News Alert: Vurugu za Kenya, CCM yachukua msimamo

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,378
39,319
Mapema leo Katibu Mwenezi wa CCM Bw. John Chiligati amezungumzia kuhusu hali ya kisiasa ya Kenya na msimamo wa CCM. Pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Bw. Membe naye amezungumzia sakata hilo. Habari hiyo ipo kwenye Breaking News sasa hivi... kwenye KLH News of course..
 
Huu ni usanii mwingine. Wanadai hawawezi kukaa kimya wakati vurugu zimeanza wiki nzima iliyopita na walikuwa hawajui la kuzungumza mara Kikwete kenda kumuona M7 mara hivi mara vile.

Nchi nyingi duniani zimetoa kauli zao kuhusiana na machafuko ya Kenya, sisi kama majirani tulinyamaza wiki nzima halafu leo wanadai hawawezi kukaa kimya!!! :confused:

CCM, ni lini mtaacha usanii wenu!? Watanzania tumechoshwa na usanii usiokwisha.Sunday, 06 January 2008
Chama cha Mapinduzi nchini Tanzania leo kimetoa kuhusu hali ya machafuko ya kisiasa yaliyotokea nchini Kenya baada ya Uchaguzi Mkuu wa Disemba 2007.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Dar-es-Saalam Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Bw. John Chiligati alisema kwamba Chama cha Mapinduzi kimesikitishwa sana na umwagaji damu uliotokea nchini Kenya na machafuko ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya wiki sasa.

Bw. Chiligati alisema kuwa CCM haiwezi "kukaa kimya" wakati majirani zake wako katika hali mbaya ya kisiasa. Bw. Chiligati alisema kuwa wakati umefika kwa viongozi wa kisiasa nchini Kenya "wakae chini na kuzungumza" ili waweze kumaliza mgogoro huo kwa amani.

Bw. Chiligati alisema kuwa jinsi ambavyo viongozi wa kisiasa walivyoshughulikia mgogoro huu kwa kweli siyo "njia sawa". Zaidi ya yote, Bw. Chiligati alisema kuwa kwa vile Kenya ni sehemu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki basi wananchi na viongozi wa Kenya wakumbuke kuwa matukio ya umwagaji damu yanatishia kwa kiasi kikubwa ujio wa shirikisho la Afrika ya Mashariki.

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania Bw. Bernard Membe amezitaka jumuiya na wadau wote wa hali ya kisiasa nchini Kenya kumsaidia Rais Kibaki katika kutafuta suluhisho la amani nchini humo. Bw. Membe alisema kuwa ipo haja ya kuchunguza kwa kina yote yaliyosababisha uchafukaji wa kisisiasa nchini humo na mwelekeo wa kulaumu "upande mmoja" haumsaidii Rais Kibaki ambaye anajaribu kutafuta usuluhishi.

Pia, Bw. Membe alisema kuwa Rais Kibaki azungumze na viongozi wengine wote ili kuweza kutafuta muafaka unaokubalika. Kwa kauli yake hiyo mapema leo, hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa serikali ya Tanzania kumtambua Bw. Mwai Kibaki kuwa Rais wa Kenya.

naona serikali imemtambua in-directly "rais" kibaki.
huenda hii inatokana na ukweli kwamba ndiye aliyeapishwa
rasmi. hata hivyo hili pia ni pigo kwa kibaki kwani
inaonyesha wazi kwamba serikali haikuridhika na mambo
yaliyopelekea kuapishwa kwake ndio maana sio jk mwenyewe
aliyetoka hadharani na kumtambua.
 
CCM wawe makini tu ili mambo yasije yakaspill bongo.Mwenzako ananyolewa..tia maji ili usije kupata maumivu time yako ikifika!Mazungumzo Kenya yalihitajika kabla hata ya umwagaji damu na maybe before even uchaguzi mkuu!Moi na Mkapa ni the same!Kibaki anaogopa na kuwalinda kina Moi na wenzake!Instead ilitakiwa wafanye kama kule South Africa!Ukweli,makubaliano,maridhiano,na kusameheana kabla ya vurugu ni very muhimu!
 
