Ngawaiya Atangaza Kumvaa Ndesamburo

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
Ngawaiya atangaza kumvaa Ndesamburo
broken-heart.jpg

Daniel Mjema, Moshi

BAADA ya kukaa nje kwa kipindi kimoja, mbunge wa zamani wa Moshi Vijijini, Thomas Ngawaiya sasa anataka kurudi tena bungeni, lakini amechagua njia ambayo itambidi afanye kazi ya ziada; kumngâoa Philemon Ndesamburo jimbo la Moshi Mjini.

Ngawaiya, ambaye alikuwa mbunge wa Moshi Vijijini kwa tiketi ya TLP kwa kipindi kimoja (2000 hadi 2005), atavaana na Ndesamburo wa Chadema kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu iwapo atapitishwa na chama chake kipya cha CCM.

Akitangaza nia yake ya kurudi bungeni, Ngawaiya alisema kuwa ameamua kugombea ubunge wa Moshi Mjini kwa sababu ana hoja za msingi ambazo hazijafanyiwa kazi kwa miaka 15 ambayo jimbo hilo limekuwa chini ya upinzani.

Awali Ngawaiya ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM alikuwa ameonyesha nia ya kuwania Jimbo la Moshi Vijijini linaloshikiliwa na Dk Cyrill Chami, lakini sasa amebadili msimamo huo na kujikita Moshi Mjini.

Hatua hiyo ya Ngawaiya imekuja miezi michache tangu mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM, Anne Kilango Malecela atangaze uamuzi wa kupiga kambi katika jimbo hilo ili kuhakikisha CCM inamng'oa Ndesamburo.

Ngawaiya alitangaza msimamo huo mbele ya wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilayani Moshi Mjini katika kikao chake kilichofanyika juzi.

"Nina hoja ya msingi hapa kwamba katika kipindi chote Ndesamburo hajaweza kutatua tatizo la ajira kwa vijana na wala hawajui wafanye nini; viwanda vimekufa na hakuna anayepigania vifufuliwe," alisema Ngawaiya alipoongea na waandishi wa n habari baadaye jana.

Aliongeza kuwa jimbo la Moshi Mjini halina mwakilishi bali ni mfadhili na kuongeza kuwa anachokifanya Ndesamburo kinaweza kufanywa na mfadhili yoyote, hasa ikizingatiwa kuwa anapata Sh12 milioni za jimbo kwa mwaka.

Ngawaiya alisema japokuwa yeye si mbunge, tayari ameshafanya mazungumzo na Waziri wa Fedha ili kuwashawishi wawekezaji kuanzisha viwanda vipya na kuwanyangâanya wale walioshindwa kuviendeleza.

Mwanasiasa huyo ambaye alikuwa amefuatana na katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoani Kilimanjaro, Godliver Kamala alisema ajira ya wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga, hailipi na imekuwa ni adha kubwa.

"Lakini mimi nitasimamia kuanzishwa kwa viwanda vya kusaga kahawa hapa hapa Moshi ili tuuze kahawa yenu ikiwa imeongezwa thamani kwa sababu kuanzishwa kwa viwanda hivyo kutapanua wigo wa ajira," alisema.

Alipoulizwa ni kwanini ameamua kumkimbia Dk Chami Moshi Vijijini, Ngawaiya alisema lingekuwa ni jambo la ajabu kwenda kupambana na mbunge ambaye yeye alimpigania ashike wadhifa huo mwaka 2005.

Ngawaiya alisema Dk Chami amefanya mambo makubwa ya kimaendeleo katika jimbo hilo hivyo haoni sababu ya msingi ya kumuondoa kwa sasa kwani anakubalika kwa wananchi kutokana na maendeleo aliyosimamia. Hatua hiyo ya Ngawaiya inafanya idadi ya wanachama wa CCM waliojitokeza kuchuana na Ndesamburo kufikia wawili baada ya aliyekuwa mhasibu wa ofisi ya mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Gibson Lyamuya kutangaza nia hiyo.
 
Moshi Mjini

Ngawaiya ana haki kama mtu yeyote yule kuweka nia yake hadharani ya kugombea jimbo hili la moshi mjini.Karibu moshi mjini tutakusikiliza cha msingi ni lazima aelewe atapambana na mpinzani hodari na aliyejidhatiti sawa sawa. Ndesamburo kashafanya mengi na ngawaiya alishakuwa mbunge wa moshi vijijini akiwa chama cha TLP na alipokosa kuwa mjasiri wa kuwa mpinzani sasa hivi anaibukia CCM.Ngawaiya alifanyanini cha msingi moshi vijijini?

