News Alert:... "Tunahitaji Msaada" - Mwakyembe !!

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Muda mfupi ujao nitazungumza na mmoja wa wabunge ambao majimbo yao yameathiriwa vibaya na mvua kubwa ambazo zimesababisha mafuriko makubwa. Mafuriko haya licha kuleta madhara kwa makazi ya watu lakini kwa kiasi kikubwa yamefuta mazao na shughuli zote za kilimo katika majimbo hayo kiasi kwamba mwaka huu wawezekana kabisa ukawa wa njaa ambayo chanzo chake siyo ukame bali mvua nyingi...
2008-04-12T18_55_53-07_00.jpg
Wakati tunapigia kelele ufisadi katika ofisi na taasisi mbalimbali, kwa wenzetu walioko katika majimbo haya wanachojali sasa hivi ni mablanketi, vyandarua, mahali pa kulala, na chakula. Pindi nikikamilisha mahojiano hayo yatarushwa baadaye ili sisi kama Watanzania tuwe tayari kutoa msaada unaowezekana.

Sasa hivi baadhi ya wabunge hao wameanza kuomba misaada toka kwa wafadhili na watu wa nje (wazungu) ili watuonee huruma. Je sisi Watanzania tulioko nje tunaweza kujitokeza kusaidia wananchi wenzetu waliopatwa na mafuriko? Au ni rahisi kulaumu kuhusu ufisadi lakini ukifika wakati wa kuhesabiwa tunafyata na kugwaya kana kwamba siyo sisi tunaozungumza?

Wakati wa maneno umepita (ndivyo nilivyosema mwishoni mwa mwaka jana); mambo ya kulaumu tu hayatoshi; mambo ya kujifanya tuna haki zaidi kuliko walioko nyumbani nayo haitoshi; wakati wa kujifanya tunajua siasa zaidi na Katiba zaidi, na sheria zaidi nao umepitwa; kwa mtu mwenye njaa na asiye na mahali pa kulaza kichwa chake la muhimu siyo EPA, RADA, TAnesco n.k kwake ni nani rafiki yake wa kweli wakati wa dhiki!

Je wana JF mtasimama mkiitwa na mmojawapo wa wabunge hawa kutoa msaada siyo wa "hali" bali wa "mali"! Misaada ya "hali" ni kama picha ya samaki ukutani kwa mtu mwenye shida.

Ndugu zangu kinachoendelea sasa hivi ni Katrina yetu kwenye majimbo hayo.

Natoa changamoto!!...
 
Hapo taabu ya kusaidia ndo inaibuka.

Ni wabunge wangapi watafikisha michango yetu kwa walengwa?

Kama wanashindwa kuongea na kuonyesha misimamo yao na kulaani ubadhirifu wa fedha za umma Bungeni ni vipi sasa wanadhani wanaweza kuaminiwa kwenye ukusanyaji misaada?

Maneno ya wabunge na vitendo vyao havikai chungu kimoja.

Binafsi sioni shida kuchangia maafa.
Shida kubwa niliyonayo ni uhaba wa wachangishaji waaminifu na moja kati ya kundi la watu waliokosa uaminifu na shukurani ni wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao siku zote wengi wao wanadhani wao ni wawakirishi au ni moja kati ya viongozi wa serikali.
 
Madela hujamjua Mbunge nitakayezungumza naye na atakayeomba msaada sidhani kama ni haki au busara kuhukumu kabla..
 
Madela hujamjua Mbunge nitakayezungumza naye na atakayeomba msaada sidhani kama ni haki au busara kuhukumu kabla..

Kama wana JF wanatoa misaada afadhali ifikishwe na wana JF wenyewe. Hao wabunge hawataifikisha yote.

Mwanakijiji, usidanganywe na umaarufu wao majukwaani, ufisadi ni mkubwa kuliko unavyodhani.

Kama kuna watu wanataka kusaidia basi kutumike njia zingine na sio through hawa wanasiasa.
 
Nimetoka kuzungumza na Dr. Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela na ameelezea ni jinsi gani misaada inaweza kutolewa. Nitawarushia mahojiano yangu naye within the hour.
 
MKJJ
Nia yako ni nzuri lakini its a shame kwamba hii misaada lazima ipitie kwa viongozi ambao wameweka maslahi yao mbele kuliko yale ya wananchi.
Kama sikosei in 2005 kulikuwa na njaa katika baadhi ya wilaya- Same na Shinyanga nakumbuka zilikuwa ni baadhi ya sehemu zilizoathirika vibaya.Yalitolewa mahindi ya msaada ili yagawanywe kwa wananchi lakini it turned out to be another scandal, kuna wakurugenzi na wakuu wa wilaya walipoteza kazi zao kwa suala hili.
Sasa you can imagine kama mahindi tu,tena yaliyotolewa na serekali,yanapigwa bei na hayafiki kwa wananchi- nini kitatokea kwa michango inayotolewa na watu walioko nje, na most of it itakuwa in form of cash?
 
