BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,011
Date::1/19/2009
WAZIRI wa zamani wa Mipango, Uchumi na Uwekezaji katika utawala wa awamu ya tatu, Dk Juma Ngasongwa amesema hatua ya serikali kuwafikisha mahakamani viongozi waandamizi wa serikali, wakiwemo mawaziri kwa makosa waliyofanya wakiwa madarakani, inatia hofu.
Ngasongwa alitoa kauli hiyo alipozungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake jijini Dar es Salam jana.
Dk Ngasongwa alisema: "Ukimshtaki mtu kwa maamuzi aliyoyafanya akiwa madarakani, ukweli inatia mashaka. Inatakiwa kuwa makini kidogo katika kulitazama suala hilo. Pale serikalini kuna mambo mtu anaweza kuamua si kwa sababu alifikiria kufanya ufisadi. "
Alifafanua kuwa kwa watendaji wa serikali, inawezekana mtu alifanya maamuzi kwa sababu alilazimika kufanya hivyo kwa sababu zilizopo wakati huo na si kwa kufikiria kufanya ufisadi.
Aliongeza kuwa, kama binadamu baadaye anaweza kugundua maamuzi yake hayo ya awali kuwa hayakuwa sahihi na kuhitaji kusahihisha, lakini hushindikana kwa kuwa tayari anakuwa nje ya nafasi hizo.
"Pengine angepata nafasi, angesahihisha," alisema waziri huyo wa zamani. Dk Ngasongwa, ambaye ni mbunge wa Ulanga Magharibi kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), alisisitiza kuwa ni muhimu suala hilo likaangaliwa vizuri na kwa umakini zaidi. Hata hivyo, alisema kuwa watu ambao wanatuhumiwa kwa ufisadi wote wafikishwe mahakamani, washtakiwe na mahakama iamue kuwahukumu kwa ushahidi na iwapo hawataridhika wakate rufaa.
"Kama mtu kweli alifanya ufisadi, basi hilo sawa. Watu ambao walifanya ufisadi kama ule wa EPA hilo ni dhahiri, wanastahili washtakiwe na mahakama siku zote tunaiheshimu, iamue lazima mmoja atusaidie, kama hataridhika atakata rufaa. "Lakini wale watu wa EPA nadhani ni muhimu wakashtakiwa. Washtakiwe kweli, kusiwe na danganya toto. Washtakiwe na utaratibu uende kwa makini... watakaonekana wana hatia, wahukumiwe kwa mujibu wa sheria."
Vita ya ufisadi hadi sasa imechukua sura tatu kuu; watu wanaotuhumiwa kuiba jumla ya Sh133 bilioni katika Akaunti ya Malipo ya Malimbikizo ya Madeni ya Nje (EPA), mawaziri wanaotuhumiwa kutumia vibaya ofisi zao na kutumia uongo ili kupata tenda ya serikali ya ufuaji umeme wa dharura.
Watu 21 wameshafikishwa mbele ya sheria kujibu tuhuma za wizi, kula njama za kuiba fedha za EPA, wakati mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona, pamoja na katibu mkuu wa wizara, Gray Mgonja wakifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutumia vibaya ofisi na kuisababishia serikali hasara.
Mtu mmoja ameshtakiwa kwa tuhuma za kughushi nyaraka ili aifanikishe Kampuni ya Richmond kupata zabuni ya kufua umeme wa dharura.
Ngasongwa: Inatia hofu mawaziri kushtakiwa
Exuper Kachenje
Mwananchi