Ok ngoja tuone daudi akipambana na goliati.
 
Nenda Ngawaia!!!! Nenda!!!! Nenda safari ya kutoonana tena!!! Moshi si boot testing political constituency.

Tutakusikia Arawa. Utatangazwa sana chalii angu.
Na ukizingatia jinsi unavyopenda vyombo vya habari!!!!!!
Mbona utajitosheleza kwa kuandikwa tu bwashee!!!!!!!
 
Nenda Ngawaia!!!! Nenda!!!! Nenda safari ya kutoonana tena!!! Moshi si boot testing political constituency.

Tutakusikia Arawa. Utatangazwa sana chalii angu.
Na ukizingatia jinsi unavyopenda vyombo vya habari!!!!!!
Mbona utajitosheleza kwa kuandikwa tu bwashee!!!!!!!

Kwanini kakimbia Moshi Vijijini?
 
Kule aende Mzee Mengi tu ili kuimarisha kikosi cha wanaopambana na ufisadi Bungeni.
 
alifanya nini kwa moshi vijijini,ni ukweli kuwa Ndesamburo ni mbunge anayewajali wananchi wake ndo maana inamlazimu kuwafadhili kwa sababu serikali haiwezi fanya anacho fanya,tengeneza uwanja mwingine kwani moshi sio uwanja wa majaribo,watu wa moshi wameamka na huwatambua mafisadi chipukizi
 
alifanya nini kwa moshi vijijini,ni ukweli kuwa Ndesamburo ni mbunge anayewajali wananchi wake ndo maana inamlazimu kuwafadhili kwa sababu serikali haiwezi fanya anacho fanya,tengeneza uwanja mwingine kwani moshi sio uwanja wa majaribo,watu wa moshi wameamka na huwatambua mafisadi chipukizi

Noted.
 
Huyo mzee kafulia anatafuta nitoke vipi. Wakati akiwa upinzani kule mooshi vijijini je ahadi alizotoa kipindi hicho alizitekeleza? Sasa anapotaka kugombea sasa hivi atatuakkishia vipi kuwa hizi ahadi za moshi mjini zitatekelezwa?
 
Mzee Ngawaiya nadhani anatakiwa apewe ushauri nasaha kuwa jimbo la moshi si uwanja wa kufanyia mazoezi ya kisiasa, ikumbukwe kuwa Big Ben alijitahidi kumchomeka shemeji ikashindikana wakati huo Big ben anashikilia nchi, sasa huyu Ngawaiya sijui anataka kutuaminisha nini, suala la kuongea na waziri wa fedha is not a big dili Mzee Ndesa Pesa alishatamka bayana kama sijakosea bungeni kuwa apewe viwanda vya moshi avifufue na kutafuta wawekezaji serikali ikakwaya nadhani kwa ujinga wa kuwa atakayepata sifa ni mzee Ndesa,na hii yote ni kutokana na kuwa na watendaji wa wajinga. Ushauri wangu kwa Ngawaiya yeye aendelee na kazi ya taasisi yake na sijui itakuwa imeshaleta mafanikio gani toka imeanzishwa, aache watu wenye mawazo mapana waendeshe shughuli za Moshi mjini si kujikomba komba.
 
Mzee Ngawaiya nadhani anatakiwa apewe ushauri nasaha kuwa jimbo la moshi si uwanja wa kufanyia mazoezi ya kisiasa,ikumbukwe kuwa Big Ben alijitahidi kumchomeka shemeji ikashindikana wakati huo Big ben anashikilia nchi,sasa huyu Ngawaiya sijui anataka kutuaminisha nini,suala la kuongea na waziri wa fedha is not a big dili Mzee Ndesa Pesa alishatamka bayana kama sijakosea bungeni kuwa apewe viwanda vya moshi avifufue na kutafuta wawekezaji serikali ikakwaya nadhani kwa ujinga wa kuwa atakayepata sifa ni mzee Ndesa,na hii yote ni kutokana na kuwa na watendaji wa wajinga. Ushauri wangu kwa Ngawaiya yeye aendelee na kazi ya taasisi yake na sijui itakuwa imeshaleta mafanikio gani toka imeanzishwa, aache watu wenye mawazo mapana waendeshe shughuli za moshi mjini si kujikomba komba.

Wonderfully Analysis!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom