Ngara, Kagera: Mkutano wa hadhara wa Rais Magufuli na Rais Nkurunziza wa Burundi

Napendekeza Rwanda na burundi zibadilishe katiba na zipelleke miswada bungeni na waitishe kura za maoni za kuomba nchi hizo ziungane na tanzania kuwa nchi moja tuwe na nchi moja ambayo itajulikana kama Tanzarwabu ikijumuisha tanganyika zanzibar rwanda na burundi.Nina uhakika kura za.maoni zikipigwa wananchi wataridhia bila shida.Rwanda na Burundi ni kama.watanzania tu na.Tanzania inaninfluence kubwa kwenye nchi.hizo kuliko kwingine.pia faida za kiuchumi na kisiasa ni kubwa mno
Akili za makinikia
 
Napendekeza Rwanda na burundi zibadilishe katiba na zipelleke miswada bungeni na waitishe kura za maoni za kuomba nchi hizo ziungane na tanzania kuwa nchi moja tuwe na nchi moja ambayo itajulikana kama Tanzarwabu ikijumuisha tanganyika zanzibar rwanda na burundi.Nina uhakika kura za.maoni zikipigwa wananchi wataridhia bila shida.Rwanda na Burundi ni kama.watanzania tu na.Tanzania inaninfluence kubwa kwenye nchi.hizo kuliko kwingine.pia faida za kiuchumi na kisiasa ni kubwa mno

Halafu Kagame, Magu na Piere wataongoza wapi? Au unataka vita vianze upya?
 
Kusema ukweli tumetunukiwa Rais ambaye kwa kiasi kikubwa ana mtazamo wa kuijenga nchi yetu. Ila kama binadamu yeyote yule, vile vile ana mapungufu yake, hasa kwenye uwasilishaji. Kuna maamuzi na hatua huwa anachukua, na unaona umuhimu wake na kujiuliza "Kwa nini halikuweza kutendeka huko nyuma?". Japo sikubaliani na mitazamo yake yote au maamuzi yake mengine, ila kiukweli kwenye swala la miundombinu kuna mabadiliko mazuri yanaonekanana, na hata kwenye kuwapa wananchi vipaumbele. Changamoto bado ni nyingi, kuna mengine tunabomoa badala ya kujenga (kwa mtazamo wangu).

Laiti kama tungekuwa na 'strategists' wazuri (labda tayari tunao ila bado nina 'upofu' wa kufahamu hilo) wakuhakikisha sera, kanuni, sheria, utendaji, matumizi, utunzaji, nk. unazingatiwa sanjari na maono ya nchi, na kushabihiana katika kila sekta na uwanda; tena kwa kushirikisha wananchi na wadau.
 
Wadau,Umofia kwenu,

Hafla inafanyika viwanja vya Posta ya zamani kwenye wilaya Ngara inayopakana na Rwanda na Burundi.

Asanteni

======

NGARA: Rais Magufuli amewasili katika uwanja wa mpira wa Lemela Wilaya ya Ngara, Kagera ambapo atampokea Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.

NGARA: Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amewasili uwanja wa mpira wa Lemela, Ngara, Kagera na kupokewa na Rais Magufuli asubuhi hii.

Rais Magufuli amesema mazungumzo yake na Rais Nkurunziza yamehusu ushirikiano wa biashara na ujenzi wa reli kutoka Dar, Rwanda na Burundi.

Rais Dakta JOHN POMBE MAGUFULI amekutana na Rais PIERRE NKURUNZINZA wa Burundi katika uwanja wa mpira wa Lemela Wilayani Ngara Mkoani Kagera.

Baada ya kuwasili katika uwanja huo Rais NKURUNZINZA amepata mapokezi ya kijeshi ya mkuu wa nchi kwa kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ na kisha kuangalia vikundi vya ngoma.

Akisalimia wananchi Rais NKURUNZINZA amesema ushirikiano mzuri kati ya nchi yake na Tanzania unaimarishwa kuhakikisha wananchi wanaendesha shughuli zao kwa amani bila hofu ya usalama wao.

Mchana huu Rais MAGUFULI atazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara Kwenye Viwanja vya Posta ya Zamani Mjini Ngara.

======

Sasa ni Hotuba ya rais katika Viwanja vya Posta ya Zamani Mjini Ngara. Fuatilia hapa chini.

