News Alert:... "Tunahitaji Msaada" - Mwakyembe !!

Status
Not open for further replies.
Mwanakijiji tuko pamoja kwa hili ila binafsi nisingependa kuhukumu ila tuangalie njia muhimu za kufikisha moja kwa moja na nahisi hiyondio malalamiko ya wengi hapo juu...kuna wengi wanchukua michango hawafikishi inapotakiwa kakayangu na mwisho kutoleta maana ya kuchangisha na hivyo sawa na kuchangia NGO,,,BADO nasubiri kuona means ya kutuambia jinsi ya kuzifikisha moja kwa moja...kaka wabunge madiwani ni sumu ya mamba...kwenye michango..afadhali sumu ya panya unaweza kunywa maziwa ukatoka...mwana kijiji tuko pamoja kwa hili tusaiiane kuwaokoa wengi wameathirika na mvua..na tunavyoongea wala si mbali hapo ruvu kuna nyumba zaidi ya 15 zilikuwa za udongo zimeyeyuka..na watu wanaishi mashuleni...fwtailia hili...
mungu awalinde na magonjwa
 
Mkuu Mwanakiji, thread yako very humanitarian. Ni ya Utu na Utanzania hasa. Lakini majibu yanayopatikana humu, mengi yao (si yote) very discouraging, na yanaonyesha tabia zetu halisi wabongo. Majibu Haya hayatutofautishi na tabia za viongozi wetu tunaoona wanatenda ndivyo sivyo kwa taifa hili la walala hoi. Au pengine ni kwa sababu wengi wetu humu ni "Analysts", na hatuguswi na Actions?

 
Jamani kikubwa hapa itazamwe hawa wenzetu waliopatwa na gharika watawezwa kusaidiwa vipi.Tuachane na ushabiki wa kisiasa!wenye uwezo tuanze kutoa michango yetu
 
Jamani kikubwa hapa itazamwe hawa wenzetu waliopatwa na gharika watawezwa kusaidiwa vipi.Tuachane na ushabiki wa kisiasa!wenye uwezo tuanze kutoa michango yetu

Labda suala la msingi hapa ni kujadili namna ambavyo tunaweza kuwakilisha misaada yetu directly kwa wananchi bila kuipitishia kwenye mikono ya viongozi wa serekali. Naamini wengi tuna nia ya kusaidia lakini hofu yetu ni kwamba misaada yetu haitawafikia walengwa.
 
Mwanakijiji,

Kwa taarifa tu hiyo Kyela Development Fund ni NGO ya Mbunge wa Kyela. Mkiamua kupitishia huko ni sawa tu na mungempatia yeye mwenyewe.

Nimeona nifafanue hilo kwasababu ninalijua baada ya kuona kwamba wana JF wengi wana wasiwasi na misaada kupitia kwa wanasiasa.

Hiyo NGO ina wana Kyela wengine lakini ni katika wale wafuasi wa Mbunge. Kama mnaona hilo sio tatizo basi mnaweza kupitishia kwenye hiyo Kyela Development Fund.
 
Nafikiri lilojema ni kutafuta njia mwafaka kuhakikisha misaada inafikia walengwa...... si lazima kila mwanasiasa awe mwizi.... nashindwa kuamini kuwa mtu mwenye ...kianzio cha DR aweza kuwa mwizi kwa misaada ya wenye shida.cha msingi siasa iondolewe kwenye janga hili likabiliwe vema na kila aliyeguswa nalo.DR H.MWAKYEMBE ANAWEZA akawa mkusanya michango ya jimbo lake,cha msingi yeye mwenyewe awe na dhamira na amaanishe kweli
 
Nimetoka kuzungumza na Dr. Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela na ameelezea ni jinsi gani misaada inaweza kutolewa. Nitawarushia mahojiano yangu naye within the hour.

Wana JF,

Mimi ninaomba tuungane na juhudi za Mwanakijiji ili kutoa msaada hata kama utakuwa kidogo.

Mimi ninaijua Kyela na kwa ninayoambiwa ni kwamba hali ni mbaya sana.

Kama tatizo ni namna ya kufikisha misaada, mimi nitakuwa tayari kusaidia kupitia connections zangu kuhakikisha kila senti inafika pale ambapo JF mtasema ifike bila gharama ya ziada. Kama kuna gharama basi mimi naweza kusaidia. Pia jina langu halitaonekana popote na badala yake JF ndio watakuwa watoaji.

Ni muhimu kuweka haya wazi ili kuondoa conflict of interest.

Kama mtaona zipitie kwenye hiyo Fund pia ni sawa lakini ninawaomba tujitolee. Mimi nimeshajitolea kupitia jumuia zingine lakini nitachangia pia kupitia JF kama tutakubaliana juu ya hili.
 
Jamni kutoa ni moyo .sasa kama tutaendelea kusema zitaliwa zitaliwa .kwa hiyo tuache ndugu na jamaa wakiendelea kuteseka kwa ajili hiyo?
 
Mimi nitawasilisha hapo; Kulingana na website ya Kijiji ilivyosema.


Kyela Development Fund MNB Bank House Acct No: 2013300198

Au Wasiliana na Dr. Mwakyembe kupitia simu Namba: 255 754 284130


Hayo mengine ya kuchanganya madesa nawaachia wataalamu wa ku-spin
 
Mimi nitawasilisha hapo; Kulingana na website ya Kijiji ilivyosema.


Kyela Development Fund MNB Bank House Acct No: 2013300198

Au Wasiliana na Dr. Mwakyembe kupitia simu Namba: 255 754 284130


Hayo mengine ya kuchanganya madesa nawaachia wataalamu wa ku-spin

What about Same, Vunjo and other places? Au ndio kila mtu anavutia kwake? Its going to be such a great inconvinience kama hizo sehemu zilizoathirika zitachangiwa separately. UKABILA pia unaweza kujipenyeza kwa utaratibu huu.
 
What about Same, Vunjo and other places? Au ndio kila mtu anavutia kwake? Its going to be such a great inconvinience kama hizo sehemu zilizoathirika zitachangiwa separately. UKABILA pia unaweza kujipenyeza kwa utaratibu huu.

Ifike mahali JF iwe na uwezo wa kusimamia baadhi ya mambo yenyewe. Mchango kama huu ungesimamiwa na JF, basi ingelikuwa rahisi kugawa pesa kiasi gani ziende wapi na pia rahisi kuhakikisha zinawafikia walengwa.

Hakuna kitu kibaya kama kusikia pesa kama hizo zaidi ya nusu zinaliwa njiani kabla ya kufika kwa wananchi. Hiyo ndio reality ya TZ, hatuwezi kuikwepa.
 
Nakubaliana na mawazo ya wote hasa suala la kuangalia ni jinsi gani fedha zitatumika. Kama mmepata nafasi ya kumsikiliza Dr. Mwakyembe amesema wazi kuwa mchakato mzima utakuwa transparent ili kujenga imani, kwani maafa hayaji mara moja.

Lakini kama kuna mtu anafikiri there is a 100 % way to stop any amount of money from being misdirected or misused anajipa moyo mno. Kwa ufupi hakuna as long as the other side there is another human being involved.

Kwangu nafikiria which is the least possible way ambayo inaweza kusaidia misaada hiyo. Dr. Mwakyembe kajikomiti hadharani kuwa:

a. Fedha yote itajulikana
b. Mapato na matumizi yote yatajulikana
c. Na masalio ya fedha yatajulikana .

What else can we ask? Naomba msikilize maelezo yake kwa sababu nimemuuliza hili swali directly kwa sababu na mimi nimetuma fedha yangu na siko katika mchakato wa kutupa fedha ovyo; lakini siwezi hata kidogo kuacha kutenda kwa sababu ninasita sita; Taifa haliwezi kujengwa na watu wasiochukua risk; that is part of leadership.

Kuhusu sehemu nyingine, kote kunahitaji msaada lakini kwa upande mmoja sijui ni kwa kiasi gani wabunge wa Same na Vunjo au maeneo mengine wameuza matatizo yao na kuomba misaada. Lakini anayetaka kusaidia au kutokusaidia kwa sababu ya ukabila sidhani kama kuna njia ya kumsaidia yeye mwenyewe maana binadamu tuna motivations za ajabu sana.
 
Hapo taabu ya kusaidia ndo inaibuka.

Ni wabunge wangapi watafikisha michango yetu kwa walengwa?

Kama wanashindwa kuongea na kuonyesha misimamo yao na kulaani ubadhirifu wa fedha za umma Bungeni ni vipi sasa wanadhani wanaweza kuaminiwa kwenye ukusanyaji misaada?

Maneno ya wabunge na vitendo vyao havikai chungu kimoja.

Binafsi sioni shida kuchangia maafa.
Shida kubwa niliyonayo ni uhaba wa wachangishaji waaminifu na moja kati ya kundi la watu waliokosa uaminifu na shukurani ni wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao siku zote wengi wao wanadhani wao ni wawakirishi au ni moja kati ya viongozi wa serikali.

Hawa wabunge wanafiki nani anawaamini! Watakusanya michango na kupeleka kwa waathirika kidogo tu halafu asilimia kubwa watie vibindoni mwao.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom