Habari wadau, kwa anayejua, nilitaka kujua TCAA salary scale 7 ni mshahara wa shilingi ngapi.

ahsante
 
jamani mkiwa mnaandika habari humu wekeni full details kama wasomi,Tanzania kuna taasisi nyingi za serikali na kuna mashirika mengi pia ya serikali na private sio rahisi kila mtu ajue hiyo TCAA ni nini?
mara mia ungesema TCAA NI NINI BASI? hata hivyo unaweza kwenda ofisini kwao ukaonana na mtumishi wa hao moja akakufafanulia
 
Wanabaraza naomba mnitoe tongo tongo TGS D (Tanzania Gov. Scale D) ni shilingi ngapi kwa sasa? Nataka kuachia tawi Private Sector niende huko lakini sijui kukoje...

==============
July 2014 UPDATE:


Yaani, I kant imajin!!!!!

Mshirazi........naomba nikupe ushauri kuhusu ajira za serikali na sitaki kuzungumzia kipato ila performance yako katika kazi.

Nina rafiki yangu tumemaliza pamoja ADA anafanya kazi serikalini siku mmoja tulikutana na kuzungumza masuala ya kazi nilishangaa sana!

Utaratibu mzima wa nidhamu pamoja na kazi zenyewe si sehemu ya kwenda unless ujitolee sana kufanya kazi la sivyo utakuwa hujifunzi chochote na utakuwa huna challenge mpya we ni kwenda na kurudi siku imepotea.

Jambo zuri ambalo lipo chance ya kuendelea kusoma ni kubwa so fanya maamuzi kutokana na malengo uliyojiwekea.

Mshahara ni mdogo ila marupurupu yakikukalia sawa utaipenda kazi.

Kuhusu scale za mshahara sina idea wenye nazo watupe mwanga please!!

hivi mimi sina aidia na scale za mishahara!halafu ninasali nipate kazi serikalini...lolz!

duh hivi wanaishije...! TGS D ni graduate huyo! Tunatarajia pia alipe deni lake la Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu!

Mbuvu yuko sahihi jamani, TGSD nI 322 ELUFU! hiyo kwako mkuu labda ilikuwa enzi zile.....
Then jambo la kusikitisha vi semina, vikongamanao, vi warsha pinda kavifuta vyoote! Sijui jamaa wanaishije kweli duniani hakuna usawa! wakati kuna watu wanajengewa nyumba moja ya kulala kwa mabilioni na taasisi ya umma mtu mwingine mwenye mahitaji sawa analipwa 322 elufu kabla ya makato! na hapo hajachukua mkopo SACCOS!!!!!....

Usichane resume yako. Badala ya kuomba hiyo kazi, sasa omba ukurugenzi, ukatibu mkuu, ukuu wa wilaya/mkoa. Ukishindwa omba basi hata ubunge manake utaweza kupata na uwaziri halafu mshahara wako pamoja na marupurupu yanaanzia mil 3 hadi karibia 20 kwa mwezi. Sio unaona kunavyolipa serikalini?

Ukishindwa vyote hivyo, hata ukatibu wa ccm wa wilaya? manake nako unaanzia na zaidi ya milioni! Hii nchi si inawenyewe? kama hutaki kuwa miongoni mwao, basi utaishia na hivyo vilaki 2 au 3 vile!

Hii post yako imenikumbusha mbali kweli. "Mtoto wa nyani alipomuuliza mama yake, mpaka wa shamba lao ili asijekula mahindi yasiyokuwa ya kwao. Mama alimjibu, kula tu mwanangu wenyewe watakuja kugawa". Tanzania, wanaendelea kula tu, hadi wenyewe watakapokuja kugawa! maybe in 50 or 100 years to come! who knows/cares? Don't you see them keeping a distance?
 
Back
Top Bottom