NFRI yaja na Mizani ya Kidijitali kupima mazao, kuondoa wasiwasi wa vipo, kuongeza ufanisi wa kutunza kumbukumbu

informer 06

Member
May 11, 2024
44
26
Wakala wa Uhifadhi wa Chakula Nchini (NFRA) ,umeanza rasmi kutumia mfumo wa kidijitali katika kupima mazao ya nafaka, hatua ambayo imeelezwa kuwa itakuwa na tija kwa pande zote mbili ikiwemo wakulima kuondoa wasiwasi wa vipimo pale wanapouza mazao yao kwenye mamlaka hiyo.

Hatua hiyo imeelezwa na Mtendaji Mkuu wa NFRI, Dkt.Andrew Komba ambaye katika maonesho ya wakulima na wafugaji, Wavuvi viwanja vya Nane nane Nzuguni jijini Dodoma yaliyoanza Agosti Mosi na kufikia kilele chake Agosti 8, 2024.
View attachment 3065281
Mtendaji Mkuu wa NFRI, Dkt.Andrew Komba

Ambapo amesema utaratibu huo unalenga kumuwezesha Mkulima kuwa na uhakika katika vipimo anapouza mazao yake NFRA, jambo ambalo amedai kuwa ni hatua yenye tija.

"Wakulima wameipokea mizani hii vizuri wakiamini kwamba inawawezesha kupata kiwango sahihi wanachotuuzia na sisi kwetu inatupa kumbukumbu sahihi kwa sababu inaingiza taarifa katika mfumo ambao unatumika katika suala zima la kuhifadhi ."amesema Dkt.Komba

Aidha amesema ,Wakala huo una jukumu la kuhakikisha nchi inakuwa na usalama wa chakula .

Ambapo Dkt.Komba amebainisha wazi kuwa ili kulitekeleza jukumu hilo, NFRA wamekuwa wakinunua na kukusanya chakula na kuhifadhi vizuri kwa utaratibu wa kuhakikisha afya na usalama wa mlaji.

"Kwa ili kuhakikisha chakula kinakuwa salama wakati wote, tunatumia maghala na vihenge katika kuhifadhi chakula,lakini pia tunawafundisha wakulima kuhifadhi chakula wanacholima katika hali ya usalama badala ya kuhifadhi kizamani."amesema Dkt.Komba

Amesema chakula wanachohifadhi kinalenga kuisaidia jamii pale panapotokea uhaba wa chakula na hivyo kutumia akiba hiyo kukidhi mahitaji.

View attachment 3065284
View attachment 3065282
 
Kazii iendelee ,japo Kuna wahunii wa chache Bado watacheza na mfumooo Ili wanufaike wao tu..
 
Back
Top Bottom