=> Niwaombe na nitoe wito kwa ndugu zangu wa Burundi 150,000, waanze kurudi kwao. Siwafukuzi ila warudi nyumbani.

=> Tunajenga reli; mazungumzo yanaendelea na kila kitu kikikamilika tutaanza ujenzi wa reli

=> Tumesema hizi ushuru ndogo ndogo kwa wakulima tumefuta. Ukisafirisha mzigo wako usiozidi tani moja hutalipa ushuru wowote.

=> Tumefuta kodi saba kwa wananchi wanyonge. Nazungumza hivi ili watendaji wasikie.

=> Tukikuta mtu ametozwa kodi kwa mzigo unaopungua tani moja huyo mkurugenzi na DC watakiona cha mtemakuni.

=> Tumeamua kutoa elimu bure na hii imeongeza hata kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi

=> Tumetenga shilingi bilioni 483 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi watakaofaulu kwenda kusoma elimu ya juu.
Tumeanza kuchukua hatua kwa mafisadi.

=> Waliokuwa wananufaika na mishahara hewa, vyeti feki hewa, kaya hewa na pembejeo hewa na wawekezaji hewa tunalala na nao mbele.

=> Tumetoa vifaa vya maabara kwa shule 1900 na tumevigawa Tanzania nzima

=> Tumeamua kuagiza madawa moja kwa moja nje ili kupunguza gharama ya dawa.

* Mmeniambia kuhusu maji, lakini najua mtu wa maji yuko hapa.

=> Mtu wa maji: Tulinunua pampu mpya na imeanza kufanyakazi tangu tarehe 15/08. Tuna mpango wa kujenga tenki la maji na mota ya maji.

=> Rais Magufuli: Maagizo kwa mkurugenzi wa H/Mashauri: Hizo milioni 200 anza kuziweka kwenye maji kwa ajili ya wananchi badala ya kuwapelekea wanajeshi.

=> Naomba hili mniachie, hili la maji nikifika Dar tutakaa na waziri wa maji tuangalie namna ya kufanya.

=> Na mimi nitaleta milioni 13 za kujenga hiyo moter na ole wao iungue na wao wataungua.

=> Tatizo la Ngara ni mgawanyo wa Bushubi na Bughufi. Niwaombe ndugu zangu wa Ngara na Mbunge; hakikisheni matatizo haya yanaisha, yanatucheleweshea Maendeleo

=> Tumetenga fedha kwa ajili kujenga barabara 92km kutoka Rulenge hadi Nyakahura.

=> Leo najua hamlizungumzii la umeme, ninafahamu umeme haujafika baadhi ya maeneo.Ila REA awamu ya tatu utafika karibu kila sehemu. Ninyi tunachowaomba ni kufanya kazi.

=> Leo nimekuja na mgeni wangu Nkuruzinza na kikubwa ni kuwashukuru. Napenda kuwahakikishia mimi na serikali yangu tushikamane.
Dunia ya leo ni biashara,

=> Kwa haya machache naomba niwashukuru, sijawahi kuona makaribisho mazuri namna hii.

+> Rais anauliza hadhara: Hayo mabango ni ya nini? Bango limeandikwa; "Sisi hapa Ngara tuna upungufu wa ardhi, tunaomba mchango wako vijana tupate ardhi tufanyekazi kama ilivyo kaulimbiu yako ya hapa kazi tuu. Tunaomba tupewe maeneo Kasulu".

=> Majibu(Rais Magufuli): Mh mkuu wa mkoa chukua namba yake na atawakilisha wote wanaohitaji ardhi. Hakikisha wanapata ardhi.

Nawashukuru wananchi, waandishi wa Habari na wanakwaya
Asanteni sana ndugu zangu wa Ngara, Mungu awabariki sana.




Rais Magufuli amhakikishia Rais wa Burundi ushirikiano wa kutosha na amemuahidi kuendelea kushirikiana na Burundi katika kuimarisha maisha ya wananchi wa nchi zote mbili na kuimarisha biashara.

Sent using Jamii Forums mobile app

MAfashist wanatakiana heri ya uwongo!! time is coming! Kwa hiyo amejipambanua na aina ya marafiki!! tujianda kupambana atakapong'ang'ania ikulu 2020!!!
 
Wengine sijui vyanzo vyenu vya habari huwa ni vya wapi

Sijawahi sikia akikutana na marais wa nchi kam,SA,Nigeria nk

97b1955c299fcddf75ccfba04050d82f.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom