Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,696
- 40,722
Habari ambazo zimeingia sasa hivi ni kuwa wananchi wa jamii ya Kimasai huko Kilosa wamejikuta wakichomewa nyumba zao kwa amri ya Mkuu wa Gereza la Mbigiri. Amri hiyo imetekelezwa bila kufuata sheria baada ya wananchi hao kudaiwa kuwa wamevamia eneo la gereza hilo. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Said Kalembo amemtaka Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro kumwajibisha Mkuu wa Gereza hilo kwa kuchukua sheria mikononi. Bw. Kalembo amesema kuwa "wananchi hao ni wananchi wenzetu na nchi hii ni yetu sote, na tusiwafanye wajihisi wako nchi nyingine". Mkuu wa Mkoa alidai sheria ni lazima zifuatwe na viongozi wa gereza hilo wangetumia muda kuwaelewesha wananchi juu ya eneo hilo badala ya kwenda na kuwachomea nyumba zao.
Hili ni suala jingine ambapo serikali inatumia nguvu zaidi katika masuala yanayohusu ardhi. Huko nyuma serikali kule Mkoani Mara iliwahi kuwachomea wananchi nyumba zao kiasi cha Tume ya Haki za Binadamu kuamua kufanya uchunguzi. Sakata la Buzwagi na lile la Bulyankulu bado yamo mawazoni mwa watu. Ni hatua gani zichukuliwe kwa wahusika hasa ukizingatia kuwa mapema mwaka jana viongozi wa magereza kule Ukonga waliamua kwenda kuwahamisha watu toka kwenye nyumba zao licha ya kesi kuwepo Mahakamani ambapo waandishi kadhaa walijikuta wanajeruhiwa..