze tafadhali.
Bila kusahau na ile ya PGMSS 1.1
 
Sasa ndugu zangu Walimu hapo hali ikoje maana nimeshafanya huko hakuna posho,allowances mpaka pesa za Likizo ni mwezi hadi mwezi au Mpk uchaguzi na Sensa...Poleni sana.
 
Naomba kujua mshahara wa afisa ustawi was jamii diploma level na changamoto pia hata fursa zilizopo kwenye kada hii kwa sasa ni medical attendant kwa mwenye uelewa naomba msaada wa mawazo maana nataka kuhamia huko
 
Write your reply...wapendwa samahani mimi ni mesomea basic technician certificate in accountancy nitafanye ili kupata ajira mana nimekosa pesa ya kujiendeleza naombeni ushauri wenu nina uzoefu mkubwa katika makampuni mbalimbali ambayo nimejitolea naombeni msaada wenu
 
Usichane resume yako. Badala ya kuomba hiyo kazi, sasa omba ukurugenzi, ukatibu mkuu, ukuu wa wilaya/mkoa. Ukishindwa omba basi hata ubunge manake utaweza kupata na uwaziri halafu mshahara wako pamoja na marupurupu yanaanzia mil 3 hadi karibia 20 kwa mwezi. Sio unaona kunavyolipa serikalini?

Ukishindwa vyote hivyo, hata ukatibu wa ccm wa wilaya? manake nako unaanzia na zaidi ya milioni! Hii nchi si inawenyewe? kama hutaki kuwa miongoni mwao, basi utaishia na hivyo vilaki 2 au 3 vile!

Hii post yako imenikumbusha mbali kweli. "Mtoto wa nyani alipomuuliza mama yake, mpaka wa shamba lao ili asijekula mahindi yasiyokuwa ya kwao. Mama alimjibu, kula tu mwanangu wenyewe watakuja kugawa". Tanzania, wanaendelea kula tu, hadi wenyewe watakapokuja kugawa! maybe in 50 or 100 years to come! who knows/cares? Don't you see them keeping a distance?
Hivi wenye shamba ndio wamekuja kugawa mpaka wa shamba sasa?
Maana kazi ya Mzee Magufuli sio mchezo.

Nyani wanakula shamba la mahindi kwa woga sasa.
 
Back
Top Bottom