naona serikali imemtambua in-directly "rais" kibaki.
huenda hii inatokana na ukweli kwamba ndiye aliyeapishwa
rasmi. hata hivyo hili pia ni pigo kwa kibaki kwani
inaonyesha wazi kwamba serikali haikuridhika na mambo
yaliyopelekea kuapishwa kwake ndio maana sio jk mwenyewe
aliyetoka hadharani na kumtambua.
Kumtambua Kibaki ni misscalculations!Kwani ni kujidanganya kuwa anaweza kutumia dola kuwatuliza wakenya waliochoshwa,hawaelewi nguvu ya umma!Na kitendo cha Tibaigana kuyazuia maandamano pia kinaonyesha woga wa vuguvugu hilo kuamia bongo!Ila bado ni makosa!Maandamano wanayotaka wapinzani si ya kumsapoti Odinga bali kusapoti haki ya wananchi wa Kenya ya kupewa kiongozi waliyemchagua kwa mapenzi na matakwa yao kwa kupitia demokrasia ya kupiga kura ambayo wakenya wenyewe wanandai Kibaki "KAIBAKA"
 
... Wanadai hawawezi kukaa kimya wakati vurugu zimeanza wiki nzima ...Nchi nyingi duniani zimetoa kauli zao kuhusiana na machafuko ya Kenya, sisi kama majirani tulinyamaza wiki nzima halafu leo wanadai hawawezi kukaa kimya!!!.......

Nadhani Serikali walikuwa wanasubiri na kupitia pitia JamboForums ili wajue msimamo wetu na pia wapate points....Kwa kifupi walikuwa wanasubiri kwanza JF
 
Choveki.. unajua inawezekana kuna ukweli maana Lunyungu aliuliza directly kuhusu CCM na Membe.. na leo wote wawili wamejibu..
 
...CCM chama cha mafisadi,wanawaza kuiba kura tuu kuendeleza ulaji wao,hata walichosema hakina maana yeyote na Kibaki hatawasikiliza maana hawana maana kabisa wanafiki tuu tena wezi wakubwa inabidi tuwa vote out next election la sivyo tutaendelea kuwa maskini tuu
 
Mfu kumzika mfu si kioja.

Kawaida ya mtu mwongo hujidanganya mwenyewe kwanza.

Chongo linaitwa kengeza kwa makusudi
 
Mimi siyo mwanadiplomasia wala siyo mwanasiasa. Hata hivyo nadhani ni makosa kwa CCM kuanza kuonyesha kuelemea upande mmoja wa mgogoro huo. Izingatiwe kuwa upande mmja wa mgogoro, yaani ODM, hawamtambui Kibaki kiama Rais wa Kenya, hivyo CCM kumwita Kibaki kama Rais wa Kenya ni kupingana na ODM na hivyo ku-side na Kibaki. Kama mimi ningelikuwa ndiye Chiligati, nadhani ningetoa tamko la CCM kama ifuatavyo:

"CCM imefuatilia kwa makini sana vurugu za kisiasa zilizotokea nchini Kenya hivi karibuni. Vurugu hizo zinazotokana na upande mmoja kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi wa rais zimechukua maisha ya wananchi zaidi ya 500. Tukio hilo ni la aibu siyo tu kwa Kenya yenyewe bali kwa Afrika ya Mashariki yote; vile vile linatishia amani ya eneo hili la maziwa ambapo kumeshakumbwa na migogoro mingi ya aina hii. Kwa vile Kenya ni mwanachama wa Jumuia ya Afrika Ya Mashariki, sisi CCM tuna imani kuwa Mwenyekiti wa sasa Jumuia hiyo atalishughulikia swala la Kenya ipasavyo. Hata hivyo CCM tunaamini kuwa ufumbuzi kamili wa mgogoro huo utapatikana kwa njia ya mazungumzo baina ya pande mbili zinazohusika. Tunawahimiza viongozi wa pande mbili zinazopingana huko Kenya wakae pamoja na kuafikiana namna ya kumaliza mgogoro huo bila kuonyeshana ubabe ili kuepusha umwagikaji damu za raia wasiokuwa na hatia."
 
Tulisema Warundi warekenishe Tofauti zao za kikablia ndo waje kujiunga na EAC.

Kwa hiyo na Wakenya nao warekebishe tofauti zao za ukabila ndo waje kujiunga na EAC.

Sisi Watanzania tulikuwa Right kuutilia mashaka Muungano wa Afrika Mashariki.

Mungu hafichi manyang'au wenye roho za uchu wa kuzidi Fisi na Vulture.
 
Bw. Chiligati alisema kuwa CCM haiwezi "kukaa kimya" wakati majirani zake wako katika hali mbaya ya kisiasa. Bw. Chiligati alisema kuwa wakati umefika kwa viongozi wa kisiasa nchini Kenya "wakae chini na kuzungumza" ili waweze kumaliza mgogoro huo kwa amani.

Mbona wao mazungumzo yao kuhusu mgogoro wa Zanzibar hayaishi miaka na miaka? Kilichotokea Zanzibar na kile tukionacho Kenya havina tofauti, sasa sielewi kwa nini Chiligati anajifanya kuwashauri Wakenya wafanye kile ambacho wao wameshindwa kukifanya na kukikamilisha kwa miaka kadhaa sasa. Sometimes ni busara kukaa kimya kuliko kutoa ushauri wenye mashaka.
Watu bwana!
 
Huu ni usanii mwingine. Wanadai hawawezi kukaa kimya wakati vurugu zimeanza wiki nzima iliyopita na walikuwa hawajui la kuzungumza mara Kikwete kenda kumuona M7 mara hivi mara vile.

Nchi nyingi duniani zimetoa kauli zao kuhusiana na machafuko ya Kenya, sisi kama majirani tulinyamaza wiki nzima halafu leo wanadai hawawezi kukaa kimya!!! :confused:

CCM, ni lini mtaacha usanii wenu!? Watanzania tumechoshwa na usanii usiokwisha.Sunday, 06 January 2008
Chama cha Mapinduzi nchini Tanzania leo kimetoa kuhusu hali ya machafuko ya kisiasa yaliyotokea nchini Kenya baada ya Uchaguzi Mkuu wa Disemba 2007.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Dar-es-Saalam Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Bw. John Chiligati alisema kwamba Chama cha Mapinduzi kimesikitishwa sana na umwagaji damu uliotokea nchini Kenya na machafuko ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya wiki sasa.

Bw. Chiligati alisema kuwa CCM haiwezi "kukaa kimya" wakati majirani zake wako katika hali mbaya ya kisiasa. Bw. Chiligati alisema kuwa wakati umefika kwa viongozi wa kisiasa nchini Kenya "wakae chini na kuzungumza" ili waweze kumaliza mgogoro huo kwa amani.

Bw. Chiligati alisema kuwa jinsi ambavyo viongozi wa kisiasa walivyoshughulikia mgogoro huu kwa kweli siyo "njia sawa". Zaidi ya yote, Bw. Chiligati alisema kuwa kwa vile Kenya ni sehemu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki basi wananchi na viongozi wa Kenya wakumbuke kuwa matukio ya umwagaji damu yanatishia kwa kiasi kikubwa ujio wa shirikisho la Afrika ya Mashariki.

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania Bw. Bernard Membe amezitaka jumuiya na wadau wote wa hali ya kisiasa nchini Kenya kumsaidia Rais Kibaki katika kutafuta suluhisho la amani nchini humo. Bw. Membe alisema kuwa ipo haja ya kuchunguza kwa kina yote yaliyosababisha uchafukaji wa kisisiasa nchini humo na mwelekeo wa kulaumu "upande mmoja" haumsaidii Rais Kibaki ambaye anajaribu kutafuta usuluhishi.

Pia, Bw. Membe alisema kuwa Rais Kibaki azungumze na viongozi wengine wote ili kuweza kutafuta muafaka unaokubalika. Kwa kauli yake hiyo mapema leo, hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa serikali ya Tanzania kumtambua Bw. Mwai Kibaki kuwa Rais wa Kenya.CCM ni wahuni sana. Leo Hii wanajifanya wao ni tofauti na serikali. Wanaongea kama chama. Je, kauli ya serikali ni ipi? Ni baada ya kuona kuwa watanzania wanakinyooshea kidole CCM na kuwashutumu kwa tabia ya kuhujumu matokeo na hata kuona juhudi za wapinzani kupinga kilichojitokeza kenya, eti ndo wahuni hawa wanataka kujionyesha kwenye vyombo vya habari. CCM wanajikosha tu, ni wezi wakubwa wa kura. Ni mara ngapi CCM imeipora tume ya uchaguzi nafasi ya kuajiri mawakala wa uchaguzi na badala yake nafasi hiyo kuonekana kuwa ni ajira inayotolewa na CCM? Inakuwaje mtu aliyepewa kazi na tume kupitia CCM anaweza kulinda kura za watanzania dhidi ya udhalimu wa CCM. Pia CCM katika nyakati tofauti wametumia umaskini wa waalimu wa Tanzani kuwatumia kama vyombo vya kuwaweka madarakani kila uchaguzi. Ni ngumu sana kuishinda CCM kwenye chaguzi ndogo, maana uhamisha watu toka eneo moja kwenda kupiga kura eneo jingine. Watu hao upelekwa kama vikundi vya burudani. Hata Zanzibar ilijitokeza hili la Watu wa msumbiji kuandikishwa huku wapemba wakizuiliwa kwenda Zenji kupiga kura. Leo wanaona Kibaki Kibaka.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom