Ngasa alipofushwa na ujinga ule ule wa miaka yote ya wachezaji wa Kitanzania

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,357
11,503
Huu ni ujinga wa wachezaji wengi wa kitanzania ambao bado hawajafahamu kuwa mpira ni kazi kama kazi nyingne yoyote ile. hawa huwa wanaweka mapenz ya team zao mbele wanasahau siku nazo hazigandi. Ngassa alionesha mapenz makubwa sana kwa team ya Yanga jambo ambalo sisemi kuwa ni baya. akasahau kuwa siku zinaenda na yanga si baba yake au team ya baba yake. tunakumbuka alipokuwa azam halafu akaamua kuvaa jezi ya yanga kuonesha kuwa ana mapenz na yanga. akaenda simba nako akakaa na kutaka kurudi yanga akisema ndo nyumban kwake.

Ikumbukwe pia kuwa wakati akiwa katika mkataba wa mkopo baina ya simba na Azam, Simba walifanya utaratibu wa kumumsajili Ngasa, usanii ni mnamo tarehe December 5, 2012 vyombo vya habari viliripoti Azam yamuuza Ngasa kwa Elmereikh kwa $ 75,000 sawa na Milioni 120 na ngasa aligoma kwenda huko akidai hawezi kuuzwa labda kwa sababu aliona kuwa alikuwa kwenye ubora wake na pengne kutaka kushindana na team hiyo. inashangaza leo ni ngasa huyu huyu inasemekana ametoroka Yanga kwenda kufanya majaribio afrika kusin. kwa mapenz aliypkuwa nayo yanga hatukudhan kama atafika hapo. hili ni tofaut na wachezaji wanaoelewa mpira ni kazi. tulimwona emmanuel okwi ambaye alilelewa na simba na inasemekana ni mpenzi wa simba. lakini kwa kujali maslahi hilo hakuliangalia na haikuwa ajabu alipowafunga simba mwaka katika moja ya mech za simba na yanga.

alifaham au anafaham mpira ni kazi na mwajiri anataka ufanye jambo lililomsababisha akuajili. siku zote ngasa aliamini kuwa yeye atakuwa yanga na kwa kuwa alionesha ana mapenz na yanga basi ana namba ya kudumu. bila kujua kila kocha ana mahitaji yake na mfumo wake, hivyo pia unaweza usipangwe kwa kuwa huendani na mfumo wa kocha huyo.

sasa ngasa amekimbilia afrika kusini kama inavyosemekana. tusuiri kuangalia sinema nyingne kwa upande wa wachezaji wa Tanzania na vilabu vyetu.

huu ujinga msiwe nao wachezaji ama sivyo siku zote mtabaki kujilaumu kuwa hamfanikiwi .
 
Back
Top Bottom