Ngawaiya amzodoa Ndesamburo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngawaiya amzodoa Ndesamburo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Habarindiyohiyo, Jan 19, 2009.

 1. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ngawaiya: Simuombi radhi Ndesamburo
  Na Mwandishi Wetu

  MWENYEKITI wa Taasisi ya Utawala Bora na Maendeleo (Cegodeta), Thomas Ngawaiya amesema hayuko tayari kumuomba radhi na kumlipa fidia ya Sh120 milioni, Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo, anayedai kukashifiwa.


  Msimamo huo wa Ngawaiya, ambaye amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini kwa tiketi ya TLP kabla ya kujiunga na CCM, umekuja wiki moja tu baada ya Ndesemburo kutoa siku 14 kwa mwenyekiti huyo kuomba radhi na kumlipa fidia ya Sh120 milioni kwa madai kuwa alimkashifu na kwamba asipofanya hivyo atafikishwa mahakamani.


  Ndesamburo anadai kuwa kupitia gazeti la Daily News la Desemba mwaka jana, Ngawaiya alimkashifu kuwa alitumia fedha za ruzuku za chama chake kununulia helikopta binafsi.


  Lakini katika taarifa yake ya jana kwa vyombo vya habari, Ngawaiya alisema hayuko tayari kutimiza matakwa ya mbunge huyo kwa maelezo kuwa hajawahi kumkashifu kama anavyodai.


  "Nimepokea barua kutoka kwa Wakili G.P. Sandi wa Moshi, (ambayo pia imenakiliwa kwenye gazeti la Mwananchi la Januari 13 mwaka huu) inayonitaka nimuombe radhi mteja wake, Mh. Philemon Ndesamburo, ambaye ni Mbunge wa Moshi Mjini ndani ya siku 14, kupitia gazeti la Daily News na pia nimlipe fidia ya Sh 120,000,000 kwa madai kuwa nimetoa matamshi ya kumkashifu kupitia gazeti la Daily News la tarehe 30/1202008," anasema Ngawaiya katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.


  "Mimi sina sababu ya kuomumba radhi Mh. Ndesamburo wala kumlipa fidia anayotaka ya Sh 120,000,000 kwa sababu sijawahi kumkashifu mbunge huyo wa Moshi Mjini ambaye pia ni mbunge wangu kwa kuwa mimi pia ni mkazi wa Moshi Mjini."


  Katika taarifa hiyo, Ngawaiya anasema ni kweli kwamba Desemba 29 mwaka jana, aliitisha mkutano wa waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kutoa salamu za mwaka mpya za taasisi yake kwa wananchi.


  Alisema pamoja na mambo mengine, katika risala yake ya maandishi, alizungumzia utawala bora na maendeleo na kuiomba serikali iongeze nguvu na kudhibiti wizi na ubadhirifu wa fedha za umma, katika vyama vya ushirika na vyama vya siasa.


  Kwa mujibu wa maelezo yake, rai hiyo inatokana na madai ya kuwepo kwa vitendo vya wizi na ubadhirifu wa fedha za ruzuku, inayotolewa na serikali kwa vyama hivyo, fedha ambazo alisema zinatokana na kodi za wananchi.


  Ngawaiya, ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM mkoani Kilimanjaro, alisema katika salaam hizo pia aliiomba serikali kuzifanyia marekebisho sheria za vyama vya siasa na vyama vya ushirika.


  "Niliiomba serikali ipitishe sheria, ili vyama vya ushirika na vyama vya siasa vikaguliwe na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (Cag), kwa sasa vyama hivyo hukaguliwa na wakaguzi binafsi, jambo ambalo limelalamikiwa na wananchi wengi kwamba linasababisha wizi na ubadhirifu wa fedha za ruzuku inayotolewa na serikali na kufuja michango na miradi ya wanaushirika," alisema Ngawaiya katika taarifa.


  Alisema katika salaam hizo za Mwaka Mpya, hakuna sehemu yoyote ambayo amemtaja Ndesamburo kama mtu binafsi na kwamba kwa msingi huo, hawezi kumuomba radhi na kumlipa fidia.


  "Nilipokuwa najibu swali la mwandishi wa Daily News nilisema kwamba kuna tuhuma kutoka kwa wananchi kwamba viongozi wao wanagawana ruzuku za vyama na kununua majumba na helikopta.


  Hivyo niliomba tuhuma hizo zichunguzwe na mahesababu yakaguliwe upya na mkaguzi mkuu wa serikali ili ukweli ujulikane. Dhana ya Cegodeta haimlengi mtu binafsi na wala sheria inayomuomba siyo kwa ajili ya kumkomoa mtu binafsi, bali ni kwa manufaa ya umma," alisema.


  Ngawaiya alisema anahisi kuwa matakwa ya Ndesamburo dhidi yake yanasukumwa na chuki binafsi baada ya kusikia kuwa baadhi ya wananchi wanamtaka agombee ubunge wa jimbo la Moshi katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010.


  "…inawezekana kwamba hiyo ni mojawapo kati ya mbinu anazofanya ili kunikwamisha. Namtaarifu kuwa sijafanya maamuzi bado kama nitagombea ubunge mwaka 2010 au la.


  Hoja ya kutaja majumba na helikopta kwenye taarifa yangu haikummaanisha mtu, kwani si yeye pekee mwenye nyumba na helikopta nchini mwetu. Naamini wakaguzi wa serikali wakatakapokagua upya mahesabu kama Cegodeta ilivyoomba, ukweli ama kuna ubadhirifu au hapana, utajulikana," alisisitiza Ngawaiya.


  Kiongozi huyo wa Cegodeta alisema: "Sitamuomba radhi (Ndesamburo) wala kumlipa fidia na ana uhuru na haki ya kwenda mahakamani kama akipenda."
   
 2. S

  Sheikh Member

  #2
  Jan 19, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lazima. Maana yeye lazima ashukuru kwa kupewa tenda za CCM kuuza mbolea kanda yote ya kaskazini sasa uliona wapi mkono mtupu ukarambwa au mtu kuuma mkono wa mtu anayemlisha.

  Aishukuru CCM maana kama sio CCM alikuwa keshafilisika. Kisha wajua huyu bwana kawasaidia watu wasiomhusu lakini ndugu zake matambara matupu, wanatembelea kanda mbili huku kaoa wake wawili......

  Nenda kwa Ndesamburo hakuna ndugu yake hata mmoja mwenye njaa wee, bwana watu wengine waone kwa nje tu, ndani wameoza kapsaaaaa!
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Jan 19, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Haki hupatikana mahakamani sio vijiweni au kwenye klabu za pombe
   
Loading...