Ney wa Mitego aanza mchakato wa kujiondoa BASATA, asema atasambaza muziki wake Mitaani

1. Ni wazi BASATA hawajui nini maana ya sanaa, hasa muziki hili wamelionyesha wazi kabisa kwa kitendo walichomfanyia kijana trueboy (Nay).

2. BASATA waache ubinafsi yaani wanajifikiria wao na faida wanayoipata wao bila kujali kile wanachokifanya na madhara yanayotokea kwa wahusika wanaowanyonya na kuwakandamiza.

3. BASATA ifanye kazi bila kuegemea upande wowote. Waache kujipendekeza kutaka sifa.

5. Muziki ni sanaa, na sanaa ni UBUNIFU. BASATA watu mnakaa hakuna aliyewahi buni chochote wala kufanya ubunifu wowote kisha mtu huyu anakuja msimamia MBUNIFU na mwenye kipaji cha ubunifu katika kuwasilisha meseji kwa jamii kwa nia njema, KWAKUWA hamtambui nini maana ya UBUNIFU ukiacha kutokuelewa maana ya sanaa mnazuia kazi za watu na kuua ajira na vipaji vya wasanii.

Wewe Doctor wa wanyama unakuja mfanyia interview Electrical Engineer unategemea mtaelewana??

Sanaa isimamiwe na watu wanaoielewa na siyo tu kuangalia vyeti ambavyo vimetolewa na vyuo vyetu ambayo nao elimu yao mpaka sasa inapigiwa makelele haina tija kwa Graduate.

Hii nchi:-

1. Kuna watu wana malengo makubwa na wanapoanza tu utekelezaji huwa wanazimwa chini kwa chini na watu ambao hata uelewa na mambo husika hawana. Wanasiasa wengi, viongozi wachache.

2. Kuna watu wanafanya vitu vya msingi sana katika jamii ila akianza kukusimulia vipingamizi anavyokutana navyo kutoka taasisi husika unaweza jiuliza maendeleo tunayoyataka yataletwa na wao au zile huwa ni chorus tu??


BASATA acheni wasanii wafanye kazi zao kwa amani. Wimbo wa MAMA wa msanii Nay MMEMUONEA KABISA, nimekaa kwa makini kusikiliza ule wimbo mpaka naurudia najiuliza mbona wimbo huu hauna ubaya wowote.

Wenye degree na Masters za music hatuwasikii wakifanya makubwa ila hawa vijana wabunifu wanafanya mengi sana na ndio tunaowaona. Nauliza, nyie na Masters zenu za Music mbona hamuimbi tuwaone na muwe mfano??

Ishu ya BASATA ni suala la ajabu sana. Tabia za ufanyaji kazi TRA kwenye kukusanya kodi kwa mabavu na kutishiana kupeana kesi za uhujumu uchumi, tabia hii MAMA ameikataa na sasa inarudi BASATA kuanza kutishiana kufunguliwa mashtaka yasiyokuwa na maana.

Wimbo wa MAMA unakosa gani? Nyimbo ngapi za aina hii zimekuwa zikipigwa Tanzania kipindi cha nyuma??

Watu kama Mrisho Mpoto kipindi cha Kikwete mbona walifanya kazi zao bila shida KABISA ? Ukiacha kipindi cha Magufuli ambacho wengi wamepitia magumu katika kufanya kazi zao za sanaa mfano mzuri akiwa ROMA MKATOLIKI.

Tupo Karne ya 21, mabadiliko ni mengi. Taratibu za miaka ya 70 huko ziacheni na kama hamuwezi ziacha, wapeni vijana wa kizazi hiki wachukue hizo nafasi wafanye kazi kulingana na mabadiliko ya ulimwengu kiujumla.

Kuna vitu havihitaji elimu ya degree au Masters kuvielewa.

Kinachouma unachukua kundi dogo lisilojua muziki ndio wanasikiliza kazi za wasanii Nguli na kufanyia maamuzi, acheni dharau aisee.

Ngoja tusubiri tarehe 8 mtatoa maamuzi gani. Ila muelewe tu hamna wimbo unasambaa kwa kasi kama wimbo wa MAMA, mmeufungulia njia.
 
BASATA imepewa nguvu kisheria,ni taasisi ya serikali, hakuna msanii anaweza kuamua eti najitoa,ni Sawa Na mfanyibiashara aseme mimi najitoa TRA
 
Back
Top Bottom