Ney wa Mitego atoboa na hit song yake kwenye wakati mgumu wa kiki za kisiasa (Free Nation)

2hery

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,700
4,616
Kwa wadau wa mziki huyu Ney mnamchukuliaje? Sikiliza muziki wake mpya



Verse 1:
Unachokipanda leo ndicho
utachovuna kesho.
Imeandikwa Mwanaume kula kwa
jasho.
Najiuliza hivi ni nani kaiona
kesho.
Chapa mwendo na ukilala hauna
chako.
Hivi uhuru wa kuongea kwenye hii
nchi bado upo?.
Usije kuongea vitu kesho ukajikuta
sentro.

Chorus:
Kuna viongozi wavuta bangi?
"wapo "
Maana wana maamuzi ya kise....
"wapo"
Kuna walio mmiss Jakaya? "wapo"
Walio choka kuisoma namba?
"wapo"
Kuna walio poteza malinda?
"wapo"
Kuna wasanii mateja? "wapo"
Kuna mademu wanasagana?
"wapo"
Kuna vidume wanalelewa? "wapo"
Kuna wasanii wanarogana? "wapo"

Verse 2
Kuna Radio na Tv, naona
zimeshapoteza CV.
Hakuna uhuru wa habari, wala
taarifa ya habari.
Wanapindisha pindisha tu
kuiogopa serikali.
Siamini nchi inaendeshwa na kiki.
Siasa inafunika mziki.
Viongozi wanashindana kukiki.
Wanagombea front page, wauze
kwenye gazeti.
Nasikia kuna viongozi wamefoji
vyeti.

Verse 3
Kiongozi mwenye busara
anapokea ushauri.
Anapokea mawazo,haweki mbele
kiburi.

Hey! Samahani mheshimiwa, hivi
unamjua BASHITE?.
hili ni jipu jipya toka koromije.
Limesha iva na usaa,
limeshatunga.
Na kukabidhi sindano ya
kulidunga.
Daktari haogopi ukubwa wa
kidonda.

We_si Dr wa majipu, tumbua
hakuna kuvunga.
Kuvamia ofisi za watu kumbe nayo
ni kazi.
Hakuna noma wanangu pigeni
kazi.
Boda boda kazi, bajaji Kazi.
Eti! Vipi? Kukaba nayo kazi?.
Refa ni wao piga manati.
Vita ya Masai na mmang'ati.
Biashara ya ngono na Super
shafti.

Pumzi imekata nashika shati...
Hahahahahaha! Wewe mtu gani
sasa......
Hutaki kushauriwa, hutaki
kukosolewa......
Umerongwa wewe,........
unajiona ndugu yake na Yesu
ee....
Oya! Wanangu eeeh! Round hii
mtanyooka haki ya Mungu.
Naona kichaa kapewa Rungu..
MWISHO:
 

Attachments

  • tmp_14965--1581776042.mp3
    8.3 MB · Views: 155
Ney wa mitego(The true boy) katoa single ambayo ni Kali na haijawahi kutokea. Song hii imeikosoa waziwazi serikali ya Magufuli bila woga wowote ule. Kwa song hii inamfanya msanii huyu kuweka record ya kipekee kabisa ambapo katika kipindi ambacho nchini Kuna issue hot inayoendelea hasa hasa issues za mkuu wa mkoa wa Dar ndugu Bashite. Pakua song ya mkali huyo wa hiphop.
 
Ney wa mitego(The true boy) katoa single ambayo ni Kali na haijawahi kutokea. Song hii imeikosoa waziwazi serikali ya Magufuli bila woga wowote ule. Kwa song hii inamfanya msanii huyu kuweka record ya kipekee kabisa ambapo katika kipindi ambacho nchini Kuna issue hot inayoendelea hasa hasa issues za mkuu wa mkoa wa Dar ndugu Bashite. Pakua song ya mkali huyo wa hiphop.
Mkuu hiyo nyimbo Basata watashughulika nae. Ni suala la muda tu..
 
Back
Top Bottom