Ngara: Kwanini afisa elimu unawang'ang'ania walimu wakuu wa certificate

Duh walimu bwana!!! So what? Mwenye certificate siyo mwalimu? Au unataka kwakuwa MTU kafika na kidigrii au kidiploma ndiye apewe u HT, Mchawi was mwalimu ataendelea kuwa mwalimu.
 
Mtu hapimwi kwa certificate wala shahada bali ni kwa namna gani anaweza kumudu majukumu ya kazi katika mjongeo chanya
 
Kwanini afisa elimu unawang'ang'ania walimu wakuu wa certificate
Elimu ni uwezo siyo vyeti. Hao wanaweza kuwa bora zaid kuliko Diploma na Digrii wengi tu. Siku hizi watu wana miliki madiploma na madigrii lakini ukija kwenye performance ni zero kabisa!
 
Hao wazee wenye certificate wako vizuri sana, dogo jifunze kwao utapata maarifa mengi! Uongozi si lazima uwe na shahada!
Huyu jamaa ina maana hajasikia kuna watu ni madokta na maprofesa lakini wapumbavu?
 
Vipi, ukipelekwa Murusagamba; Kaburanzwiri, utamudu majukumu: nikupigie pande?
 
Kwanini afisa elimu unawang'ang'ania walimu wakuu wa certificate
Kazi ipate mtu sio mtu apate kazi, miaka ya hivi karibuni wanafunzi wengi wanaomaliza kidato cha sita wanachagua course ya ualimu ngazi ya shahada ili wapate mkopo hiyo ni kwa mujibu wa imani zao lakini sio kwamba wanapenda kuwa walimu ni tofauti na zamani.
Kuna shule fulani nilibahatika kusoma miaka 20 iliyopita mwalimu mkuu alikuwa wa certificate aliweza kuimudu vyema shule katika kipindi chake chote cha uongozi, baadae walijitokeza wadau wataka mabadiliko wakaomba wabadilishiwe mwalimu mkuu aletwe mwenye shahada ndani ya wiki moja shule ilimshinda ilibidi kurudishwa yule wa certificate aendelee kuiongoza
 
Back
Top Bottom