Kama hali ndiyo hii watu wanakula misaada iliyokusudiwa kwa wenye matatizo basi Tanzania tuna safari ndefu kufika kwenye maendeleo ya kweli...
 
Kwani hatuna Red Cross....?

Ndugu yangu hii tabia kuwa kila tupatapo matatizo basi tusubiri kusaidiwa naomba uiondoe kichwani mwako manake hakuna msaada wa bure. Itatugharimu zaidi, cha muhimu tujitume wenyewe na atakayeiba tumwajibishe hata kwa kumzomea ni mwanzo mzuri pia..
 
nimeangalia post yangu ya awali nione kama kuna mahali nilisema michango ipitishiwe kwa mbunge..... bado naangalia.. labda lugha hii imekuwa ngumu kidogo kwangu.. sorry.
 
Vipi ile dola milioni moja ya Chenge haiwezi kutusaidia saidia wakati tunaendelea kujipanga kwa michango zaidi?
 
Vipi ile dola milioni moja ya Chenge haiwezi kutusaidia saidia wakati tunaendelea kujipanga kwa michango zaidi?

Was abt to say the same thing...wakiuza nyumba za Balali since hatujui aliko, Crib ya Mgonja LA pamoja na 1 mill ya chenge im sure hili tatizo dogo litapita!!!
 
Kama pesa za kupigana vita COMORO zipo then i dont think pesa za kutatua hili zitakuwa tatizo kuzipata

zote ni kodi za walala hoi

by the way tunataka ripoti za matumizi BUSHA lipokwenda Tanzania
 
hayo ya Comoro ya wengine na mambo ya Bush ya wengine (kuna mada zake). Kama hujisikii kusaidia kaa pembeni tu; kwani kwa mtu ambaye hana pa kulala kumwambia aulizie mambo ya Komoro au habari za Bush ni kutrivialize the gravity of the situation. Unapoangalia mambo yote kwa mwanga wa siasa unaweza kujikuta unapoteza ubinadamu.
 
hayo ya Comoro ya wengine na mambo ya Bush ya wengine (kuna mada zake). Kama hujisikii kusaidia kaa pembeni tu; kwani kwa mtu ambaye hana pa kulala kumwambia aulizie mambo ya Komoro au habari za Bush ni kutrivialize the gravity of the situation. Unapoangalia mambo yote kwa mwanga wa siasa unaweza kujikuta unapoteza ubinadamu.

Yashakuwa haya tena?

nilikuwa naulizia tuu kuwa je kama pesa za kuvamia nchi nyingine zipo kwanini tukose pesa la jambo kwenye cnhi yetu wenyewe?

Na mbona taarifa za matumizi wakati wa ziara ya Busha hayajatolewa mpaka leo?

zote hizo ni pesa za walipa kodi

lakini kama kuuliza ni kosa, basi tuwiane radhi mheshimiwa

 
hapana hakuna kibaya, nilishangazwa kuwa hukuguswa na plight of our people in these flooded areas nor show any sense of concern over their welfare... lakini ukaamua kuchomekea mambo ya Komoro na Ziara ya Bush na hivyo kuonesha kipaumbele ulichonacho na labda bila ya shaka kwa haki kabisa. Nadhani ilikuwa misplaced kwenye mada hii tu. Vinginevyo I share your sentiments..

Hakijaharibika kitu mheshimiwa; niwie radhi kama nimeovereact..
 
hapana hakuna kibaya, nilishangazwa kuwa hukuguswa na plight of our people in these flooded areas nor show any sense of concern over their welfare... lakini ukaamua kuchomekea mambo ya Komoro na Ziara ya Bush na hivyo kuonesha kipaumbele ulichonacho na labda bila ya shaka kwa haki kabisa. Nadhani ilikuwa misplaced kwenye mada hii tu. Vinginevyo I share your sentiments..

Hakijaharibika kitu mheshimiwa; niwie radhi kama nimeovereact..

La hasha Mwinyi wangu

sikuzote mkubwa huwa hamuombi radhi mdogo hata kama ndio kakosa

yote ni khishma yangu kwako
 
Juzi Pinda katoa/kakopesha 3billions kwa TRL.......huyu anayo pia bajeti ya maafa....hata hivyo kujitolea ni moyo.....hivyo wanaJF shime tunyoshe mkono pale tunapoweza.........sidhani kama serikali pekee itafanikisha hili bila ushirikiano wetu pia..........naamini kuna watu hapa tayari wameshaanza juhudi hizo.......Mungu awajalie sana
 
Hivi kwanini Wamarekani waliwachangia ndugu zao wa New Orleans wakati taifa hili ndilo lenye nguvu zaidi ya kiuchumi? au wana utu zaidi na wanawajali wenzao zaidi. Or are they morally superior to the rest of the humanity?
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom