Ngassa kutambulishwa leo,aliahidiwa 3m kila goli!!!!!

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
7,113
930
Ndugu wanajangwani lile jembe la Yanga Mrisho Halfan Ngassa leo atatambulishwa kwa waandishi wa habari.Mshahara wake utakua $2000.

Wakati huo huo katika kile kilichoonyesha kwa anamapenzi kutoka ndani ya moyo wake na timu ya Yanga juzi alikataa kuifunga timu yake hiyo ya mitaa ya twiga/jangwani ingawa aliahidiwa kulipwa million3 kwa kila goli atakalolifunga.

More updates to come.................
 
Karibu sana Jembe letu, naamini utakua msaada mkubwa ktk club bingwa Africa.
 
Ndugu wanajangwani lile jembe la Yanga Mrisho Halfan Ngassa leo atatambulishwa kwa waandishi wa habari.Mshahara wake utakua $2000.

Wakati huo huo katika kile kilichoonyesha kwa anamapenzi kutoka ndani ya moyo wake na timu ya Yanga juzi alikataa kuifunga timu yake hiyo ya mitaa ya twiga/jangwani ingawa aliahidiwa kulipwa million3 kwa kila goli atakalolifunga.

More updates to come.................

Mrisho Ngassa akiibusu jezi ya Yanga baada ya kutambulishwa rasmi kurejea katika klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili asubuhi ya leo, makao ya klabu hiyo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.

Katibu wa Yanga, Lawrence Mwalusako akimkabidhi Ngassa jezi ya Yanga leo
 
Ahsante sana mkuu kwa mipicha!
Jf ni zaidi ya habari!
 
Yeah mkuu kijana tayari kesha mwaga wino, msimbazi walie tu

Ngassa alinikera sana alivyomdanganya refa kwa ile penati...hakuna penati ya kirahisi vile!!!
Halafu alicheza hovyoooo!!!
 
Ngassa alinikera sana alivyomdanganya refa kwa ile penati...hakuna penati ya kirahisi vile!!!
Halafu alicheza hovyoooo!!!

mpwa watu8 ile mikono Canavaro ilimponza alionekana amemkumbatia
 
Last edited by a moderator:
mkuu mandieta, sina uhakika kama ninchosoma kiko sawa hapo kwenye red, au ninaota! Je, kwa gear hii mtawaza kuwatoa hata Wacomoro kwenye klabu bingwa? By the way, Muyi Twuite yupo!? Kweli tanzania ni nchi ya maajabu ninakubali
Ndugu wanajangwani lile jembe la Yanga Mrisho Halfan Ngassa leo atatambulishwa kwa waandishi wa habari.Mshahara wake utakua $2000.

Wakati huo huo katika kile kilichoonyesha kwa anamapenzi kutoka ndani ya moyo wake na timu ya Yanga juzi alikataa kuifunga timu yake hiyo ya mitaa ya twiga/jangwani ingawa aliahidiwa kulipwa million3 kwa kila goli atakalolifunga.
 
mkuu mandieta, sina uhakika kama ninchosoma kiko sawa hapo kwenye red, au ninaota! Je, kwa gear hii mtawaza kuwatoa hata Wacomoro kwenye klabu bingwa? By the way, Muyi Twuite yupo!? Kweli tanzania ni nchi ya maajabu ninakubali
Ni sahihi mkuu!
Ata baadhi ya vyombo vya habari vimeriport juu ya hili.
 
mmmh....

huyu mtoto nina wasiwasi na washauri wake..

nadhan wanaamin mpira n simba na yanga 2... hafikiri hata kutoka nje ya nchi
 
Ahsante sana mkuu kwa mipicha!
Jf ni zaidi ya habari!

Huyu mtoto malaya sana...

simpimii kijana atavyokuwa atakavyokuwa anagawa maumivu msimbazi

Welcome back JEMBE

mmmh....

huyu mtoto nina wasiwasi na washauri wake..

nadhan wanaamin mpira n simba na yanga 2... hafikiri hata kutoka nje ya nchi

ngs.jpg

Mrisho Ngasa akiongea na waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu ya Yanga baada y akutambulishwa rasmi leo

Katibu Mkuu wa klabu ya Young Africans Lawrence Lawrence Mwalusako leo amemtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari mchezaji Mrisho Ngasa ambaye amerejea katika klabu yake ya zamani kufuatia kumalizika kwa mkataba wake wa miaka miatatu (3) dhidi ya timu ya Azam FC.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu Mwalusako amesema Ngasa amerejea katika timu yake, alikuwa mchezaji wetu kwa muda mrefu kabla ya kuhamia katika timu ya Azam FC ambako alitumikia mkataba wa miaka 3 uliomalizika mwisho mwa msimu huu.
Naye mwenyekiti wa mashindano wa klabu ya Yanga Abdallah Bin Kleb amesema anashukuru kwa Ngasa kuamua kurudi nyumbani, kwani amekuwa mchezaji anayejitolea kwa moyo wake wote katika timu zake zote alizokuwa akichezea hali iliyompelekea kuendelea kuwa katika kiwango cha hali ya juu.
Kwa kweli mimi binafsi nimefurahi kijana kurejea nyumbani, amerejea katika timu inayomjali, inamsikiliza alisema Bin Kleb huku akimalizia kwa kusema kuwa Ngasa ataitumikia Yanga kwa mkataba wa miaka 2.
Aidha Ngasa mwenyewe amewashakuru wapenzi, washabiki na wanachama wa klabu ya Yanga kuwa naye kwa nyakati zote, nilipohamia Azam walikua wakishangilia, nilipohamia Simba pia walikuwa wakinipa moyo na kunishangilia pia.
Nimeamua kurudi katika timu yanga ya zamani sababu ndio sehemu pekee wanaponisikiliza na kunithamini, timu niliyotoka pamoja na kucheza kwa moyo wangu wote bado viongozi wake hawakua na imani na mimi hicho ndo kilichonipelekea kurudi katika timu yangu ya Yanga.
Ngsa anakua mchezaji wa kwanza kusajiliwa na klabu ya Yanga kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi kitachoitumikia Yanga katika msimu ujao.
DAIMA MBELE NYUMA MWIKO (DMNM)
EVER FORWARD BACKWARD NEVER (EFBN)

ngsa.jpg

Mrisho Ngasa akikabidhiwa jezi ya klabu ya Yanga na katibu mkuu Lawrence Mwalusako
 
Back
Top Bottom